KLABU ya mastaa wa filamu jijini Dar es
Salaam, Bongo Movie ‘Bongo Muvi’ imepasuka katikati kisa kikidaiwa kuwa
ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Vincent
Honorati Lasasi Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilio
asitie miguu kwenye msiba wa baba mzazi wa mwenzao, Wema Sepetu,
marehemu Balozi Isaac Sepetu.
Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa
maombolezo ya kifo cha mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu
katika Hospitali ya TMJ kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa
nyumbani kwake, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
LAWAMA ZOTE KWA RAY
Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii
wa Bongo Muvi (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku
wengine wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na
limejaa unafiki.
Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza kumzika baba yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar.
RAY AAGIZWA AITISHE KIKAO CHA DHARURA KUMJADILI
Habari za uhakika zinasema kwamba,
wasanii waliotangaza kujiengua klabuni humo wameshamuomba Ray aitishe
kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumzia hatua yake ya kuwapiga
marufuku wasanii hao kutoshiriki msiba wa mzee Sepetu huku akijua wema
wa binadamu unapatikana kwenye kushiriki mazishi ya wenzake.
“Kikubwa zaidi ni kwamba, Ray wakati
akisambaza zile meseji alisahau kuwa kuna siku Wema aliwahi kuwaalika
wasanii wa Bongo Muvi nyumbani kwake Makumbusho (Dar) wakala na kunywa,
mbona hawakugoma kwenda?” alihoji staa mmoja aliyepinga katazo la Ray.
NJAMA ZA KUINGAMIZA KABISA BONGO MUVI ZAUNDWA CHINI KWA CHINI
Habari zaidi kutoka kwenye kundi
linalodaiwa kujimega kwenye mpasuko huo zinasema kuwa kuna njama za
makusudi za kuiangamiza klabu hiyo kwa kuwa mbali na mwenyekiti huyo
kuwazuia wajumbe wasiende msibani kwa mzee Sepetu lakini imekuwa
ikiendeshwa kitemi na kibaguzi.
Ilisemakana kuwa kuna wasanii wameifanya
klabu hiyo kama yao huku wengine wakiwa hawatakiwi hata kukohoa jambo
walilosema si sawasawa.
“Kwa mpasuko huu, wasanii waliochukizwa
na Ray wamesema nao wao wanakazia hapahapa, Bongo Muvi lazima iangamie
moja kwa moja, isiwepo tena,” alisema msanii mmoja ambaye jina lake
linapanda kwa kasi.
KISINGIZIO CHA WASANII WANAFIKI CHAPINGWA
Maumivu makali zaidi yaliibuka kufuatia
baadhi ya wasanii waliotaka kujifanya hawajapata meseji ya Ray ambapo
walisema walishindwa kushiriki msiba huo kwa sababu walikuwa ‘shooting’.
“Kuna wasanii walishindwa kuweka wazi
kwamba walipokea meseji ya katazo ya Ray, walipopigiwa simu na wenzao
kuulizwa kwa nini hawaonekani msibani kwa Wema walisingizia eti wako
location wanarekodi!
“Kwa akili za kawaida, mwenzenu kafiwa
mnaweza kushikwa na ubize wa kurekodi filamu? Hawa ni wanafiki,
walisingizia vile ili ionekane wana hudhuru,” alisema staa mwingine.
MAMA WEMA ASHTUSHWA
Akizungumza na waandishi wetu kwa mara
ya kwanza baada ya kusikia mwanaye alisusiwa msiba wa baba yake, mama
mzazi wa Wema, Mariam Sepetu alionesha kusikitishwa sana na kitendo
hicho.
Alisema kitendo hicho kilitokea wakati
ambao Wema au familia nzima ilikuwa inasaka faraja na si mfarakano kwa
vile kufiwa kupo na hakuna dalili wala kujiandaa.
“Nilisikitika sana, lakini siwezi kusema
mengi kwa sababu vijana wanataka mwongozo ili kwenda mbele, naamini
watakaa na kuondoa tofauti zao,” alisema mama huyo mwenye mapenzi
makubwa na mastaa wa filamu Bongo.
KATAZO LA RAY
LILISIMAMIA HIVI
Habari kutoka chanzo chetu makini
zilidai kuwa hoja dhaifu iliyotumiwa na Ray ni kwamba Wema huwa haendi
kwenye misiba ya wenzake hivyo walitaka na yeye amzike baba yake
mwenyewe.
MISIBA ILIYOTOLEWA MFANO
Ulitolewa mfano msiba wa aliyekuwa staa
wa filamu za Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2,
mwaka huu ambapo Wema alishindwa kufika kwa sababu alikuwa studio
akirekodi wimbo wake mpya ambao haujatoka hadi leo.
MISIBA ALIYOSHIRIKI
Ilidaiwa kuwa Wema huwa hashiriki misiba
ya wenzake, ikatolewa mifano misiba miwili aliyoshriki kuwa ni marehemu
Sharo Milionea (Hussein Mkiety) na (Steven) Kanumba kwa sababu alikuwa
mtu wake.
ANACHOSIMAMIA WEMA
Akizungumzia tukio la kususiwa msiba wa baba yake, Wema alifunguka:
“Nimesikitishwa na kitendo hicho naamini
hakikuwa cha haki, mimi nimekuwa nikihudhuria misibani kwa watu
mbalimbali na si kweli kwamba niko kivyangu, nimehukumiwa bure.”
RAY AINGIA ‘PANGONI’
Juzi Jumanne, Amani lilimsaka Ray kwa njia ya simu ili aelezee ukweli wa madai hayo lakini aliingia ‘pangoni’ (hakupokea simu).
Hata hivyo, katika gazeti ndugu la hili,
Ijumaa la Ijumaa, Novemba Mosi, 2013 ukurasa wa mbele ambapo kuna
habari yenye kichwa; WEMA SEPETU ASUSIWA MSIBA, Ray aliulizwa kuhusu
madai hayo ambapo alijibu:
“Mh! Kweli Wema haendagi kwenye misiba
ya watu, hata mimi sikumuona kwa Sajuki ingawa sijui kama alionekana
baadaye ila kwa sasa niko sehemu mbaya nitakupigia baadaye tuongee kwa
kirefu.”
Hakupiga.
MASTAA KIDUCHU MSIBANI
Pamoja na katazo hilo la Ray, wasanii
wengine waliamua kwenda msibani Sinza – Mori (Dar) na wachache sana
kwenye mazishi, Zanzibar.
Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na
Kajala Masanja, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’,
Jacob Stephen ‘JB’, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Salum Mchoma ‘Chiki’, Ahmed
Olotu ‘Mzee Chilo’ na Jacqueline Wolper.
WASIOFIKA MSIBANI
Wengi walimsusia msiba Wema, lakini
majina makubwa zaidi wakiongozwa na Ray mwenyewe ni Single Mtambalike
‘Richie’, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, Irene Paul, Blandina Chagula
‘Johari’, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ na Ruth Suka ‘Mainda’
Chanzo:GPL
-----------
No comments:
Post a Comment