Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Nassari alikanusha
taarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari jana kuwajuzi
alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa
Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha, uchaguzi uliofanyika juzi ambapo
mgombea wa Chadema aliibuka mshindi.
Nassari ameyasema hayo jana
jioni wakati akihutubia katika Mkutano wa hadhara kuzindua kampeni
nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa
ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika
Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa
na watu wengi, ulifanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River ambapo
mbali na Nassari, Katibu wa CHADEMA Kinondoni Ng Henry Kileo nae
alikuwepo na alipewa nafasi ya kuzungumza.
Nassari alidai kuwa
katika uchaguzi wa juzi yeye alikuwa Wakala Mkuu wa CHADEMA Kata ya
Bangata na hivyo kumhusiha na ya Daraja Mbili haelewi inakujaje. Amedai
kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na
kwamba Polisi walimuweka ndani na kuandika maelezo yake, lakini
anashangaa kuambiwa ni yeye wakati siyo!
Akifafanua zaidi
aliviomba vyombo vya usalama avinavyohusika na masuala ya vibali vya
kumiliki silaha za moto, kufanya uchunguzi wao na waeleze hiyo bunduki
walimpa lini na ni risasi zimetumika, na kwamba kama ni kumkamata yeye
yupo huru muda wowote wanaweza kumkamata.
Katibu
wa CHADEMA Kinondoni, Dar es Salaam, Henry Kileo akizungumza na
wananchi wa Usa River leo jioni.Nassari alisema kampeni hizo
zitahitimishwa Novemba 3, 2012 katika viwanja hivyo na kuna uwezekanao
Mh Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chama hicho taifa akahudhuria.Awanadi wagombea wa Chadema
Mh
Nassari aliweza kuwatambulisha rasmi wagombea wa Chama chake
(waliosimama) watakaoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 9
katika Halmashaur ya Mji Mdogo wa Usa River, uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika Jumapili ya Novemba 4, 2012. Katika wagombea hao, mwanamke
aliyejitokeza ni mmoja tu, Verian Mushi ambae anagombea mtaa wa
Magadini.
1. Verian Mushi – Magadini,
2. Henry Benjamin Mpinga – Manayata
3. Ernest Makalla Shilla – Magadirisho
4. Exaud Jackson Mbise – Nganana
5. Richard Mohamed Ngungu – Kisambare
6. Malisa – Mji Mwema
7. Santrumini Filipo – Mlima Sioni (Lake tatu)
8. Frank Anael Msuya – Usa Madukani
9. William – Ngarasero
Nassari azungumzia mafanikio ndani ya miezi 5 ya ubunge wake
Katika
hotuba yake, Mh Nassari aliweza pia kuzungumzia baadhi ya mambo ambayo
amekwishayafanya kwa wananchi wake wa Arumeru tangu wamchague kuwa
mbunge wao, takribani miezi mitano iliyopita.
Akiorodhesha mambo hayao harakaharaka, Nassari alisema kwamba amekwishakamilisha mradi wa majai ya kisima wenye thamani ya sh mil 60 kwa maeneo ya Ngobobo na Ngarenanyuki.
Akiorodhesha mambo hayao harakaharaka, Nassari alisema kwamba amekwishakamilisha mradi wa majai ya kisima wenye thamani ya sh mil 60 kwa maeneo ya Ngobobo na Ngarenanyuki.
Akaeleza kuwa ameanzisha ligi ya mpira wa miguu kwa
Kata zote za Jimbo lake ambapo amedai kuwa vifaa vimemgharimu zaidi ya
sh milioni 5. Ligi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 10 Novemba,
2012.
Alidai kuwa ameshiriki kwenye harambee nyingi za maji na
kwamba ya karibuni amechagia kiasi cha sh milion 1.5, pia amechangia sh
milioni 1 kwaya ya Jimboni kwake iliyomwaomba kuwasaidia.
Mambo
mengine ni pamoja kusambaza vitabu vyenye thamani ya sh milion 38 kwa
shule 15 za Kata, sehemu kubwa ikiwa ni msaada wa rafiki zake wa
Marekani. Pia nmatengenezo ya choo kwa shule ya msingi Liganga,
kuchangia vikundi vya kina mama.
CHANZO; NOISE OF SILENCE BLOG
No comments:
Post a Comment