Pages


Photobucket

Wednesday, October 31, 2012

TMEA YATOA MSAADA WA KOMPYUTA KWA TANGO

 Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Tanzania (TANGO), Ngunga Tepani akiangalia kompyuta, skana, printa pamoja na king’amuzi cha inteneti vilivyotolewa na TradeMark East Afrika (TMEA). Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa TMEA, Paulina Elago. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Tanzania (TANGO), Ngunga Tepani akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni  Mkurugenzi Mkazi wa TMEA, Paulina Elago.(Picha na Habari Mseto Blog)

MKUU WA MKOA ARUSHA AAMURU WANAFUNZI WASWEKWE MAHABUSU

 
Picture
Mwanafunzi wa Sekondari ya Kimnyaki, Arumeru, Ezekiel Memiri, alivyoshikiliwa na Askari Polisi Peter Mvula, Mkuu wa Operesheni wa Mkoa baada baada kuamuru akamatwe kwa kosa la kushinikiza maandamano ya Wanafunzi wenzake hadi Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa.
Picture
Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo akiongea na wanafunzi na kutoa onyo kali kwa wanafunzi ambao hawatarudi shuleni watafukuzwa mara moja
Habari imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Pamela Mollel

MKUU wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewasweka lumande wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Kimnyaki kwa kosa la kushinikiza maandamano ya wanafunzi wenzake hadi Ofisini kwake.

Wanafunzo hao waliokamatwa kwa kosa la kuchochochea maandamano hayo ni pamoja na Ezekiel Memiri, Losijaki Lunde, na Meshack Lomunyaki.

Maandamano ya wanafunzi hao yalikuwa na lengo la kumshinikiza Mkuu huyo wa Mkoa kumuondoa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo.

Akizungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo jana Ofisini kwake alisema kwamba wanafunzi hao wameshindwa kufuata maagizo yaliyoandikwa katika fomu zao za kujiunga na masomo shuleni hapo.

 Mkuu wa Mkoa alisema kwamba ni makosa makubwa kwa wanafunzi kukaidi ama kushindwa kufuata maagizo ya shule hasa yaliyoandikwa katika fomu zao za kujiunga na shule.

“Askari kamata hawa jamaa weka ndani hawana heshima hata kidogo,haiwezekani wakalifanya jiji la Arusha kama kiwanja cha michezo kwamba kila anayehitaji kucheza anaruhusiwa kufika, haya mambo hayawezekani hata kidogo, lazima utaratibu ufuatwe na kila mmoja apewe haki ya kusikilizwa”alisema Mkuu wa Mkoa na kuongeza:

“Tena nataka kuchukuwa nafasi hii kupiga marufuku maandamano yote ya wanafunzi katika Jijini la Arusha, siwezi kukubaliana na suala hili hata kidogo, kuna viongozi wa serikali wapo shuleni,nyinyi mko huku,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru yuko huko tayari kwa ajili ya kuwasiliza mmekimbilia kwa Mkuu wa Mkoa tena bila vibali vya maandamano”

 Awali kabla ya wanafunzi hao kufika Ofisini kwake walikutana na vikwazo vya Askari wa Jeshi la Polisi na kuwapiga mabomu ya machozi wanafunzi hao.

Maandamano hayo  yaliyoanza juzi kwa lengo la kumshinikiza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo aondolewe kwa kile walichodai kwamba anachangia kudidimiza maendeleo yao kitaaluma na kwamba anafurahia matokeo mabaya ya wanafunzi hao baada ya mitihani yao.

Baada ya Jeshi la Polisi kufanikiwa kuzuia maandamano hayo siku ya kwanza, jana wanafunzi hao walibuni njia nyingine ya kuandamana na kufanikiwa kufika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

“Juzi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru alifikia shuleni kwetu akatuambia kwamba angekuja kesho (yaani leo) tukamsubiri hadi saa nne bila mafanikio ndipo tulipobuni njia nyingine ya kuandamana, tukaamua kuondoka shule mmoja mmoja mpaka katikati ya mji, na tulipokutana na askari hao tukaanza tena kupambana na kila walipoturushia mabomu ya machozi sisi tuaanza kuwarushia mawe huku tukinawa usoni”alisema Ezekiel Memiri.
Picture
Wanafunzi wakiwa wamenyanyua juu mabango yenye ujumbe wa kutomtaka mkuu wa shule
Picture

HAYA NDIO YALIYO MKUTA HAMAD RASHIDI (MB) NDANI YA MASAA 4

Picture
Francis Godwin (kofia nyekundu) akihojiana na Mhe. Hamad huko Iringa jana.



Uhaba  wa mafuta  ya petroli na dizeli ambao  umeendelea  kuukumba mji  wa Iringa kwa  zaidi ya  siku tano  sasa, umeendelea  kuwatesa  wananchi  wa kada mbalimbali ambapo jana, Mbunge  wa  jimbo la Wawi katika  Serikali ya Mapinduzi  ya  Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed (CUF) ameonja keor hiyo baada ya kuingia mjini Iringa  na  kujikuta akisota kwa  zaidi ya saa nne katika foleni ya kusubiri kununua mafuta katika  kituo cha kimoja wapo  kilichokuwa  kikiuza mafuta katika eneo la Ipogolo.
Mbunge  Hamad  alikuwa  safarini  kutokea  mkoani Morogoro  akielekea Mafinga  wilaya ya  Mufindi. Mbunge huyo amesema,  "serikali inapaswa  kuangalia  uwezekano  wa  kutatua tatizo hilo la uhaba wa mafuta hapa nchini vinginevyo uchumi  wa nchi utaendelea  kuyumba  zaidi"

Amesema  kuwa kitendo  cha  wananchi  kushinda katika foleni kwa  saa zaidi ya sita  wakisubiri kununua mafuta katika  kituo hicho ni sawa na wananchi hao kupoteza muda wa kuzalisha, hivyo Serikali iliyopo madarakani inapaswa  kushughulikia tatizo hilo ambalo linasababishwa na  waagizaji  wakubwa wa mafuta hapa nchini.

Mbunge huyo alisema  alifika katika  foleni  hiyo majira ya saa 8 mchana na  kufanikiwa  kununua mafuta  saa 12 jioni.

Mbali ya uhaba  huo  wa mafuta, uchunguzi  uliofanywa na Francis Godwin (kutoka
francisgodwinblog )   umebaini  kuwa baadhi ya  vijana  walikuwa  wakishirikiana na wafanyakazi  wa vituo  hivyo vya mafuta kwa  kununua mafuta na kujaza katika mapipa na kupakia katika magari na kwenda kuyauza kwa bei  kubwa  zaidi mjini Iringa.

Tuesday, October 30, 2012

KASHESHE LA HURRICANE SANDY NCHINI MAREKANI (HII SIO MAREKANI UNAYO IFAHAMU)


Photo: Kwa Mujibu wa taratibu zinavyokwenda Atlantic City tayari imeshavamiwa na kimbunga na  hapa mitaa yetu ambapo tupo kando kando kitaapita mida ya saa tisa mchana yani 3:PM na kinatarajiwa kuungana na vimbunga vingine viwili kutoka kaskazini na kusababisha hali mbaya ya hewa itakayotanda kwa upana wa kilomita 1,200 na kuathiri wakazi milioni 60.
  Eneo la  Atlantic City tayari likiwa limevamiwa  jana  mida ya saa tisa mchana  ambapo kilitarajiwa kuungana   na vimbunga vingine viwili kutoka kaskazini na kusababisha hali mbaya ya hewa kwa kutanda  upana wa kilomita 1,200 na kuathiri wakazi milioni 60.
On its way: A car plows through a flooded street in Norfolk, Virginia after the impact of Hurricane Sandy
Mitaa ya Norfolk, Virginia  kukiwa kumezongwa na wimbi la Hurricane Sandy
Rising: Pieces of the boardwalk float in sections through the flooded streets of Atlantic City - which is expected to get the brunt of the storm tonight
Atlantic City  kukiwa  kumeshavamiwa na kimbunga (siku ya jana)

Group work: Pedestrians come to the aid of a motorist stuck on a flooded-out road along the shoreline area of Milford, Connecticut
Wakazi wa mji wa Milford, Connecticut wakionekana kusukuma gari lililonasa katika Maji yaliosababishwa na Kimbunga kilichoendelea baadhi  maeneo ya mashariki mwa Marekani  siku ya jana
Felled: A broken tree is seen during winds as the Path Station starts to get flooded in Hoboken, New Jersey

Mti uliopata dharuba ya kimbunga katika mitaa ya Hoboken,jijini New Jersey

Hali ilitia  kutia simazi dhidi ya dhoruba ya kimbunga kikali Maeneo  ya  Mashariki mwa Marekani hii hapa picha ya nyumba ilioelemewa na Mti mkubwa katika maeneo Delaware County, Jijini Pennsylvani ( siku ya jana)

Taken off: A trampoline becomes caught in the power lines on Norman Drive in Long Island as Hurricane Sandy gathers speed
Kama manavyoona pichani Trampoline limechukuliwa juu kwa juu kwa dhoruba kali na kunasa kwenye nyaya za umeme  huko, Long Island wakati Kimbunga Sandy kikizidi kuendele kingia Jimbo hadi Jimbo(siku ya jana)
Rais Obama  ikiteremkakutoka  katika ndege  (Air Frce One)  siku ya jana mara baada ya kuwasili   Andrews .

