KAJALA KUIGIZA FILAMU YA MAISHA YAKE HALISI SEGEREA, APONGEZWA NA KUPONDWA.
News is that actress Kajala Masanja anatarajia kucheza katika filamu
ambayo itaelezea maisha yake halisi ya kesi yake iliyokuwa ikimkabili.
filamu hiyo itaelezea tangu mwazo wa issue hilo, mahakamani, segerea
mpaka anatoka baada ya Wema Sepetu kumtolea faini ya sh. millioni 13.
Kajala mwenyewe amesema ni kweli na kwasasa story na script ndiyo
vinafanyiwa kazi. Hata hivyo wadau wanaweza kuwa na hamu ya kuiona
filamu hiyo kama kweli itafanikiwa kuonyesha mazingira halisi ya
mahakamani na segerea kama ilivyokuwa kwa mwigizaji huyo kabla ya kuwa
uraiani ikichukuliwa kwamba bado ni shida sana kupata location katika
taasisi za serikali hasa huko segerea ambako Kajala mwenyewe aliwahi
kusema kuna mambo ya kuhuzunisha sana.
Kwasasa inadaiwa Kajala anafanya filamu ya Princess Sasha chini ya Wema
Sepetu huku tayari baadhi ya watu wakisema Kajala ana haraka sana
pengine ameburuzwa na watu kuhusu kucheza story ya kesi yake kwakuwa
bado mumewe yupo jela hajatoka lakini tayari yeye amepanga yake huku
uraiani. Shabiki mmoja amesema " i think Kajala bado hajashauriwa vizuri
kwa time hii kucheza maisha yake halisi hata miezi 2 bado kuisha".
mashabiki wake wengine wamesema ni poa tu apige kazi "
No comments:
Post a Comment