Pages


Photobucket

Thursday, May 16, 2013

Zitto: Pendekezo binafsi kuzuia unyonyaji dhidi ya Wasanii wa Tanzania katika Biashara ya Miito


 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisVExU3V0yykEVEWhc7SXTH64m6GFnyNgPZcZieucYcEVGHKBhFEq-Zsvjz_iVwrDuSK3ttttFg7KrcxLbSBGVwvkBWsonGiJ2LlndQ1NfYbkChduI27T3_0c9JuiEcKprQnt9MIGa7tA/s1600/Zitto-Kabwe.jpg
 PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES) Kwenda kwa: DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara Kuhusu: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES) Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.

No comments:

Post a Comment