Pages


Photobucket

Saturday, September 28, 2013

AZAM TV KUANZA KUONYESHA MECHI ZOTE ZA YANGA

tv 

KITUO cha Televisheni cha Azam kimeahidi kuonyesha mechi za Yanga zitakazochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na zile za ugenini kwa sababu mkataba unawaruhusu.
 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah amethibitisha kuwa Azam TV wapo huru kuonyesha mechi yoyote ya Ligi Kuu Bara.
Habari nzuri ni kuwa ving’amuzi vya Azam TV vitaanza kuuzwa mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya mwezi ujao kabla ya mechi kuanza kuonyeshwa ama Oktoba 5 au Oktoba 9, mwaka huu.
Habari kutoka Azam TV zinasema kuwa wataonyesha pia mechi zinazoihusu Yanga kwa sababu mkataba unawataka kuonyesha mechi za Ligi Kuu Bara.
Yanga waligoma kusaini mkataba wa Azam TV kwa madai kuwa Sh 100 milioni ambazo kila klabu inapewa ni ndogo sana kwao.
“Mkataba wetu unasema kuwa tunatakiwa kuonyesha mechi za Ligi Kuu Bara, kwa hiyo tutaonyesha pia mechi za nyumbani na ugenini za Yanga, kwa sababu mkataba wetu tumesaini na Kamati ya Ligi,” alisema mmoja ya viongozi wa Azam TV.
Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu wa TFF, Osiah alisema Azam TV wapo huru kuonyesha mechi yoyote kwa sababu mkataba unawaruhusu.
“Hata kama ni mechi za Yanga iwe Dar es Salaam au mikoani, Azam TV wanaruhusiwa kuonyesha,” alisema Osiah.
Katika hatua nyingine, wataalamu kutoka Afrika Kusini wanatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Azam TV mpaka Oktoba 15, mwaka huu.
“Hawa wataalamu wameomba kabla hawajaondoka warushe mechi mbili laivu kuona kama kuna upungufu wowote. Na ndiyo maana nadhani mechi za raundi ya saba za Oktoba 5 au mechi za raundi ya nane za Oktoba 9, zitaanza kuonyeshwa moja kwa moja,” alisema mmoja wa mabosi wa Azam TV.
Alisema wataanza kuonyesha mechi za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mechi za mikoani zitaanza kuonekana baada ya kuwasili kwa gari la OB Van ambalo litashughulika na mechi za mikoani tu.
Kama Azam TV itaanza kuonyesha mechi Oktoba 5, ina maana kwamba wataanza na mechi ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting au siku inayofuata wanaweza kuonyesha pia Yanga dhidi ya Mtibwa. Iwapo mechi hizo hazitaonyeshwa maana yake mechi za raundi ya nane zinazoweza kuonyeshwa ni Azam dhidi ya Mgambo Oktoba 9, au Simba dhidi ya Prisons Oktoba 12 na Ashanti dhidi ya Coastal Union Oktoba 13.
Habari za ndani zinasema ving’amuzi vya Azam TV vitaanza kuuzwa wiki ya kwanza ya mwezi ujao.
CHANZO: GAZETI LA MWANASPOTI

DIAMOND AFANYA KUFURU NDANI YA VISIWA VYA MARASHI ZANZIBAR .TAZAMA PICHA HAPA

Baada ya kuwasili uwanja wa ndege Zanzibar

Akifanya mahojiano na waandishi wahabari.

Mashabiki wakisubiri  kwa hamu kumwona the president


Akizungumza na mashabiki wake wa zanzibar ndani ya kituo kikubwa kabisa cha Radio Zanzibar.Coconut Radio

Baadae alikutana na waandishi wa habari ndani ya hotel ya kisasa kabisa,Zanzibar beach  lesort

Wanahabari kazini





















Friday, September 27, 2013

FEDHA IMESHINDWA KUZUIA KIFO TU,BABU WA LOLIONDO AWA KIJANA,TAZAMA PICHA BEFORE AND AFTER KIKOMBE


Duh.acha pesa iitwe pesa....
jamaa alikuwa mzee kabisa sasa ona uso kama kijana kabisa!

