Pages


Photobucket

Friday, January 31, 2014

Chadema kususia Bunge la Katiba

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema wabunge wa chama chake watasusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba ikiwa hoja ya kuundwa kwa Serikali tatu itapingwa na wabunge wa CCM, Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu ametaka kuvunjwa kwa Muungano.
Akihutubia kwenye Uwanja wa Tubuyu nje kidogo ya Mji wa Morogoro juzi, Mbowe alisema wabunge wa chama chake wataandamana nchi nzima kufikisha ujumbe kwa wananchi kwamba maoni yao yamepingwa na wabunge wa CCM walio wengi.
“Tutawaeleza wananchi kwamba maoni ya CCM ndiyo yameonekana ya maana kuliko ya wananchi ambao ni wengi zaidi,” alisema Mbowe kwenye mkutano huo ambao ni sehemu ya Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko - M4C Pamoja Daima.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikusanya maoni na kubaini kuwa asilimia 62 ya Watanzania wanataka Serikali tatu za Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano.
“Serikali ya CCM haitaki kusikia maneno Serikali tatu wanasema sera yao ni ya Serikali mbili, wanafanya kila hila ili kuikataa hoja hiyo. Natangaza kwamba wakifanya hivyo tutasusia na kwenda kuwashtaki kwa wananchi,” alisema Mbowe.
Aliongeza kwamba wataandamana kuanzia Kagera hadi Mtwara kuwaeleza wananchi kwamba hoja yao imepingwa na CCM.
Mbowe alisema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakitoa kashfa dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwamba amechukua maoni ya Chadema.
“Wanakosea hayo si maoni ya Chadema, bali ni maoni ya wananchi, Warioba amezingatia maoni ya wananchi,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Katiba inayotafutwa si ya chama, bali ni ya Watanzania na kwamba inashangaza CCM kuipinga hoja Serikali tatu.
“Tunafahamu wanaogopa kuikubali hoja ya Serikali tatu kwa sababu wanafahamu huo ndiyo utakuwa mwisho wao wa kuwa madarakani,” alisema Mbowe huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.
Alisema CCM wanaelewa kwamba kukiwa na Serikali tatu, Chadema kitashinda Tanganyika na CUF Zanzibar katika uchaguzi wowote utakaoitishwa.
“Kwa hiyo hivi sasa wana wasiwasi kweli, wanatafuta kila njia ya kuichakachua hoja ya Serikali tatu lakini wafahamu kuwa Chadema wanaifuatilia hoja hiyo kwa ukaribu,” alisema.
Aliwataka wananchi kufuatilia Bunge Maalumu la Katiba litakapoanza mwezi ujao ili kuangalia wabunge wao wanavyowawalisha katika suala hilo muhimu.
Hata hivyo, Mbowe alisema chama hicho kikishinda katika uchaguzi wa mwaka 2015 hakitahangaika kulipa kisasi kwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi, bali kitajikita kutafuta maendeleo.
“Wasituogope tutasamehe kama alivyosamehe aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Hatutalipa kisasi tukiingia Ikulu, kwa sababu hakuna binadamu asiye na makosa. Tutaelekeza nguvu zetu kuwaletea maendeleo Watanzania,” alisema Mbowe.
Jussa na Muungano
Akihutubia mkutano wa kampeni katika Jimbo la Kiembesamaki jana, Jussa alisema hakutakuwa na maendeleo yatakayofikiwa Zanzibar ikiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hautang’oka.
Jussa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF, alisema Zanzibar yenye watu milioni 1.5 haiwezi kuwa na tatizo la watu kukosa ajira lakini sera na mipango ya kiuchumi imekuwa ikikwama katika utekelezaji wake kutokana na kukosa mamlaka kamili.
Alisema Zanzibar haiwezi kukopa katika taasisi za kimataifa bila ya kuwekewa dhamana na Waziri wa Fedha wa Muungano wakati Zanzibar ni nchi na kuwataka wananchi kutumia kura zao katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuleta mabadiliko ya kiutawala.
“Hakuna sababu ya vijana Zanzibar kukosa ajira, kuna watu wasiozidi milioni 1.5, Muungano umefika wakati ung’oke, ndiyo kikwazo cha maendeleo ya Zanzibar na watu wake kiuchumi na kisiasa,” alisema Jussa.
Alisema mradi wowote unaobuniwa Zanzibar hauwezi kupata mfadhili bila kuwekewa dhamana na Serikali ya Muungano na kukwama kwa juhudi zote za kujiunga na jumuiya za kimataifa akitolea mfano Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC).
Alisema Rais wa Zanzibar amepoteza mambo muhimu chini ya mfumo wa Muungano ikiwa ni pamoja na kutopigiwa mizinga 21 akiwa nje ya nchi, kupeperusha bendera ya Zanzibar, kutokagua gwaride na kupigiwa wimbo wa Taifa la Zanzibar.
“Haya ya sasa si mamlaka kamili, wapi Dk Shein alikokwenda akapigiwa mizinga 21 au alipeperushwa wapi bendera ya Zanzibar wakati wa safari zake za nje?” alihoji Jussa.

