Chama
cha Wafanyakazi wa Reli nchini (Trawu), kimeitaka Serikali kuongeza
kiwango cha mishahara kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL),
vinginevyo kitaisimamisha treni ya abiria maarufu kama treni ya
Mwekyembe. Akizungumza
kwenye mkutano na wafanyakazi wa TRL jana jijini Dar es Salaam, Katibu
Mkuu wa Trawu Taifa, Erasto Kihwele, alisema kuwa wafanyakazi
wamechoshwa na mishahara midogo wanayolipwa kwa miaka 15 sasa bila ya
nyongeza.
Kiwhele
alisema kuwa ni miaka 15 sasa toka Serikali ilipopandisha mishahara kwa
wafanyakazi wa shirika hilo kutoka Sh. 50,000 mpaka 205,000 wakati
gharama za maisha zimepanda huku wafanyakazi wa kada nyingine
wakiongozewa mishahara kila wakati.
Aliongeza kuwa uongozi wa Trawu umeamua kwenda Dodoma kwa lengo la
kuonana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili kuzungumza naye kuhusu
mustakabali wa nyongeza ya mishahara ya wafanyakzi wa kampuni hiyo.
“Kwa kweli safari hii tumeamua endapo hawatatupandishia nyongeza ya
mishahara kwa asilimia mia moja tutaweka vitendea kazi chini na kuanza
mgomo wa nchi nzima ili kuishinikiza Serikali,” alisema.
Alisema wameazimia kwenda Dodoma kuonana na Pinda baada ya kuona Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Naibu wake kushindwa kutatua
matatizo yao.
No comments:
Post a Comment