Pages


Photobucket

Tuesday, March 5, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA KIVUKO CHA MV MUSOMA LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Kivuko cha MV Musoma, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara. Kutoka (kulia) kwake ni mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Bw. John
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi uzinduzi wa Kivuko cha Mv Musoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013, kijiji cha Kinesi Wilayani Rorya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akibonyesha kitufye kupiga alam, kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko cha Mv. Musoma, wakati wa uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013 katika kijiji cha Kinesi. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akipiga makofi kufurahia uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakiwa ndani ya Kivuko cha Mv. Musoma baada ya kuzinduzliwa rasmi na Makamu wa Rais, leo Feb 5, 2013 wilayani Rorya kijiji cha Kinesi mkoa wa Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa MKoa wa Mara, John Tupa, pamoja na viongozi wa Chama na Serikali, wakiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu baada ya uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na viongozi wa Chama na Serikali, wakati akitoka kukagua Kivuko cha Mv. Musoma, baada ya kukizindua rasmi leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi wilayani Rorya. Picha na OMR.

No comments:

Post a Comment