Pages


Photobucket

Tuesday, December 3, 2013

Kocha Kibaden afungukakuhusu kuachia ngazi na matatizo aliyokutana nayo ?


Kibaden1Baada ya kukabidhiwa barua ya kusimamishwa kazi kuitumikia klabu ya Simba, kocha Abdallah Kibaden amesema anakubali kuachia ngazi ila anaomba kulipwa pesa zake.
Anasema ‘kuna migogoro sana hata mimi nimechoka hii kazi, kubwa ilikua tuhakikishe kwamba timu inafanya vizuri ili mradi badae tuje kutafuta ubingwa, nilikua na imani kwamba hata mwaka huu tungeweza kupata ubingwa kwa jinsi timu ilivyokua inakwenda’
‘Tumecheza michezo 13 ya mzunguko wa kwanza, tumeshinda 6, sare 6 na kupoteza mchezo mmoja, nafasi tuliyoipata ni nafasi ya nne katika michezo 13, katika hizo mechi 13 mi nasema kwa nafasi ya nne sio mahali pabaya kwa sababu wao walicheza mechi 26 ligi ya mwaka jana na timu ikamaliza kwa nafasi ya nne’ – Kibaden
Kwenye sentensi nyingine Kibaden anasema ‘katika barua ya kusitisha mkataba ni kwamba timu haifanyi vizuri, wanasema uwezo wangu kufundisha ni mdogo.. mi sitaki kubishana nao kwenye hilo ila watu wenye kujua ndio wanaweza kusema kama hilo ni tatizo, narudia kusema nakubali kuachia ngazi ila nitashukuru wakinipatia haki yangu ambayo nastahili kupata’
‘Hiyo ni sehemu moja, sehemu ya pili ni matatizo niliyokumbana nayo sana baada ya kukubali kuifundisha Simba, ni kwamba kuna watu wako nje ya timu wanataka nafasi ya kuingia ndani ya timu, hilo ni tatizo’

No comments:

Post a Comment