 
TASWIRA YA KIMBUNGA HICHO KATIKA PICHA

LIVE HURRICANE SANDY COVERAGE - THE WEATHER CHANNEL

JOSHUA NASSARI AKANUSHA KUFYATUA RISASI KWENYE UCHAGUZI WA MADIWANI DARAJA II ARUSHA JUZI

Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Nassari alikanusha taarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari jana kuwajuzi alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha, uchaguzi uliofanyika juzi ambapo mgombea wa Chadema aliibuka mshindi.
Nassari ameyasema hayo jana  jioni wakati akihutubia katika Mkutano wa hadhara kuzindua kampeni nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na watu wengi, ulifanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River ambapo mbali na Nassari, Katibu wa CHADEMA Kinondoni Ng Henry Kileo nae alikuwepo na alipewa nafasi ya kuzungumza.
Nassari alidai kuwa katika uchaguzi wa juzi yeye alikuwa Wakala Mkuu wa CHADEMA Kata ya Bangata na hivyo kumhusiha na ya Daraja Mbili haelewi inakujaje. Amedai kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na kwamba Polisi walimuweka ndani na kuandika maelezo yake, lakini anashangaa kuambiwa ni yeye wakati siyo!
Akifafanua zaidi aliviomba vyombo vya usalama avinavyohusika na masuala ya vibali vya kumiliki silaha za moto, kufanya uchunguzi wao na waeleze hiyo bunduki walimpa lini na ni risasi zimetumika, na kwamba kama ni kumkamata yeye yupo huru muda wowote wanaweza kumkamata.
DSCN5926Mh Nassari akihutubia mkutanoni hapo jana
DSCN5946Sehemu ya umati ulijitokeza katika ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Ngaresero, Usa-River
DSCN5906Katibu wa CHADEMA Kinondoni, Dar es Salaam, Henry Kileo akizungumza na wananchi wa Usa River leo jioni.Nassari alisema kampeni hizo zitahitimishwa Novemba 3, 2012 katika viwanja hivyo na kuna uwezekanao Mh Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chama hicho taifa akahudhuria.

Awanadi wagombea wa Chadema
DSCN5952Mh Nassari aliweza kuwatambulisha rasmi wagombea wa Chama chake (waliosimama) watakaoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 9 katika Halmashaur ya Mji Mdogo wa Usa River, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili ya Novemba 4, 2012. Katika wagombea hao, mwanamke aliyejitokeza ni mmoja tu, Verian Mushi ambae anagombea mtaa wa Magadini.

Wagombea wa Chadema na Mitaa wanayogombania ni hawa wafuatao
1. Verian Mushi – Magadini,

2. Henry Benjamin Mpinga – Manayata
3. Ernest Makalla Shilla – Magadirisho
4. Exaud Jackson Mbise – Nganana
5. Richard Mohamed Ngungu – Kisambare
6. Malisa – Mji Mwema
7. Santrumini Filipo – Mlima Sioni (Lake tatu)
8. Frank Anael Msuya – Usa Madukani
9. William – Ngarasero
DSCN5908Baadhi ya viongozi wa Chadema Usa River na wagombea wao

Nassari azungumzia mafanikio ndani ya miezi 5 ya ubunge wake
Katika hotuba yake, Mh Nassari aliweza pia kuzungumzia baadhi ya mambo ambayo amekwishayafanya kwa wananchi wake wa Arumeru tangu wamchague kuwa mbunge wao, takribani miezi mitano iliyopita.

Akiorodhesha mambo hayao harakaharaka, Nassari alisema kwamba amekwishakamilisha mradi wa majai ya kisima wenye thamani ya sh mil 60 kwa maeneo ya Ngobobo na Ngarenanyuki.
Akaeleza kuwa ameanzisha ligi ya mpira wa miguu kwa Kata zote za Jimbo lake ambapo amedai kuwa vifaa vimemgharimu zaidi ya sh milioni 5. Ligi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 10 Novemba, 2012.
Alidai kuwa ameshiriki kwenye harambee nyingi za maji na kwamba ya karibuni amechagia kiasi cha sh milion 1.5, pia amechangia sh milioni 1 kwaya ya Jimboni kwake iliyomwaomba kuwasaidia.
Mambo mengine ni pamoja kusambaza vitabu vyenye thamani ya sh milion 38 kwa shule 15 za Kata, sehemu kubwa ikiwa ni msaada wa rafiki zake wa Marekani. Pia nmatengenezo ya choo kwa shule ya msingi Liganga, kuchangia vikundi vya kina mama.


