Pages


Photobucket

Saturday, June 1, 2013

USHER AFUNGUKA KUHUSU MISUKUSUKO INAYOMWANDAMA JUSTIN BIEBER BIEBER

usher_grammy_engagement_rumou
Baada ya msanii Justin Bieber kuwa katika vichwa vya habari vya media mbalimbali kwa matukio ambayo si mazuri katika siku za karibuni, Msanii wa Muziki Usher Raymond ambaye pia ni kaka mlezi na kiongozi wake, ameongelea swala hili na kusema kuwa anaelewa misukosuko ya Bieber kutokana na ukweli kuwa kwa sasa yupo katika umri wa mambo mengi wa ujana.
Justin-Bieber-Won-Billboard-Music-Awards
Usher amesema kuwa, mtu yoyote angeweza kufanya kama Bieber ama hata zaidi katika umri kama ule na hatari zaidi, akiwa anafuatiliwa na mapaparazzi kwa karibu.
Bieber amekuwa mada ya majadiliano mbalimbali katika tasnia ya burudani hasa baada ya tukio la kuzomewa na mashabiki wakati akipokea tuzo za Billiboard, kulalamikiwa na majirani zake kwa uendeshaji mbovu wa magari na matukio mengine mengi yanayofanana na hili.

SIRI YA KUTEKWA ABSALOM KIBANDA YAANIKWA, ISOME HAPA

Timu ya kuchunguza tukio la kutekwa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda (pichani), imebaini kuwa kazi yake ya uandishi wa habari na siasa vimechangia kuvamiwa kwake na kuna kutupiana mpira kati ya vyombo vya dola na vyama vya siasa. Aidha, uchunguzi wa timu hiyo umebainisha kuwa baadhi ya watu waliohojiwa walidai kuwa utekaji wa Kibanda ulifanywa na vyombo vya dola ukiwa sehemu ya mpango mkakati wa vyombo hivyo kukihusisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vitendo vya ugaidi. 
Taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa tukio hilo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa timu hiyo, Deodatus Balile, iliyoundwa na TEF katika mkutano wa pili wa mwaka wa mashauriano kati ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) na jukwaa hilo jijini Tanga.
“Uchambuzi uliofanywa na timu hii umebaini kuwa hoja nne zinazungumzwa kuhusiana na kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda. Hoja hizi ni:- Kazi yake ya uandishi wa habari, Uhusiano wa kisiasa na vyama au wanasiasa mbalimbali, uhusiano wa kijamii ikiwamo mapenzi na vitendo vya rushwa,” ilieleza taarifa hiyo.
Alisema timu hiyo imejiridhisha kutokana na majibu ya wengi kuwa dhana ya mapenzi na rushwa, havina nafasi yoyote katika tukio hilo kwani waliohojiwa walieleza pasi na shaka kwamba kushambuliwa na kuumizwa Kibanda halina uhusiano wowote na rushwa au mapenzi.
Imeeleza kuwa kazi yake ya uandishi wa habari na siasa vikiunganishwa vimechangia kuvamiwa kwa Kibanda na kuna kutupiana mpira kati ya vyombo vya dola na vyama vya siasa.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa waliohojiwa waliyataja matukio ya uchaguzi Mdogo wa Igunga, maandamano ya Morogoro ya  Chadema na mkanda anaodaiwa kurekodiwa Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, kuwa vililenga kukifanya chama hicho kichukiwe na Watanzania kwa kukitaja kama chama cha kigaidi ambacho kinateka watu na kuwaumiza.
“Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anadai kwamba mpango kama huo vyombo vya dola viliutumia kwa NCCR Mageuzi vikakisambaratisha, Chama cha Wananchi (CUF) kilisingiziwa udini kikapoteza mwelekeo na sasa vyombo hivyo vililenga kukifanya Chadema kionekane cha kigaidi mbele ya macho ya jamii, ndiyo maana imerekodiwa mikanda kwa nia ya kuitumia kujenga hoja hiyo,” taarifa hiyo ilieleza.
Aidha, baadhi ya watu waliohojiwa walidai kuwa Chadema kimepewa mafunzo na ushauri kutoka nje ya nchi kuwa kikitumia baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola wasiokuwa waaminifu kuteka, kuumiza na hata kuua baadhi ya watu maarufu nchini wakiwamo waandishi na wanasiasa, hivyo wananchi wataamini kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kimeshindwa uongozi na sasa kimeanza kazi ya kuua wanaowapinga.
