
 Kaimu
 Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo 
(katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  mradi wa msaada wa 
kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani 
Lushoto mkoani Tanga jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la 
 Equality for Growth (EfG), Jane Magigita na Katibu Tawala wa wilaya 
hiyo (DAS), Josephine Kisigila. Mradi huo unaendeshwa na EfG.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akitoa hutuba fupi kwa mgeni rasmi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliopatiwa mafunzo hayo.
 Wanawake wa Wilaya ya Lushoto wakiwa kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa mradi huo na ofisi.
Viongozi mbalimbali waliojumuika kwenye uzinduzi huo.
 Mkurugenzi
 Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (mbele
 katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wasaidizi hao wa kisheria na
 maofisa wa EfG.
 Wanahabri
 kutoka vyombo mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi huo. Kutoka 
kushoto ni Shadrack (Channel 10), Nasra Abdallah (Tanzania Daima), Dotto
 Mwaibale (Jambo Leo na Mtandao wa www.habari za jamii.com na Sophia 
kutoka Televisheni ya Mlimani.
 Wanafunzi nao walijumuika kuona shughuli mbalimbali za uzinduzi huo hasa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani.
 Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.
 Zawadi zikitolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita.
 Mkurugenzi
 Mtendaji wa EfG, Mary Magigita akiwa ameshika mkungu wa ndizi 
aliozawadiwa. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Josephine 
Kisigila.
 Kaimu
 Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo 
(kushoto), akifurahi na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for
 Growth (EfG), Jane Magigita baada ya kukabidhiwa machapisho mbalimbali 
ya EfG.
Maofisa wa EfG, Eva (kushoto) na Samora wakiwa katika maandalizi ya uzinduzi huo "Chezea EfG wewe"
Doto Mwaibale
WAJASIRIAMALI
 wanawake wametakiwa kutumia mafunzo ya usimamizi wa sheria katika 
masoko waliyopata kwa kuwaelimisha wengine badala ya kukaa nyumbani bila
 ya kutoa elimu hiyo.
Mwito 
huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto 
Dk.Hassan Shelukindo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mradi wa msaada wa 
kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani humo 
 mkoani Tanga jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Jumanne 
Shauri. 
"Ninyi
 Wanawake wa Lushoto mmepata bahati kubwa ya kuletewa mradi huu pamoja 
na mafunzo haya mliyopata nawaombeni nendeni mkayafanyie kazi katika 
maeneo yenu" alisema Dk. Shelukindo
Alisema
 elimu waliyoipata ya msaada wa kisheria ni muhimu sana kusaidia jamii 
katika masoko na itasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijisinsia.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), ambalo linaendesha 
mradi huo, Jane Magigita alisema lengo la mradi huo katika wilaya hiyo 
ni kuhamasisha na kulinda haki za wafanyabiashara iwanawake katika 
masoko kwa kuwapatia elimu ya sheria, biashara, elimu ya vicoba, elimu 
ya uongozi na usimamizi wa vikundi.
Alisema
 EfG ni shirika la pekee nchini linalotoa msaada wa kisheria kwa sekta 
isiyorasmi hivyo kuonesha ni kiasi gani sekta hiyo ilivyo sahulika.
Alisema
 EfG  inaendesha mradi huo katika masoko ya wilaya ya Lushoto pamoja na 
vikundi mbalimbali vya maendeleo na kuwa shirika hilo linawajibika kutoa
 mafunzo  ya siku 25 kwa wasaidizi 25 ambao watasambaza huduma sheria 
kwa jamii.
Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu tano ambapo kila awamu yatakuwa yanafanyika kwa  takribani siku tano.
" 
Shirika linawajibika kutoa mafunzo mafunzo mbalimbali kwa 
wafanyabiashara ikiwa na lengo la kuinua hali za wanawake 
wafanyabiashara sokoni kupitia mafunzo ya biashara, uundwaji wa vikundi 
vya Vicoba, mafunzo mbalimbali kwa watendaji na viongozi wa Halmshauri 
ya wilaya ya Lushoto kwa lengo la kuboresha hali za wafanyabiashara 
sokoni" alisema Magigita.
Alisema
 mpaka sasa shirika hilo limefanikiwa kuwapatia mafunzo ya sheria ya 
siku tano wasaidizi wa sheria 25, wanaume 8 na wanawake 17 kutoka katika
 masoko na wengine kutoka katika vikundi vya maendeleo ndani ya 
Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto.
Alisema
 pia wanakituo maalumu cha msaada wa sheria katika ofisi za EfG Lushoto 
ambapo wafanyabiashara mbalimbali wanaruhusiwa kupeleka matatizo yao ya 
kisheria kila siku za Jumatatu na Jumatano kuanzia saa tatu asubuhi 
mpaka saa 10 jioni.