Pages


Photobucket

Saturday, November 2, 2013

Upatikanaji Huduma za Maji Rombo Tatizo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judathadei Mboya

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judathadei Mboya
Na Yohane Gervas, Rombo
IMEELEZWA kuwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Wilaya ya Rombo imekua mbaya hasa katika tarafa za Mengwe na Tarakea. Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
ya Rombo, Anthoni Tesha katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Rombo.
Tesha alisema kuwa maeneo mengi ya Tarafa za Mengwe na Tarakea yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa huduma ya maji, hali inayowafanya baadhi ya waalimu kuvunja vipindi vya mchana na kuwarudisha wanafunzi kwenda kutafuta maji.
Aidha Tesha alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judathadei Mboya, kuhakikisha wanakutana na Meneja wa Kampuni ya Maji ya Kiliwater ili kuzungumzia suala hilo mapema.
Uhaba wa maji katika vijiji mbalimbali katika wilaya ya Rombo imeonekana kuwa changamoto kubwa hasa katika maeneo ya ukanda wa chini wa wilaya hiyo ambapo baadhi ya maeneo hupata huduma ya maji kwa mgao na maeneo mengine kukosa kabisa huduma hiyo.   

No comments:

Post a Comment