Waziri
Mkuu Mizengo Pinda pamoja na mawaziri wake wawili; Khamisi Kagasheki
(Maliasili na Utalii) na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk Mathayo David
wameingia matatani kutokana na shinikizo linalowataka wang’oke katika
nafasi zao.
Pinda
pamoja na mawaziri hao wanatakiwa kuachia ngazi kama hatua ya
kuwajibika kutokana na matukio ya vifo na baadhi ya watu kujeruhiwa,
katika matukio ya migogoro ya wakulima na wafugaji kwa upande mmoja na
utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Majangili kwa upande mwingine.
Jana
wabunge walicharuka na kuwataka mawaziri waliohusika katika Operesheni
Tokomeza Ujangili wawajibishwe wakieleza kutoridhishwa na maelezo
waliyoyatoa mapema jana, baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Kelele
za wabunge zilizuka baada ya wabunge kuanza kuchangia maelezo ya
Serikali kuhusu migogoro ya wafugaji na wakulima, hifadhi za wawekezaji
na maelezo ya Serikali kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili.
Aliyekuwa
wa kwanza kuchangia mjadala huo ni Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter
Msola (CCM) ambaye katika hitimisho lake alitoa hoja ya kuundwa kwa
Kamati Teule ya Bunge kuchunguza kile ambacho alikiita kuwa ni
unyanyasaji wa wafugaji na uporaji wa mifugo yao.
Profesa
Msola alielekeza shutuma zake kwa Serikali kuwa ilifanya operesheni
zake kwa pupa bila kufanya maandalizi hivyo kuwaathiri wananchi
wasiokuwa na hatia.
Spika
wa Bunge, Anne Makinda kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge jana mchana
aliridhia kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kwa ajili ya kuchunguza
migogoro baina ya wakulima na wafugaji, wakati ‘madudu’ ya Operesheni
Tokomeza Majangili yatachunguzwa kupitia Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira.
Chimbuko la hoja
Jana
asubuhi kabla ya Bunge kuanza kikao chake, Spika Makinda alitoa taarifa
kwamba Kikao cha Kamati ya Uongozi kingekutana wakati kipindi cha
maswali na majibu kikiendelea, kwa lengo la kutoa mwelekeo wa mjadala wa
hoja za dharura.
Hoja
hizo ni zile zilizotolewa na wabunge wawili kwa nyakati tofauti;
Alphaxard Kangi Lugora wa Mwibara (CCM) kuhusu Operesheni Tokomeza
Majangili na Saidi Nkumba wa Sikonge (CCM), kuhusu vita baina ya
wakulima na wafugaji.
Kamati
hiyo ilikutana baada ya kipindi cha maswali na majibu na Spika Makinda
alitoa taarifa za kusitisha shughuli nyingine, ili wabunge waweze
kujadili masuala hayo ambako kabla ya kuanza mjadala aliwaita mawaziri
kutoa taarifa zao.
Alianza
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Kagasheki ambaye katika maelezo
yake alihitimisha kwa kutangaza kusitisha Operesheni Tokomeza ili
kupitia mpango huo na kufanya maboresho ili kuondoa upungufu uliopo.
Licha
ya kueleza sababu nyingi zilizofanya Serikali kuendesha operesheni
hiyo, alisema ina manufaa makubwa katika kuokoa wanyama aina ya tembo,
lakini waziri alihitimisha kwa kusema itakuwa ni busara kuifanyia
tathmini wakati ikiendelea, hivyo kutangaza kuisitisha mara moja.
Kwa
upande wake Dk Mathayo alitoa maneno ya kuomba radhi na kuwapa pole
watu waliopatwa na usumbufu ikiwa ni pamoja na kupoteza mali zao na
mifugo.
Mathayo
aliwaeleza wabunge kuwa Serikali imepanga kujenga malambo katika maeneo
mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wafugaji kupata maji ili kupunguza
safari za kuhamahama kutoka eneo moja kwenda jingine.
Shinikizo kwa Pinda
Baada
ya kumaliza hotuba zao, wabunge kadhaa walipata nafasi ya kuchangia
maelezo hayo huku wengi wakielekeza shutuma zao kwa mawaziri hao na
wenzao wa Mambo ya Ndani ya Nchi na yule wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa.
Wabunge
wawili wa Chadema, Paulina Gekul (Viti Maalumu) na John Shibuda (Maswa
Mashariki) walitaka Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu kutokana kushindwa kwake
kudhibiti mauaji na mateso kwa wananchi.
Gekul
alisema kinachotokea sasa ni utekelezaji wa kauli ya Pinda aliyoitoa
bungeni akisema wahalifu wapigwe tu pamoja na ile ya Kagasheki aliyoitoa
mjini Arusha akisema majangili watakaokamatwa wamalizwe hukohuko kwenye
hifadhi.
Mbunge
huyo alieleza operesheni hiyo kwamba imesababisha mauaji ya watu wasio
na hatia ikiwemo mama Emiliana ambaye alifuatwa akiuza nyanya, lakini
akateswa hadi kufa na hadi sasa mwili wake bado uko katika Hospitali ya
Babati baada ya wananchi kugoma kuuzika.
Shibuda
kwa upande wake alisema Pinda anapaswa kufungua milango kwa mawaziri
wanaotakiwa kujiuzulu haraka, kutokana na kulea uzembe ambao
umesababisha madhara makubwa kwa wafugaji.
Shibuda
alisema kuwa Wizara ya Mifugo imekuwa na mtazamo hasi lakini
akasisitiza kuwa uzembe wa viongozi wa ngazi za mikoa, wilaya hadi
vijiji unatokana na ukimya wa Pinda ambaye anashindwa kuchukua hatua
yoyote dhidi yao.
Wabunge wengine
Kwa
upande wake Nkumba aliunga mkono kuundwa kwa kamati teule, lakini
akasisitiza kuwa mawaziri hao wanne wana hoja za kujibu ndani ya chama
tawala CCM na kwa Rais, vinginevyo Serikali haipaswi kuendeshwa na
viongozi wazembe
No comments:
Post a Comment