FIRST MEETING OF THE AFRICAN AMBASSADORS IN THE AFRICA HOUSE

 Balozi wa African Union nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali (kulia) akiongoza mkutano wa kwanza wa Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwenye jengo jipya la ofisi ya African Union lililopo Georgetown, Washington, DC. siku ya Jumatano January 29, 2014
 Waheshimiwa Mabalozi waliohudhuria mkutano huo wa kwanza wa Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwenye jengo jipya la ofisi ya African Union lililopo Georgetown, Washington, DC. siku ya Jumatano January 29, 2014.

 Waheshimiwa mabalozi wakifuatilia mkutano wa kwanza wa Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwenye jengo jipya la ofisi ya African Union lililopo Georgetown, Washington, DC. siku ya Jumatano January 29, 2014

D’BANJ NA YAYA TOURE WAUNGA MKONO KAMPENI YA KILIMO YA RAIS KIKWETE

page
D’Banj alishirikiana na washirika wa Kilimo wa Afrika katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Shiriki Kilimo’ (Do Agric) kwenye kongamano la Umoja wa Afrika. Kampeni hiyo inalenga kuwasaidia watu zaidi ya milioni 85 barani Afrika kutoka katika lindi la umasikini kupitia uwekezaji maalumu katika kilimo na sera za kilimo za Maputo zilizoboreshwa.
D’Banj alikuwa mmoja wa waliozungumza Addis Ababa jana wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo yenye lengo la kuwahamasisha viongozi wa kisiasa kutumia sera nzuri zitakazonyanyua uzalishaji, kuongeza kipato na kuondoa mamilioni ya Waafrika kutoka katika umasikini.
“Nataka Waafrika kufahamu kilimo ni msingi mzuri wa uchumi ambacho kinatakiwa kutiliwa mkazo na kuleta mabadiliko katika uchumi wa wananchi na nchi na pia tukitilia mkazo tunaweza kuilisha dunia nzima kwa ujumla sisi kama Waafrika,” alisema D’Banj.
Kwa upande wake mchezaji wa timu ya Manchester City, Toure alisema wakati viongozi wengine wa Kiafrika wakitoa kauli zenye nia njema, kwa sasa ni nchi 8 tu zililizotimiza ahadi zake za kuwekeza 10% ya bajeti za nchi katika kilimo.
“Kwahiyo ni muhimu kufanya zaidi na kwenda mbele zaidi. Kilimo sio muhimu pekee, pia ni lazima. Kilimo kinalipa,” alisemaToure.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na asasi mbalimbali za kiraia zikiwemo Pan African Farmers Association (PAFO), Action Aid International , Acord International, Oxfam na Alliance for Green Revolution In Africa (AGRA) mbali na asasi hizo mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure pia ametia saini kuunga mkono uhamasishaji huo.
Source:Habari leo

JUSTIN BIEBER AJISALIMISHA POLISI NCHINI CANADA KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA DEREVA WA LIMO

Bieber mwenye miaka 19 alijisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha polisi jijini Toronto ambako alizungukuwa na kundi kubwa la maripota wa TV, wapiga picha na mashabiki wake waliokuwa wakishangilia. Kesi hiyo inakuja ikiwa ni wiki moja baada ya kushikiliwa na polisi kwa kosa jingine huko Miami kwa kuendesha gari akiwa amelewa. Hata hivyo wakili wa muimbaji huyo amesema mteja wake hana hatia.
Polisi jijini Toronto wanasema Justin Bieber alikuwa miongoni mwa watu sita waliochukuliwa na limousine nje ya klabu ya usiku December 30. “Wakati kundi hilo linapelekwa hotelini, ugomvi ulitokea kati ya abiria mmoja na dereva wa limousine hiyo,” maelezo ya polisi yalisema.
Maelezo hayo yamedai wakati wa vurugu huyo, mmoja wao alimpiga dereva nyuma ya kichwa chake mara kadhaa na hivyo limousine kusimama na dereva akaita polisi lakini mtu aliyemshambulia dereva huyo alikimbia.
Kutokana na kosa hilo, Bieber atapanda kizimbani kwenye mahakama ya Toronto, March 10.
Mapema Jumatano hii, jumla ya sahihi 100,000 zilikusanywa kupitia website ya ikulu ya Marekani zinazodai Bieber afukuzwe nchini Marekani. Rais wa Marekani hana mamlaka ya kuagiza kufukuzwa kwa mtu na haijulikani kama White House itajibu malalamiko hayo.

Magazeti ya leo January 31 2014

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Thursday, January 30, 2014

PICHA KIJANA ALIYEGONGWA NA TRENI BAADA YA KUWEKA HEADPHONE MASKIONI



Jamaa mmoja amekubwa na mkasa wa aina yake pale alipogongwa na treni ambayo ilikuwa na kazi kubwa ya
kumpigia honi ili atoke pembezoni mwa reli alipokuwa akitembea. Walioshuhudia tukio hilo wamesema treni hiyo ilipiga honi lakini jamaa alikuwa ameweka Head phones masikioni. 
Credit:Udaku Specially

MABASI YA MWAKYEMBE YAANZA KUTESA APA MUJINI BONGO LIVE!!


 Basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar.