Na Yohane Gervas, Rombo
IMEELEZWA kuwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji
katika Wilaya ya Rombo imekua mbaya hasa katika tarafa za Mengwe na
Tarakea. Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
ya Rombo, Anthoni Tesha katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Rombo.
Tesha alisema kuwa maeneo mengi ya Tarafa za Mengwe na Tarakea
yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa huduma ya maji, hali inayowafanya baadhi
ya waalimu kuvunja vipindi vya mchana na kuwarudisha wanafunzi kwenda
kutafuta maji.
Aidha Tesha alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Rombo, Judathadei Mboya, kuhakikisha wanakutana na Meneja wa Kampuni
ya Maji ya Kiliwater ili kuzungumzia suala hilo mapema.
Uhaba wa maji katika vijiji mbalimbali katika wilaya ya Rombo
imeonekana kuwa changamoto kubwa hasa katika maeneo ya ukanda wa chini
wa wilaya hiyo ambapo baadhi ya maeneo hupata huduma ya maji kwa mgao na
maeneo mengine kukosa kabisa huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment