Pages


Photobucket

Tuesday, May 7, 2013

Jaji Eusebia Munuo awa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taifa ya Parole

JAJI EUSEBIA MUNUO
 
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Kifungu cha 3(2) (a) cha Sheria ya Bodi ya Parole Sura 400 amemteua Jaji Mstaafu Eusebia Nicholaus Munuo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kuanzia tarehe 24 Aprili, 2013. Mheshimiwa Eusebia Nicholaus Munuo ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Sambamba na uteuzi huo Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya kifungu 3(2)(f) cha Sheria hiyo, amewateua Bw.John William Nyoka na Bw. Fransis Stolla kuwa wajumbe wa Bodi hiyo. Bw. John William Nyoka ni Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu na kabla ya kustaafu kwake alikuwa Mshauri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, nchini Namibia kama Mshauri wa Magereza na Bw. Fransis Stolla ambaye ni Wakili wa Kujitegemea na kwa sasa ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(Tanganyika Law Society).
Wajumbe hawa pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkemia Mkuu wa Serikali, Kamishna wa Ustawi wa Jamii na Mjumbe mmoja kutoka Ofisi ya Rais ndio wanaounda Bodi ya Taifa ya Parole kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha Sheria hiyo.
Mbarak Abdulwakil
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

No comments:

Post a Comment