MBUNGE wa
Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amesema migogoro iliyojitokeza wakati wa
Operesheni Tokomeza Majangili haiwezi kutenganishwa na agizo la Amiri
Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete.
Mnyika
alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua mafunzo ya wajumbe na
viongozi wa CHADEMA kutoka kata 35 kati ya 37 zinazounda Jimbo la
Dodoma.
Alisema
pamoja na baadhi ya wabunge wa CCM kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki na Waziri wa Mambo ya
Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi kuwajibika, Rais Kikwete hawezi kuachwa
kando.
Alisisitiza
kuwa Rais Kikwete asiwekwe kando kwani sababu kubwa ya mifugo ya
wafugaji na wao wenyewe kuuawa, kumetokana na udhaifu wa serikali ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM), inayoongozwa na Rais Kikwete.
Mnyika
alimtaka Rais Kikwete kutonyamaza bali atoe tamko kwanini Operesheni
Tokomeza Ujangili imegeuka kuwa tokomeza mifugo na mauaji ya wafugaji.
“Pamoja na
ukweli kuwa baadhi ya mawaziri wana udhahifu katika kusimamia
operesheni hiyo, lakini Rais Kikwete naye anapaswa kujiuliza na
kuwajibika kwanini yametokea hayo na yeye amekaa kimya hadi Bunge
limefikia hatua ya kujadili jambo hili kwa uzito mkubwa?
“Haiwezekani
Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na kiongozi wa nchi akanyamaza bila
kutoa tamko, kwanini matukio hayo yametokea badala ya kupambana na
majangili askari wanapambana na wafugaji na mifugo yao,” alisema.
Akiendelea
kuzungumza na viongozi hao wa kata, Mnyika alisema CCM pamoja na
serikali yake haina nia njema na wafugaji kwani kila kinachotendeka kina
baraka ya serikali ya Rais Kikwete.
Aidha,
alisema kuna kila sababu ya viongozi wa CHADEMA kuhakikisha wanasimamia
vema mchakato wa rasimu ya Katiba mpya kwa kuhakikisha wanapiga kelele
ili Katiba mpya iwe na kipengele cha kumruhusu Mtanzania kumiliki
rasilimali ardhi.
Alisema
haiwezekani Mtanzania asiwe na uhakika wa kumiliki ardhi, kwani kwa
Katiba ya sasa ambayo ni mbovu inampa madaraka makubwa na ardhi yote ni
mali ya Rais
No comments:
Post a Comment