Bw. Peragius  Cosmas mwanafunzi aliyehitimu shahada ya Uhasibu na kupata  GPA 4.91 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.
Bi. May Issa  mwanafunzi aliyehitimu shahada ya kwanza ya Usimamizi wa manunuzi  na 
kupata  GPA 4.92 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha 
CBE Prof.Emanuel Mjema.Kwa kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wanafunzi hawa kutoka kampasi ya Dodoma wameweza kupata ufaulu mkubwa katika masomo yao.
Bi. May Issa Mwanafunzi aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa Manunuzi katika mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE Dodoma mwaka 2014 ametangazwa kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa ufaulu kwa kupata GPA ya 4.92. ambapo aliweza kupata alama A 28 , alama B+ tatu na alama B moja kati ya masomo 32 ya shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na Bw. Peragius Cosmas aliyepata GPA ya 4.91.
Kwa upande wake Mwanafunzi mwingine Bw, Peragius Cosmas aliye kuwa akisoma Shahada ya kwanza ya Uhasibu yeye pia alionyesha maajabu kwa kuweza kupata GPA ya 4.91 ambapo aliweza kupata alama A 29 na alama B+ tatu kati ya masomo 32 ya shahada yake ya kwanza ya uhasibu.
Hivi karibuni katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) pia tulishuhudia Msichana Doreen Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa Mhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche alitangazwa kuwa kinara kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano,
 Bi. May  Issa akionekana mwenye furaha siku ya mahafali  ya 49 iliyofanyika hivi karibuni katika chuo cha Elimu ya biashara kampasi  ya Dodoma.
Bw. Peragius Cosmas akionekamna mwenye furaha  katika mahafali ya  49 ya  chuo cha CBE iliyofanyika hivi karibuni katika  Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dodoma.
  Bw. Peragius  Cosmas (kulia)  na May  Issa  (Kushoto) wakiwa na tabasamu  kufurahia kile walichoweza kukivuna katika kipindi chote cha miaka mitatu katika masomo yao CBE Dodoma .
  Rais mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi CBE  kampasi ya Dodoma 2013/2014 Bw. Remidius Emmanuel (kulia) akimpongeza  Bi. May  Issa kwa kufanya vizuri katika  masomo yake  kwa kipindi chote cha masomo yake.
 
 

