Edward Snowden aliyefichua siri za Marekani
Snowden, ambaye alifichua siri hiyo akiwa Hong Kong ametoweka baada ya kuondoka ghafla kwenye hoteli alimokuwa anaishi.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 29 alisema kuwa aliamua kutoa siri hiyo akiwa na lengo la kuwakomboa watu duniani kutoka kwa serikali ya Marekani na kuonesha nchi yake kuwa ni sharti iheshimu haki na uhuru wa watu.
Ilibainika wiki iliyopita kuwa idara ya ujasusi nchini Marekani ilikuwa inakusanya Mamilioni ya rekodi za simu na pia imekuwa ikichunguza watumizi wa mitandao.
Idara ya ujasusi nchini Marekani imesema kuwa hatua ya Snowden kutoka siri hiyo ni kosa kubwa la kihalifu na anafanyiwa uchunguzi ili kufunguliwa mashtaka.
Awali Snowden aliomba kupewa hifadhi katika kisiwa cha Iceland kutokana na ufichuzi wake ambao anaamini utamweka matatani baada ya kutoa siri ya serikali.
Ufichuzi huu umezua mjadala nchini Marekani kuhusu mpango wa serikali kuyataka kuchunguza mitandao suala ambalo wanasema ni kuingilia uhuru wa watu.
No comments:
Post a Comment