KWA MARA YA KWANZA IANPHI KUFANYA MKUTANO WAKE WA NANE NCHI TANZANIA


Picture
Dk Mwele Malecela
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kuratibu mkutano wa nane wa mwaka wa taasisi hiyo na kupata nafasi ya kuing'arisha nchi katika 
ramani ya dunia na hatimaye kuweza kutangaza maliasili zake na vivutio vya Utalii vilivyomo.

Mkutano huo wa nane wa IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka huu jijini Arusha katika Hoteli ya Ngurdoto. 
Picture
Akizungumza hii leo jijinni Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii (IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela amesema mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama.

Dk Malecela ameimabia “Father Kidevu Blog”, katika ofisi zake za NIMR jijini Dar es Salaam hii leo kuwa mkutano huo unataraji kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi.

Makamu huyo wa Rais wa IANPHI Daktari. Mwele amesema kuwa wanachama wa taasisi hiyo watakao shiriki katika mkutano huo hususan wakuu wa Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii watapa fursa ya kujadili masuala muhimu ya afya ya jamii: kugbadilishana uzoefu na kubuni mbinu za kitaalam za kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya afya ya jamii.

"Mkutano pia utatoa nafasi kwa washiriki kujadili mbinu za kukuza ushirikiano ili kuimarisha afya ya jamii kuelekea mwaka 2015, ambapo mataifa yamejiwekea nia ya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG's).

Kauli mbiu katika mkutano huo wa mwaka 2013 ni "Afya ya Jamii baada ya mwaka 2015 na mabadiliko ya majukumu ya Taasisi za kitaifa za afya ya Jamii."

Chama hicho cha IANPHI kina wanachama 81 huku makao makuu ya Sekretarieti yake yakiwa mji wa Helsinki, Finland.

TRUE STORY,BINTI AOGELEA NA KICHANGA HADI KUFANIKIWA KUJIOKOA ZIWA TANGANYIKWA,13 WAFARIKI DUNIA





MWANAFUNZI wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Kipwa mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa mwenye miaka minane ameweza kujiokoa yeye na mtoto wa dada yake mwenye umri wa miezi mitano kwa kuogelea hadi ufukweni baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama kwenye ziwa Tanganyika. Manusura huyo aliyefahamika kwa jina moja la Prisca akiwa miongoni mwa wengine 15 walinusurika kufa maji ama kwa kuogelea au kuokolewa alipoona mtumbwi huo ukizama, inadaiwa alipiga mbizi majini akiwa na mtoto huyo mchanga mgongoni mwake na kuweza kuogelea kwa saa kadhaa hadi ufukweni wote wakiwa hai. Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Kipwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyika , Benson Silinjile alithibitisha mkasa huo wa aina yake akisema msichana huyo Prisca alikuwa amempeleka mtoto huyo kupata chanjo katika kituo cha afya kijijini Kapele kwa kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa mgonjwa hivyo alimwomba msaada huo. Licha ya msichana huyo kuweza kujiokoa yeye na mtoto huyo mchanga kwa kuogelea hadi ufukweni pia nahodha wa mtumbwi huo uliopata ajali hiyo iliyosababisa vifo vya watu 13 wakiwemo wanawake na watoto wenye umri chini ya miaka mitano , Lazaro Sikapote (26) aliweza kuokoa familia yake akiwemo mama yake mzazi Rose Sikapote , mkewe Rakadia Sikazwe na mwanae aliyefahamika kama Nazaro Sikapote........

BIBI HUYU ASIKIA SAUTI YA MUNGU,AAGIZWA KUONANA NA RAIS KIKWETE


Amani usiamini! Bibi kizee Veronica Amos Kayombo (76), mwenyeji wa Ludewa, Njombe anayeishi Buza, Dar, amedai kuisikia sauti ya Mungu ikimuagiza akaonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ampe ujumbe muhimu, shuka nayo.

MAHOJIANO MAALUM
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum mwanzoni mwa wiki hii akiwa nyumbani kwake Buza, Bibi Veronica alisema amekuwa akitokewa na Mungu mara kwa mara na kumpa maelekezo mengi ambayo anatakiwa kuyatoa pale atakapofika kwa Mheshimiwa Rais Kikwete.
 
