Pages


Photobucket

Saturday, December 14, 2013

HUYU NDIYE MWENYEKITI MPYA WA TAHLISO 2013/2014


   Bw, Musa  Mdede -Rais waChuo kikuu cha Bugando   (Katikati) Akizungumza Mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti  wa TAHLISO 2013/2014

Bw.Musa Mdede ameibuka Kidedea katika hatua ya pili baada ya kupata kura 18, akifuatiwa  na Rais wa  St. John  Dodoma Bw, Katumbi Edmund  kupata kura 7 akifuatiwa  na Bw.Hemed Ally Rais wa IFM aliyepata kura 6.
Ingwa katika hatua ya kwanza wagombea wa nafasi hiyo walikuwa  ni Watano,Ambapo matokeo yao ya awali   Musa Mdede  (Kura 16),Hemed Ally (kura 7) ,Katumbi Edmund (Kura  5) ,Bi. Tusubilege  Benjamin (Makamu wa Rais wa UDSM -Kura 3) na paschal  Mlela(  kutoka chuo cha Theophilo Kisanje  Mbeya -  kura  3) .Hali hiyo ilifanya  jumla ya kura kuwa 34   na kati ya wagombea wote katika hatua ya kwanza hakuna aliyefikisha  zaidi ya asilimi Hamsini (50%)  hivyo kuufanya uchaguzi kurudiwa katika nafasi hiyo kwa washindi watatu wakwanza katika hatua ya pili.

 Muonekano wa Viongozi wapya wa TAHLISO 2013/2014,kutoka kulia ni Mhazini  Bw.Mollel Hilary (Kutoka Chuo cha Kodi Dae es salaam),Bi.Halima Bakari -Katibu Mkuu(Kutoka chuo cha AMUCTA-Tabora),Makamu Mwenyekiti  Bw.Abdul Mohamed (Rais wa Chuo cha kikuu Zanzibar),Mwenyekiti  Bw.Musa  Mdede (Rais Chuo kikuu Bugando) na Naibu Mhazini  Bw.Khamis  Hamza (kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar)


 
 Mwenyekiti  Anayemaliza Muda wake Bw. Amon  Chakushemeire   akizungumza  maneno machache baada ya  Mwenyekiti mpya kutangazwa.

No comments:

Post a Comment