Wayne Rooney ndio mwanasoka tajiri zaidi katika wachezaji wanaocheza kwenye ligi kuu ya England akiwa na utajiri binafsi wa £51million, kwa mujibu wa list ya gazeti la Sunday Times ya wanamichezo matajiri.
Mshambuliaji huyo, utajiri wake umeongezeka kutoka £45m mwaka uliopita, na sasa amempita kiasi cha £9m mchezaji mwenzie wa Manchester United Rio Ferdinand. Rooney na mkewe Coleen kwa pamoja wana utajiri wa £64m.
Rooney na Ferdinand ni miongoni mwa wachezaji 24 wa Premier League waliopo katika listi ya wanamichezo matajiri wa Uingereza na Ireland.
David Beckham ndio mwanamichezo tajiri zaidi U.K akiwa na utajiri £165m.
Staa wa Formula One Lewis Hamilton na mwenzie Jenson Button wapo katika 10 bora huku Lewis akiwa na £60m na Button akiwa na £58m.
Michael Owen (£38m) anashika nafasi ya tatu katika wanasoka matajiri wa EPL, akifuatiwa na Ryan Giggs na Frank Lampard (wote £34m).
Kuna wachezaji sita wa Manchester United katika listi, wakiwemo Paul Scholes, Michael Carrick na Robin van Persie, ambaye ndio ameingia kwenye listi hiyo akiwa na utajiri wa £12m.
Steven Gerrard ndio mchezaji wa Liverpool tajiri kuliko wote akiwa na utajiri wa £33m, Carlos Tevez (£18m) ndio anawaongoza Manchester City katika listi.
No comments:
Post a Comment