Wiki kadhaa
baada ya shirikisho la soka duniani kutuma ujumbe wake kuja kufuatilia
suala la uchaguzi mkuu wa TFF uliogubikwa na matukio kadhaa ya utata,
leo hii shirikisho hilo la soka duniani limetoa maamuzi ya mchakato wote
wa uchaguzi mkuu wa TFF kuanza upya, kwa maana wale wagombea wote
waliokatwa wanaweza kurudi kwenye mchakato wa uchaguzi.
Taarifa
nilizonazo FIFA imeshatuma barua ya kuelezea uamuzi kwa TFF na muda
mchache ujao TFF inatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu uamuzi huo wa
FIFA.
Kwa taarifa zaidi kuhusu suala hili endelea kutembelea ....www.shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment