Melfu ya waombolezaji walijitokeza kwa mazishi ya mwandishi mashuhuri wa
nchi hiyo marehemu Chinua Achebe, katika jimbo la Anambra.
Wageni mashuhuri akiwemi, rais Goodluck Jonathan pia hawakuachwa nyuma,
Mamia ya watu walikusanyika kanisani baadhi wakivalia mavazi ya kitamaduni yenye picha ya Achebe.
Marehemu Achebe alisifika sana kama baba mwanzilishi wa fasihi ya kiingereza barani Afrika.
Mwili wa mwandishi mashuhuri wa vitabu barani Afrika Chinua Achebe
uliwasili nyumbani kwake katika jimbo la Anambra nchini Nigeria siku ya
jumatano.
Mwandishi wa BBC aliyekuwepo kwenye mazishi hayo alisema kuwa Achebe alipewa mazishi ya kiheshima, mjini Ogidi.
Hata hivyo, baadhi ya mambo aliyochukizwa nayo ikiwemo vubaraka wa
kisiasa na mali wanayojilimbikizia, yalishuhudiwa katika mazishi yake.
Wanasiasa walisindikizwa kanisani na maafisa wa usalama wakiwa na
sialaha za kisasa. Baadhi pia waligika wakiwa wamavalia mavazi yenye
rangi ya vyama vya kisiasa.
Hafla mbali mbali ziliandaliwa nchini Nigeria kumuenzi bwana Achebe kabla ya mazishi yake kufanyika.
Mwandishi huyo mashuhuri alifariki mjini Boston,Marekani, akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Hayati Achebe, anasifika sana kwa kuwa mwanzilishi wa fasihi ya kiafrika kwa kiingereza.
Kitabu chake alichokianda cha kwanza, mwaka 1958, 'Things Fall Apart',
ambacho kilizungumzia sana athari za ukoloni barani Afrika, aliweza
kuuza zaidi ya vitabu milioni kumi.
Mwandishi huyo na msomi, aliendelea na uandishi wake na kuandika vitabu
vingine 20 baadhi vikikosoa sana wanasiasa na kile alichokitaja kama
ukosefu wa uongozi nchini Nigeria.
Alikuwa anaishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 baada ya ajali ya barabarani kumjeruhi kiasi cha kumlemaza.
Makundi ya kitamaduni yalifanya tamasha mbali mbali nje ya uwanja wa
ndege wa Enugu, huku ndege iliyokuwa inambeba marehemu Achebe ilipotua.
Inaarifiwa kuwa licha ya kuwa watu wana majonzi tele, lakini pia wanasherehekea maisha ya mwandishi huyo.
Achebe atazikwa karibu na nyumbani kwa familia yake mjini Ogidi, mji mdogo kwenye vilima vya jimbo la Anambra
No comments:
Post a Comment