ATOKEWA NA TASWIRA YA MUNGU
“Nimekuwa nikitokewa na taswira na sauti ya Mungu, kwa idadi inaweza kufika mara saba na kuambiwa
kuwa nisiondoke Dar, bila kuonana na Kikwete ili nimpe zawadi zake ambazo nimezitunza kwa muda mrefu na siri iliyoko moyoni ambayo nimepewa na Mungu,” alisema bibi kizee huyo.
 
KWA NINI JK?
Aliendelea kusimulia kwa masikitiko kuwa zawadi atazompatia JK ni kwa ajili ya kumpongeza kwa kuweza kuwasaidia albino, watu wasiojiweza, wazee na kutuliza vita nchini Kenya na Uganda ambazo zilikuwa zimejifichwa kwani nchi nyingine kama Rwanda na Burundi zilikuwa wazi.


ANATOKEA NJOMBE
Bibi Veronica alifika Dar akitokea Njombe kwa ajili ya mazishi ya mama yake mdogo na baada ya kumaliza msiba alijiandaa kuondoka lakini Mungu alimtokea 6:00 mchana na kumweleza kuwa asiondoke hadi atakapoonana na JK. 
ATUMIA MKWANJA MREFU
Baada ya hapo amekuwa akifanya jitihada za aina mbalimbali kwa ajili ya kuonana na rais lakini hadi sasa hajafanikiwa kwani ameshapoteza fedha nyingi kwa kuwahonga watu ili wamfikishe Ikulu pale Magogoni, Dar na kutoa kopi za barua kwa ajili ya kuomba maombi ya kukutana naye.
“Nimepoteza fedha nyingi sana kila ninayekutana naye ananiambia atanipeleka lakini nimpatie fedha, natoa mpaka sasa nimeishiwa, nimeshaenda mpaka ofisi zote zinazohusika na kuwakutanisha watu na rais lakini sikufanikiwa, watu wamekuwa wakiniona chizi lakini nina akili zangu timamu na maono haya ni ya Mungu kwani mbali na kuambiwa pia la kufanya nikifika huko lipo kwenye kitabu hiki (anaonesha Biblia).
Bibi kizee huyo alipoona ameshahangaika huku akizuia kila mara kuingia Ikulu, aliamua kuita vyombo mbalimbali vya habari na kufikisha ujumbe wake ambapo mbali na hapa gazetini pia radio zitarusha matangazo yake moja kwa moja yatamfikia Rais Kikwete. 
AMPA ZAWADI LOWASSA, MKAPA
Kwa mujibu wa bibi Vero, aliwahi kukutana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye alimpatia gunia la mahindi na zawadi za Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Mama Ana Mkapa alipokuwa kwao Njombe.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa mama huyo wakati anatoa zawadi hizo alioneshwa kwenye vyombo vya habari ambapo alitoa kitenge cha mama, gunia la mahindi na zawadi ya rais huyo mstaafu

ORODHA YA WASANII 10 WA MUZIKI BONGO WALIOTENGENEZA FEDHA NYINGI ZAIDI MWAKA HUU 2013


Biashara ya muziki Tanzania imeendelea kupanuka kwa kiasi kikubwa, na wasanii wenye hits, majina, connection, bahati na sababu zingine wameendelea kuingiza fedha nyingi kutokana na muziki wao.
Njia kubwa na za uhakika zinazowapatia mapato wasanii ni pamoja na malipo ya show, malipo ya ringtones, endorsements (mfano kuwa mabalozi wa brands mbalimbali na kufanya matangazo) na wengine kupata kipato kupitia biashara walizozianzisha.
Kama njia kubwa zingine mbili za kuwaingizia kipata wasanii wengi duniani zingefanikiwa nchini, wasanii wetu wangekuwa mbali zaidi. Njia hizo ni mauzo ya albam za muziki na malipo ya mirahaba kutokana na matumizi ya nyimbo zao kwenye kumbi za starehe na kwenye vituo vya radio au TV.
Licha ya kuwepo kasoro hizo, bado Bongo Flava imebadilisha maisha ya wasanii wengi.
Bongo5 imejitahidi kukusanya kadri iwezavyo, data za uhakika kutoka kwa watu walio karibu na wasanii kadhaa wa Tanzania kutaka kufahamu, kiasi walichoingiza, malipo waliyoyapata mwaka huu na data zingine zingine, kuandaa orodha hii ya wasanii 10 walioingiza fedha nyingi zaidi mwaka 2013.
Wafuatao ni 10 waliongiza fedha nyingi zaidi mwaka 2013.

