Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini
Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la
mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais
Kikwete alikuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amekatiza ziara hiyo na
anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na
wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni
mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni
ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi
mjini Kuwait.
Aidha,
Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa
na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad
Al Sabah.
No comments:
Post a Comment