Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic
Solar Contractors Patrick Ngowi akisikiliza mawazo ya mmoja wa vijana
wajasiriamali mwenye nia ya kukataka kukuza biashara yake na kuifanya
kuwa endelevu wakati wa uzinduzi wa Mara Foundation ambao uliotoa fursa
ya washiriki kuzungumza na wafanyabiashara waliopiga hatua na wenye
uzoefu katika kuendesha biashara zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim
Limited Emelda Mwamanga akimsikiliza mmoja wa washiriki ambaye ni
mjasiriamali anayechipukia aliyetaka kupata uzoefu na mawazo zaidi jinsi
ya kuendesha biashara yake.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees
ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali
akimsikiliza mjasiriamali mdogo mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa
kimataifa.
Ma-Mentors waliokuja kuzungumza na
wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya kuwapa mbinu mbalimbali za
kibiashara na kuwaongoza kufikia malengo yao.
Taasisi ya Mara Foundation
ilianzishwa na Ashish Thakkar ambaye ndie mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu
wa Mara Group. Ashish alitumia muda wake mwingi katika kutimiza malengo
ya Taasisi hiyo kwa kuwa alikuwa na imani na wajasiriamali na
kuendeleza biashara ndogo.
Tangu mwaka 2009 Taasisi hiyo
ililenga mtazamo wake na imefanya vizuri sana nchini Uganda, Tanzania,
Kenya na Nigeria katika muelekeo huo. Kuanzia mwaka 2013 mikakati ya
taasisi ya Mara Foundation inaendelea kukua katika nchi za Kusini mwa
Jangwa la sahara huku ikiendelea kuongeza wigo wake katika nchi
nyingine duniani. Mara Foundation inafanya kazi ya kubuni na kukuza
uchumi endelevu na kufungua fursa endelevu kwa vijana wamiliki wa
biashara za kati kwa kupitia vituo vya uwezeshaji vya Mara Launchpad na
Mara Launch Fund.
Pichani juu na chini ni Washiriki
na wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kabla ya mgeni rasmi Dkt. Mary
Nagu kuzindua Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Mara
Foundation Tanzania Nina Werner (kulia) akizungumza machache kuhusiana
na malengo ya Taasisi yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mh. Dkt.
Mary Nagu kuizindua rasmi.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa
taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akizungumza wakati
kuzindua taasisi ya Mara Foundation ambapo amewataka vijana
wajasiriamali kutumia fursa ya taasisi hiyo kujijenga kibiashara Taasisi
ya Mara Foundation yenye makao yake makuu jijini Dubai sasa imejikita
katika nchi za Afrika ambazo ni Uganda, Tanzania, Kenya na Nigenia kwa
lengo kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuwezeshwa kimuongozo na kuwa
wafanyabiashara wakubwa ambao wataweza kutoa ajira kwa watu wengine.
Washiriki na wageni waalikwa
wakifurahi jambo wakati mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu akitoa risala kwenye
uzinduzi wa Taasisi ya Mara uliofanyika hivi karibuni kwenye jengo la
Mayfair Plaza.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa
taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akikata utepe kuzindua
rasmi taasisi hiyo yenye matawi 28 barani Afrika. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkazi wa Mara Foundation Nina Werner.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Wageni waalikwa wakishangilia kwa makofi.
MC wa uzinduzi huo ambaye pia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Problem Solved Eric Mutta akimkabidhisha
Mjasiriamali mdogo Peter Christopher kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic
Solar Contractors Patrick Ngowi (katikati) atakayekuwa mshauri wake
wa kibiashara kwa muda wa miezi sita ijayo.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees
ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali
(katikati) akimpokea mmoja wa wajasiriamali waliohudhuria uzinduzi wa
Mara Foundation kwa lengo la kuhakikisha anatimiza malengo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim
Limited Emelda Mwamanga (kushoto) akipata picha ya ukumbusho na kijana
aliyemchagua kumsaidia kimawazo na kumwongoza kwa muda wa miezi sita
ijayo mpaka kufikia lengo lake.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation uliofanyika hivi karibuni Mayfair Plaza.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic
Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) na Mkurugenzi Mshirika wa
IMMMA Advocates Lawrence Masha wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Mara Foundation.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic
Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA
Advocates Lawrence Masha (kulia) na Mkurugenzi wa man Magazine Dismas
Massawe (katikati) katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Mara
Foundation.
No comments:
Post a Comment