1. Diamond Platnumz
Hakuna ubishi kuwa, mwaka 2013 Diamond Platnumz ndiye msanii aliyeingiza fedha nyingi zaidi. Pesa nyingi ya Diamond imetokana na malipo ya show zake za ndani na nje ya nchi. Kwa uhakika, mwaka huu pekee, Diamond amefanikiwa kuingiza takriban shilingi bilioni 1.
Kwa show za ndani peke yake, Diamond hutoza si chini ya shilingi milioni 10 ama 15 na kila wiki hufanya show zaidi ya 2. Hivyo tangu mwaka uanze, Diamond amekuwa akiingiza shilingi milioni 40 kila wiki. Tour za nje alizofanya mwaka huu ni pamoja na zile za Uingereza ambako alifanya show kwenye miji mitatu, show ya Burundi na Congo, show mbili za Kenya (Nairobi na Mombasa), show ya nchini Comoro ambako alilipwa si chini ya dola 30,000 na show ya Malaysia wiki iliyopita.
Kwa upande wa show za hapa nyumbani ambazo ni nyingi mno zisizo na idadi, ukiachana na zile za kawaida, Diamond aliingiza shilingi milioni 40 kwenye show 4 za Kili Music Tour ambapo kila show alilipwa shilingi milioni 10. Ndiye msanii aliyelipwa fedha nyingi zaidi kwenye ziara hiyo.
Pia amefanya show kadhaa za Fiesta 2013, show za promotion za Tigo na makampuni mengine, Tamasha la Matumaini, show ya Tulizana Tuko Wangapi ya Leaders Club, show yake na Nay wa Mitego (Dar Live na Maisha Club). Mwezi February 16 mwaka huu, Diamond alifanya show jijini Arusha ambayo kiingilio chake kilikuwa ni shilingi 150,000 ndani ya Club Safari na ukumbi kufurika.
Miezi kadhaa iliyopita pia hitmaker huyo wa ‘Number 1’ ameshaalikiwa kwenye show corporate kuburudisha wafanyakazi wa benki na taasisi zingine pamoja na watu binafsi na zote hizo zimemuingizia fedha nyingi. Pamoja na show, Diamond amekuwa akiingiza fedha nyingi zaidi kwenye malipo ya ringtones ambapo kila baada ya miezi mitatu amekuwa akiingiza si chini ya shilingi milioni 20. Kwa mujibu wa Push Mobile, akaunti ya Diamond kwenye kampuni hiyo ndio inayoingiza fedha nyingi kuliko msanii mwingine yeyote wa Bongo Flava.
Mkataba exclusive alioingia na kampuni ya simu ya Vodacom kuuza wimbo wake mpya My Number One kama muito wa simu, umezidi kumpandisha juu na ikidaiwa kuwa mkataba huo ni wa mamilioni ya shilingi.
Ikumbukwe pia, Diamond ni balozi wa Cocacola. Mkataba huo ambao haijajulikana umemuingizia shilingi ngapi, lakini ni fedha inayoweza kuwa si chini ya shilingi milioni 100.
Diamond ni miongoni mwa wasanii wengine 23 wa Afrika akiwemo Lady Jaydee kwenye mradi mkubwa wa Cocacola wa Coke Studio Africa.
2. Lady Jaydee
Huwezi amini, vuguvugu la Anaconda limemsaidia Jaydee si tu kukusanya mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi mno. Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100. Haikuishia hapo, albam yake Nothing But The Truth ilinunuliwa kwa kiasi kikubwa na kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya albam zake.
Hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye albam yake hiyo, zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki mwenye show nyingi zaidi pia. Lady Jaydee ametumbuiza kwenye karibu show zote za Kili Music Tour ambako ameingiza shilingi milioni 25.
Mwaka huu pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu, Foolish Age, show yake kwenye Miss Tanzania 2013, Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili, Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi za albam yake kama njugu pamoja na tiketi za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja.
June mwaka huu pia, Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini, iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge, imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda kupata chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi.
Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya.
Coke Studio Africa – the new, exciting music show featuring incredible live performances by the very best in Africa
3. AY
Humsikii sana rapper huyu kwenye show za Tanzania. Tofauti na wasanii wengine, fedha anazoingiza AY zinatokana zaidi na endorsements na biashara zake anazofanya. Pesa nyingi alizoingiza zimetokana na mkataba wa mwaka mmoja na Airtel wa ubalozi uliokamilika mwezi May mwaka huu.
Katika ubalozi huo wa Airtel Africa, AY aliungana na wasanii wengine watatu wa Afrika ambao ni pamoja na Papa Wemba, Tuface na Daddy Owen wa Kenya. Katika mkataba huo AY alilipwa dola za Kimarekani 80,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 129.
Rapper huyo wa ‘Machoni Kama Watu’ ni balozi pia wa bia ya Peroni ya Italia na kupitia mkataba huo, AY ameingiza mkwanja mwingi. AY pia ni mwanzilishi mwenza wa kipindi cha Mkasi kinachoendeshwa na Salama Jabir. Kipindi hicho kina wadhamini wawili, Cocacola na Airtel na hivyo kupitia mgawanyo wa mapato, AY amekuwa akiingiza pia fedha ya kutosha.
AY ni CEO wa kampuni ya Unity Entertainment inayojihusisha na kuandaa show, matangazo, kuleta wasanii wa nje na mambo mengine. Mwaka huu pekee, ikishirikiana na kampuni ya SK Entertainment, kampuni yake imeandaa show kibao zikiwemo zile zilizofanyika Elements Lounge ambapo Avril, Prezzo, Huddah Monroe na J-Martins wamewahi kuhudhuria.
Maisha ya kawaida ya rapper huyu ndio yanayowafanya watu wengi wasijue ukubwa wa kile anachokiingiza. Macho yake ameyaelekeza zaidi kwenye uwekezaji na anawekeza haswaa. Kuna tetesi kuwa, AY anajenga ghorofa lake maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. Anasemekana kuwekeza pia mkoani Mtwara alikonunua ardhi ya kutosha. Mungu ndio anajua ni wapi alikowekeza tena.
4. Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya muziki nchini Marekani ameingiza fedha zake nyingi kupitia show alizofanya. Ziara zake za Ulaya na Marekani pekee zimemuingizia dola 50,000 ambazo ni sawa shilingi milioni 81.
Tangu aachie wimbo wake mpya Tupogo, tayari Ommy ameshaingiza shilingi milioni 50. Kwenye show yake ya hivi karibuni ya Tupogo Night iliyofanyika Club Billicanas, Ommy alipeleka nyumbani shilingi milioni 10 baada ya kukata gharama zote. Watu 1,770 walihudhuria show hiyo.
Show yake ya Burundi ya mwanzoni mwa mwezi uliopita ilimuingizia staa huyo shilingi milioni 30. Ommy hutoza si chini ya shilingi milioni 7 kwa show na kwa mwezi, amekuwa na uhakika wa kufanya show tatu ama nne za ndani bila kusahau show za Kili Music Tour.
Hivi karibuni kwenye segment ya Tell it All ya Bongo5, Ommy alifunguka kuwa makampuni mengi yamekuwa yakimfuata kumpa endorsements lakini msimamo wake wa kutaka kulipwa fedha ya uhakika imemfanya azikatae nyingi lakini yupo mbioni kupata deal kubwa. Mpaka sasa Ommy anajenga nyumba mbili kwa mpigo zenye thamani ya shilingi milioni 250 hadi zilipofikia. Tayari ana viwanja vingine viwili anavyotaka kuangusha mijengo mingine. Hivi karibuni pia atakuja na clothing line yake ya PKP.
5. Madee
Hii inaweza kuwa surprise kwa wengi lakini Madee ni mfano tosha wa jinsi single moja inavyoweza kubadilisha maisha ya msanii. Tangu atoe single yake, Sio Mimi, Madee ameshaingiza si chini ya shilingi milioni 200.
Mwaka huu ameshafanya show 10 za kampeni ya Tigo ambapo kila moja alilipwa shilingi milioni 3, show 15 za Airtel kwa kiwango hicho hicho. Alifanya show mbili za kampeni za Coca Cola, ile ya uzinduzi wa Coke Zero na Cocacola Bonanza Mlimani City. Bado ameendelea kufanya show za Fiesta 2013. Madee pia alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye show ya Fuse ODG iliyofanyika September 7 kwenye viwanya vya ustawi wa jamii jijini Dar es Salaam.
