Saturday, June 8, 2013
MSHINDI WA KUTWEET WAZO JIPYA LA KUONDOA UMASKINI APATIKANA NA KUKABIDHIWA MILLION MOJA .
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi
akimkabidhi kitita cha shilingi milioni moja
mshindi wa kwanza wa shindano la, "Tweet Wazo
Jipya Kuondoa Umaskini", Jilly Gaudence Kyomo katika
hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management
and Enterprenuership, Dkt. Donath Olomi.
Kulia ni mshindi wa pili, Peter George aliyejinyakulia
shilingi laki tano na mwanafunzi wa
chuo cha CBE, Ludovick Angelino, ambaye ni
mshindi wa tatu aliyejinyakulia shilingi laki tatu
Dkt.Reginald Mengi,ameanzisha kampeni kupitia
twitter inayoitwa "tweet wazo jipya kuondoa umaskini"inayotaka
mtanzania yeyote kumtweet Reginald mengi tweet yenye wazo zuri juu ya namna ya
kuondoa umaskini nchini na mtu atakaye tweet
itakayomgusa huyo ndiye atakuwa mshindi wa million 1 ,mshindi
atakuwa akipatikana kila mwezi.
Hongera Bwana Mengi kwa kuja na wazo jema kama hilo.
DIVA WA CLOUDS FM NAYE ATOA PICHA YA NUSU UCHI ILI KUMTEKA PREZZO ANAYEONEKANA KUHAMISHIA PENZI KWA HUDDAH
Baada ya huddah kuweka picha yake akiwa na prezzo na kuzua gumzo mitandaoni, Diva wa clouds fm ameamua kuweka picha yake
ya NUSU UCHI ili
kupotezea Aibu hiyo..
"Love at the first sight imekwishaimekwisha."....
Ulimpiga KIBUTI mbunge mh. JEPESI , tena kwa mbwembwe, vijembe na kejeli kibao mtandaoni......
Leo hii jamii inashuhudia unavyoumbuka.Penzi la Huddah na Prezzo lilikuwa wazi na la vitendo.....
Siku
moja kabla ya kutolewa katika jumba la big brother, Huudah
aliweka wazi juu ya uhusiano wake na Prezzo huku akielezea
jinsi alivyo miss kushikwa shikwa...!!
Prezzo na mpenzi wake....
Nani alikurupuka kati yake na wewe???
Si mbaya sana, ENDELEA KUWEKA PICHA ZA UCHI, PENGINE ATAHAMISHIA PENZI KWAKO
YAKIWA YAMEBAKI MASAA MACHACHE TAIFA STARS KUSHUKA DIMBANI NA MOROCCO,KOCHA POULSEN AWATOA HOFU WATANZANIA
“Wachezaji wako katika hali nzuri kabisa na
wana ari ya kushinda mechi hii…tuna nguvu na tunajua namna ya kuwapiga Morocco,”Akaongeza kwa kusema,swala si mchezaji
gani anaanza au washambulizi ni wangapi, bali ni
kazi itakayofanyika uwanjani na ubora wa
wachezaji wa Taifa Stars, Alisema Morocco ni timu kubwa
na ina wachezaji wengi wa kulipwa
lakini inafungika na Taifa Stars itaweka
nguvu kuanzia mwanzo wa mechi.
“Unapocheza mechi kama hii inabidi uweke nguvu
dakika za kwanza za mechi ili umpe mpinzani
wakati mgumu kwa hivyo dakika za mwanzo zitakuwa
muhimu sana katika mechi hii,” alisema.
Poulsen alisema baadhi ya watu nchini Morocco bado
wanaamini kuwa ushindi wa mechi ya awali Jijini
Dar es Salaam wa 3-1 dhidi ya Morocco ulikuw
a wa kibahati tu. “Tunataka kuwadhihirishia kuwa
tunaweza na Taifa Stars sio timu ndogo kama wanayodhani.”
Akizungumzia swala la kuwekewa mazingira
mabaya ya kambi pale wanapocheza mechi za nje,Poulsen
alisema mazingira ya kambi ni mazuri kabisa na
wachezaji wote wako katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huu...
“Katika hali ya kawaida ungetegemea hujuma nyingi
ikiwemo hoteli mbovu, viwanja vibovu vya mazoezi na
kadhalika lakini hapa ni tofauti kabisa…kwani
mazingira ni mazuri,” alisema Poulsen.
Taifa Stars imeweka kambi katika Hoteli ya Pullman
iliyoko nje kidogo ya Mji wa Marrakech.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Taifa stars.
Saturday, June 1, 2013
MUSHARAF AKAMATWA TENA.
ISLAMABAD-PAKISTAN,
Polisi nchini Pakistan wamemkamata rais wa zamani wa nchi hiyo Pervez Musharraf, kutokana na agizo la Mahakama siku ya Alhamisi.
Hatua ya kukamatwa kwa Musharraf ilitolewa na Mahakama hiyo kutokana na uamuzi wake wa kuagiza kifungo cha nyumbani kwa Majaji nchini humo mwaka 2007 akiwemo Jaji Mkuu.
Musharraf, alikamatwa nyumbani kwake nje kidogo ya mji wa Islamabad siku ya Ijumaa na kufikishwa Mahakamani huku serikali ikisema nyumba yake itakuwa jela kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo.
Kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi ameonekana siku ya Ijumaa akisindikizwa na polisi Mahakamani na tayari anazuiliwa rumande kwa siku mbili kabla ya kupewa kifungo cha nyumbani.
Hii ni ndio mara ya kwanza kwa Mahakama nchini humo kutoa agizo la kukamatwa kwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo ambaye pia alikuwa Mkuu wa Majeshi.
Wakati uo huo, Mahakama mjini Islamabad imeanza kusikiliza kesi ya uhaini dhidi ya Musharraf kwa kuagiza kuwepo kwa sheria ya hatari nchini humo mwaka 2007 na ikiwa atapatikana na kosa atahukumiwa kifo au kufungwa maisha jela.
Kiongozi huyo wa zamani pia anatuhumiwa kupanga mauaji ya kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto mwaka 2007.
Musharraf mwenye umri wa miaka 69 alikuwa rais wa kumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 2001 hadi 2008 kabla ya kujiuzulu na kukimbilia ukimbozini jijini London nchini Uingereza.
Musharraf alirudi nyumbani mwezi uliopita kutoka Dubai alikokuwa anaishi, na kusema kuwa amerudi nyumbani ili kuikoa Pakistan hatua iliyokaatiliwa na tume ya uchaguzi nchini humo.

ZAIDI YA WATU 56 WAFARIKI KWA KIMBUNGA TONARDO
OKLAHOMA -MAREKANI,
Kimbunga kikubwa cha Tornado kimeukumba mji wa Oklahoma mapema leo Jumatatu na kubomoa vitalu vya nyumba, shule mbili na kuua takribani watu 91 ikiwa ni pamoja na watoto 20, viongozi wa mitaa wamearifu.
Ofisi ya mtabibu wa serikali imetoa taarifa ya karibuni kuhusu idadi ya waliopoteza maisha lakini idadi hiyo inaongezeka kwa kasi, wakati kikosi cha huduma ya dharura wamesafisha mabaki yote ya nyumba zilizobomolewa pamoja na shule katika kitongoji cha Moore mjini Oklahoma.
Watabiri wa hali ya hewa wamearifu kuhusu uwepo wa upepo mkali wa maili mbili, na helikopta ya habari za televisheni imenasa faneli zito likipita katika vitongoji kadhaa.
Gavana wa Oklahoma Mary Fallin ameviambia vyombo vya habari kuwa kimbunga hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea katika eneo hilo akiongeza kuwa majeruhi ni wengi na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu umefanyika.
Naye mkuu wa polisi katika kitongoji cha Moore Jerry Sillings amewataka wakazi wa kuondoka katika eneo hilo wakati masuala kadhaa ya kiusalama yakifanyika.(RFI SWAHILI).
293 WAKAMATWA KWA KUPINGA NDOA ZA JINSIA MOJA UFARANSA.
PARIS-UFARANSA,
Polisi jijini Paris, Ufaransa wamekabiliana na maelfu ya waandamanaji
wanaopinga sheria iliyoidhinishwa na bunge kuruhusu ndoa za watu wa
jinsia moja.
Maandamano hayo ambayo awali yalianza kwa amani yaligeuka kuwa vurugu pale ambapo polisi walilazimika kuingilia kati kuwatawanya waandamanaji hao ambao walianza kuharibu mali.
Waandishi kadhaa wa habari walishambuliwa na waandamanaji hao, hali iliyowalazimu polisi kuingilia kati kuwanusuru kutokana na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kuwatuhumu kuunga mkono ndoa hizo.
Polisi jijini Paris wanasema kuwa inawashikilia watu zaidi ya 293 ambapo watu sita ndio wanaoelezwa kujeruhiwa kutokana na maandamano hayo wakiwemo polisi wanne waliokuwa wakishiriki kwenye operesheni hiyo.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Manuel Valls amelaani maandamano hayo yaligeuka kuwa vurugu, na kuyashutumu makundi yenye msimamo mkali kuhusu ndoa za jinsia moja nchini humo.
Maandamano hayo yamefanyika wakati huu ambapo jopo la majaji wa tamasha la filamu la Cannes wakitoa tuzo ya filamu bora ya mwaka kwa mtunzi mwenye asili ya Tunisia na Ufaransa aliyetengeneza filamu inayoitwa :Blues is the Warmest Colour" ambayo inaelezea maisha ya wanawake waliooana.
Waandaji wa maandamano hayo wanasema kuwa zaidi ya watu milioni moja walijitokeza kwenye maandamano hayo kuoinga sheria hiyo inayoruhusu ndoa za watu wa jinsia moja.(RFI)

Subscribe to:
Posts (Atom)