Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya
Watangazaji wa Clouds FM (wote waliosimama nyuma).Reedio Clouds FM
imezindua msimu wake mpya ulioitwa TWENZETU kwa minajili ya kuielimisha
jamii kuwa na tabia ya kupenda vya kwao na kutumia fursa walizonazo
ndani ya MADE IN TANZANIA kujikwamua kimaisha.
Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniii
(wote waliosimama nyuma),mara baada ya kuzungumza nao kuhusiana na mambo
mbalimbali juu ya sanaa ya Tanzania na namna ya kupambana na maharamia
wa kazi zao,ambapo pia redio ya Clouds FM imezindua msimu wake mpya
ulioitwa Twenzetu kwa minajili ya kueilmisha jamii ya kupenda vya kwao
kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA .
Waziri Mkuu Pinda akizungumza mbele ya baadhi ya wasanii wa muziki wa
kizazi kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wadau wengine
wa sanaa waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema
leo mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka
Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua
wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa
sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.
Mh.Pinda aliishukuru kampuni ya Clouds Media Group kwa kazi nzuri
walioianzisha ya kuwasaidia vijana kwa namna moja ama nyingine katika
suala zima la kuwaamsha na kuwafungua macho na kuwaelimisha namna ya
kuziona fursa zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha,aliongeza kuwa
kupitia ujumbe huo wa MADE IN TANZANIA kinachohitajika sasa ni kupanga
ratiba nzuri ya kuliendeleza zoezi hilo ikiwemo pia kwa kuzishirikisha
taasisi nyingine zikiwemo za serikali katika kuhakikisha jambo hilo
linaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akiwakaribisha watu wote
waliofika kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,tayari kwa kumpokea mgeni
rasmi, Waziri Mkuu Pinda.
Baadhi Wadau wa Muziki na Filamu wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe
mbalimbali mapema leo kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali
iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa
upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba
na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia
kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea
Sehemu ya umati wa watu ukiwa kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka
Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua
wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe katika
nafasi ya kujikwamua kimaisha,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia
wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na
kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea
No comments:
Post a Comment