CHANZO;  NOISE OF SILENCE BLOG

DK.MWAKYEMBE ATIKISA: NI KUHUSU USAFIRI WA TRENI JIJINI DAR ES SALAAM

 Baadhi ya abiria wakiingia kwenye treni
 muonekano ndani ya treni
 Baadhi ya abiria wakishuka na kupanda kwenye treni
 Kwa usafiri wenye utulivu kama huu kwanini usijisomee kwenye treni.
 Tiketi zikikatwa ndani ya treni
 Treni ikiwasili Kituo cha Ubungo Maziwa
 Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akiwasili kupanda treni kituo cha tazara kuelekea mjini kufanya uzinduzi
 Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndani ya treni
Chombo kikichanja mbuga kuelekea mjini

Na Joachim Mushi, Thehabari.com
USAFIRI wa kutumia treni jijini Dar es Salaam kutokea eneo la Ubungo Maziwa kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni ya Treni) umeanza jana. Treni ya kwanza iliondoka Ubungo majira ya saa 12:00 asubuhi kuelekea katikati ya jiji, ambapo kwa mujibu wa maofisa wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ilitumia wastani wa dakika 30 kufika katikati ya jiji.

Treni ilioanza kazi jana iliyokuwa na injini mbili (vichwa vya traini) moja ikiwa imefungwa nyuma na nyingine mbele huku ikiwa na mabehewa sita, yaani matano ya abiria wa kawaida (watu wazima) na moja likiwa ni maalumu kwa ajili ya kubeba wanafunzi. Abiria mmoja ni sh. 400 kwa tripu huku wanafunzi wakitakiwa kulipa sh. 100 kwa kila mmoja.


Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndiye aliyezindua usafiri wa jana ambao ni wamajaribio, akiwa pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha Reli. Treni hiyo pia ilizinduliwa pamoja na treni ya TAZARA ambayo itafanya kazi kama ya Ubungo, lakini yenyewe ikianzia eneo la TAZARA kuelekea Mwakanga.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi huo Waziri Mwakyembe alisema atahakikisha treni hiyo inaendelea kufanya kazi ili kuwasaidia kiusafiri wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisumbuliwa na kero ya usafiri hasa kwa foleni, ambapo utumia muda mrefu njiani kuingia na kutoka jijini.

Alisema jumla ya mabehewa ya treni 14 pamoja na injini mbili zimekarabatiwa na mafundi wazalendo nchini, ambayo ndiyo yatakayokuwa yakifanya kazi ya kusafirisha abiria kuingia na kutoka jijini kila asubuhi na jioni. Alisema kwa sasa inafanya treni moja kwa majaribio lakini baada ya uzinduzi mkubwa zitafanya kazi treni mbili, na zitakuwa zikipishana njiani moja ikirudi na nyingine ikienda.

Akifafanua zaidi alisema kitendo cha mafundi wazalendo kufanya ukarabati kwa mabehewa na injini kimeokoa kiasi kikubwa cha fedha za umma kwani ukarabati wote umetumia sh. bilioni 2.1 tu, ilhali kama Serikali ingelazimika kukodi injini gharama ingekuwa kubwa zaidi kwani bei ya kukodi injini moja ya treni ni sh. milioni moja kwa siku.

Hata hivyoDk. Mwakyembe aliwataka Watanzania hasa abiria kuwa wavumilivu kwa upungufu utakaojitokeza kwa safari za mwanzo kwani bado wanaendelea kufanya marekebisho kadhaa, lakini baada ya muda mambo yatakaa sawa. Mwandishi wa habari hizi alikuwa ni mmoja wa wasafiri walioizindua treni hiyo jana.

Awali akizungumza mmoja wa viongozi waandamizi wa TRC, alisema treni hiyo itafanya kazi kila siku isipokuwa kwa siku za jumapili na siku kuu na itaanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa sita mchana na kupumzika hadi saa 9:00 za jioni, itakapoendelea tena na safari zake hadi majira ya saa nne usiku.

Uchunguzi uliofanywa na muandishi wa habari hizi umebaini kuwa behewa moja la treni linauwezo wa kuchukua abiria 66 wakiwa wamekaa, lina milango minne, feni, taa, muziki/redio, pamoja na mikanda maalumu ya kujishikia kwa abiria ambao watakuwa wamesimama.

Aidha mabehewa yote yana madirisha ya kutosha kuingiza na kutoa hewa ya kutosha. Treni ilioanza kazi jana, ikitokea Ubungo ilikuwa ikisimama vituo vya eneo la Mwananchi (relini), Tabata Relini, Buguruni Miamani, Tazara, Kariakoo Gerezani (Kamata), na mwisho Kituo Kikuu cha Treni kilichopo jirani na Kituo cha Polisi Kati (Katikati ya Jiji)