6. Mwana FA
Mwanzoni mwa mwaka huu, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA alikuwa msanii wa tatu miongoni mwa wasanii waliongiza fedha nyingi kupitia malipo ya miito ya simu, RBT ambapo aliingiza shilingi milioni 18. Alifanya show mbili kwenye Kili Music Tour ambapo aliingiza si chini ya shilingi milioni 7 pamoja na show kadhaa za Fiesta 2013.
Show yake ya The Finest ilimuingizia shilingi milioni 19. Hivi karibuni alichukuliwa na kampuni ya Vodacom kuzunguka baadhi ya mikoa kwenye kampeni yao na CCBRT kuhusiana na kukuza uelewa wa tatizo la Fistula na kulipwa mkwanja kama balozi wa kampeni hiyo.
Mwaka huu FA amefanya matangazo kadhaa ya Vodacom. Hivi karibuni pia aliingia kile kilichoonekana mkataba kama balozi wa simu za Samsung Galaxy Tanzania japo haijulikani kama ulikuwa mkataba wa ubalozi kama ilivyo mingine.
Mwana FA pia amefanya show za nje zikiwemo za Kenya na Afrika Kusini aliyofanya siku ya Eid mwezi uliopita. Kama wasanii wengine pia, FA ameingiza fedha nyingi kwa show za kawaida za hapa nyumbani na zile za promotion.
7. Chege
Mwaka huu Chege peke yake alifanya show sita nje ya nchi ambazo kila show alilipwa shilingi milioni 4. Akiwa na Temba ambao kwa pamoja hutoza shilingi milioni 6, Chege amefanya show zaidi ya 30 zikiwemo zile za Fiesta, za promotion mbalimbali na zile za kawaida.
Mwezi ujao yeye na Temba wataanza tour ya miezi mitatu barani Ulaya ambapo show ya kwanza itakuwa nchini Sweden, October 5. Pamoja na hivyo, Chege ana biashara ya salon.
8. Profesa Jay
Profesa Jay aliingiza shilingi milioni 20 za Kili Music Tour, alifanya show kubwa ya Jose Chameleone April mwaka huu, show kibao za promotion za makampuni, show ya kampuni ya IPP kwaajili ya Walemavu, Diamond Jubilee mwezi January, na show zingine za kawaida za Dar na mikoani. Pia nguli huyo wa rap ya Tanzania ameingiza fedha nyingi kupitia show nyingi za Lady Jaydee.
Prof J amewekeza kwenye biashara ya salon ambayo tayari inafanya vizuri na ameshafungua studio ya kurekodi muziki iliyopo kwenye hatua za mwisho kuanza kazi. Jize aliingiza pia fedha kupitia kampeni ya magazeti ya Mwananchi kwa kufanya matangazo na show za mikoani.
9. Nay wa Mitego
Tangu mwaka uanze, Nay wa Mitego ameshafanya show zaidi 20 zilizomuingizia si chini ya shilingi milioni 60. Show hizo ni pamoja na zile za promotion za makampuni ya simu, show mbili za Muziki Gani, show ya Kili Music Tour, show za Fiesta na zile za kawaida. Pia ana biashara zake ambazo kwa pamoja humuingizia si chini ya shilingi milioni 4 kwa mwezi.
10. Temba
Fedha nyingi alizoingiza Temba mwaka huu zimetokana na show walizofanya pamoja na Chege. Ukitoa muziki, Temba pia ni mfanyabiashara na anamiliki duka la vifaa vya ujenzi.

Source:Bongo5.com

Sunday, September 22, 2013

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA REDD'S MISS TANZANIA LILIVYOFANYIKA USIKU WA KUAMKIA LEO...!!



Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kulia  ni mshindi wa tatu,Clara Bayo.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakifungua shindano la mwaka huu kwa kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano la mwaka huu ambalo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania  ya Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.

 Warembo walioingia hatua ya kumi na tano bora. 

 Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Dkt. Ramesh Shah akitangaza Warembo walioingia hatua ya tano bora.
Warembo walioingia hatua ya tano bora,toka shoto ni Happiness Watimanya,Elizabert Peter,Clara Bayo,Lucy Tomeka pamoja na Latifa Mohamed.