Hatimaye Mnyama TID ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia suala la
kukosa kutajwa kuwania tuzo za Kili mwaka huu na kudai anahisi
amehujumiwa. Akiongea exclusively na Bongo5, TID amesema ameshangaa
wimbo wake Kiuno kutoingizwa kwenye tuzo hizo ilhali ulifanya vizuri
kwenye redio na kwenye TV.
“Waliniita before hata hizo nominations na nini, mimi nilikuwa
safarini nikashindwa kufika na tayari nilishaongea na Kavishe tulikuwa
gym tukakubaliana kwamba hizi issue ziishe sasa nashangaa kwenye
nominations sijawekwa na wimbo wangu sijui maana yake nini,” amesema
TID.
Amesema hawezi kuilaumu academy inayochagua nominations hizo kwakuwa hupelekewa majina.
“Hapo kuna kauli imetoka ya mtu mwingine ambaye amekataza nisiwekwe,” amesisitiza.
Amesema tayari alishakubali kuziweka tofauti zake na waandaji wa tuzo
hizo pembeni ili kuanza ukurasa mpya lakini haelewi ni kipi
alichowakosea mara nyingine.
“Kwanini sasa wasiniweke, nini kitu kibaya nilichofanya mimi? Nahisi
kuna mchezo kwasababu wimbo wangu ulitakuwa uingie kwenye categories
kibao na ushinde sababu umehit sana mwaka jana.”
Msikilize zaidi hapa.............................
No comments:
Post a Comment