Mtoto
Mwita Matinyi (pichani kushoto), Jumapili iliyopita alipata furaha
kubwa baada ya kutwaa ushindi wa tatu kwenye Michuano ya Nne ya Kaizen
Karate ya Kila Mwaka inayotumia mtindo wa Goju Ryu iliyofanyika kwenye
Shule ya Kati ya Kimataifa ya Silver Spring jimboni Maryland, kilomita
mbili nje ya Jiji la Washington DC. Kevin mwenye umri wa miaka tisa,
alishinda kwenye michuano ya kupigana ulingoni kwa watoto wenye mkanda
wa rangi ya machungwa. Mdogowe, Chacha Matinyi, mwenye umri wa miaka 6
(pichani kulia), ingawa hakuibuka na ushindi lakini alijitahidi na
kuacha matumaini makubwa ya kushinda mwakani. Watoto hawa walikuwa
Watanzania pekee walioshiriki michuano hiyo iliyofurika watoto wa rika
mbalimbali ambayo majaji wake wenye vyeo cha Grand Masters walikuja
kutoka California mahsusi kwa kazi hiyo. Watoto hawa wameyazima makeke
ya baba yao, Mobhare Matinyi, ambaye alikuwa akiwaringishia medali zake
alizopata enzi akiwa bondia wa light heavy weight chuo kikuu nchini
India.
No comments:
Post a Comment