Saturday, November 2, 2013
BAADA YA NICK WA PILI KUMALIZA MASTER DEGREE MLIMANI HUU NDIO USHAURI ALIO TOKA KWA WANAMUZI
Rapper wa kampuni ya Weusi, Nick wa Pili amefanikiwa kuhitimu shahada yake ya pili kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.
Nick aliitoa taarifa hiyo kwenye kipindi cha Club 10 cha Clouds FM na kutoa ushauri kwa wanafunzi wanaofanya muziki.
“Mimi ni mwanafunzi, jana nimemaliza degree ya pili mlimani. Nimefurahi kuna wanafunzi wanataka kuwa kama mimi,kuna vitu vichache vya msingi vya kuzingatia kwa upande wa sanaa. Inabidi waache mambo mengi ya sanaa wachague kitu kimoja, atake kuwa msanii bora. Ukitaka kuwa msanii bora usihangaikie mambo ya kwenda studio, sijui kumtafuta nani ,sijui kutafuta interview, atake kuwa msanii bora hayo mambo mengine yatakufuata,” alisema Nick.
“Ukitaka kufanikiwa kitaaluma, njia moja ni kusoma lakini kusoma vipi,sio kusoma unasubiri kufika form 4 ndio unaanza kusoma au umefika form 6 ndio unaanza kusoma. Mwanafunzi bora ni yule anayesoma kila siku na unatakiwa kusoma kila siku. Soma kidogo, elimu sio ngumu, tatizo wanafunzi wanafeli katika mipango. Soma kidogo tambua masomo yako, tambua topic zako.Kila somo tambua topic ngapi, angalia muda wangu mwaka huu ilitakiwa nisome moja mbili tatu,nne ,tano jee nimefika? au unajipima. Pili ni kusoma kidogo hata ikawa ni kwa masaa mawili kila siku yanatosha kabisa.”
Hivi karibuni Nick wa Pili alipata shavu la kuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu kwenye semina za fursa kwenye mikoa zaidi ya 13
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment