Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Anne Makinda,
ameamuru kambi ya upinzani kuyaondoa maneno yote yaliyomo kuanzia
ukurasa wa kwanza mpaka wa 14 katika hotuba rasmi ya Kambi ya upinzani
iliyosmwa na mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu,’ ambaye
ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mh. Makinda ametoa amri hiyo baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge
kujadili hotuba hiyo na kubaini kuwa ina kauli za uchochezi; na kusema
kuwa kuwa Bunge sio sehemu kugombanisha wananchi, hivyo maneno yote ya
uchochezi hayaruhusiwi.
Katika hotuba hiyo, Mh. Mbilinyi
aliishutumu serikali kuhusika na kuteka nyara waandishi wa habari, kauli
iliyopelekea Spika Makinda kuahirisha Bunge.
No comments:
Post a Comment