Imeeleza kuwa kwa njia hiyo, hesabu za Chadema ni kuwa wananchi wataichukia CCM na Serikali yake na kukipa nafasi ya kuingia madarakani na kauli ya Chadema kuwa nchi haitatawalika itakuwa imetimia.
Taarifa zaidi ya kamati hiyo imebainisha kuwa maisha ya wanahabari yapo hatarini kutokana na makundi mengi yenye maslahi kuwaona wanahabari wanaosimamia ukweli kuwa maadui wa maslahi yao haramu. 
“Kuna hatari kubwa inayowakabili waandishi wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015,” taarifa hiyo ilisema.
Uchunguzi umebaini kuwa usiri umepungua katika vyombo vya habari tofauti na zamani wakati ambao habari nyeti ziliandikwa kwa kuhifadhi majina ya waandishi wakitumia jina la Mwandishi wetu, lakini siku hizi hata habari za kutisha waandishi wanaweka majina yao na hata wasipoweka, ndani ya vyumba vya habari vingi waandishi wapo tayari kutaja nani ameandika habari fulani.
Uchunguzi huo pia umebaini kuwa usaliti miongoni mwa waandishi wenyewe ndani ya vyumba vya habari unazidi kuongezeka na usipodhibitiwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi. 
Taarifa hiyo inamnukuu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi akisema: “Hili ni jambo muhimu sana. Tuache usaliti vinginevyo wengi wataumia.”
Taarifa ya kamati hiyo inabainisha kuwa mazingira ya kazi ndani ya Kampuni za New Habari (2006) Limited na Freemedia Limited, yanaacha maswali kadhaa yenye kustahili majibu na ndani ya New Habari kumekuwapo na misuguano isiyo na afya kwa kazi ya Kibanda kama mwandishi na tasnia ya habari kwa ujumla.
“Mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd ni utata. Uhusiano katika chumba cha habari si mzuri. 
Ndani ya kampuni hawaaminiani na imefikia hatua wanatuhumiana kuwa huenda baadhi ya viongozi ndani ya New Habari wamehusika kumteka na kumuumiza Kibanda. Haya yameandikwa ndani ya mitandao ya kijamii, ikidai kwamba kiongozi mmoja ndani ya kampuni hiyo alihusika na utekaji wa Kibanda, uchunguzi huo umebainisha. 
Timu ya uchunguzi ilibaini kuwapo mgawanyiko mkubwa ndani ya New Habari (2006) Ltd kwa kuwapo kundi la ‘Habari Wazawa’ na ‘Habari wa Kuja’. Malalamiko mengi yanajikita katika msingi kuwa ajira hazitangazwi na watu wanaajiriwa bila kuzingatia sifa za kitaaluma.
“Kibanda hakuhama Free Media kwa amani. Uchunguzi unaonyesha kuwa miezi kadhaa kabla ya kuondoka kwake alianza kupoteza mamlaka. Mwenyekiti wa Kampuni ya Free Media Ltd, Freeman Mbowe, alianza kumsikiliza zaidi msaidizi wake ambaye alikuwa Naibu Mhariri Mtendaji, Ansbert Ngurumo kuliko yeye Kibanda.” 
Kibanda alitekwa usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, mwaka huu  na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake  eneo la Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo, Kibanda aliumizwa kwa kutobolewa  jicho la kushoto, akaumizwa kichwani kiasi cha kusababisha  kuvunjika kwa baadhi ya mifupa ya kichwa. 
Aidha watekaji walimng’oa meno mawili na kucha mbili, walimkata pingiri ya kidole cha pete chini ya kucha na kuondokana nayo.
Wakati timu hiyo iliyowashirikisha Balile, Pili Mtambalike , Jane Mihanji, Tumaini Mwailenge na Rashid Kejo ikiwasilisha taarifa yake, timu iliyoindwa na jeshi la Polisi kuchunguza tukio hilo hadi sasa haijafanya hivyo, badala yake imekuwa ikisisitiza kuwa uchunguzi unaendelea.
 
habari NA THOBIAS MWANAKATWE
CHANZO: NIPASHE

KUTOKA KUAJIRIWA MPAKA KUJIAJIRI: MAMBO 8 MUHIMU YA KUZINGATIA.

Kuna sababu mbalimbali kwanini mtu atake kuajiri, badala ya kuajiriwa, mfano kipato kidogo anachopata katika kazi husika, hitaji la kutaka uhuru zaidi binafsi wa kufanya kazi, hitaji la kuweza kutoa ajira kwa wengine na zaidi sana kuweza kutumia vema kipaji na uwezo wa kuzalisha ambao katika kazi ya sasa mtu hapati nafasi ya kufanya hivyo.  
Kujiajiri ni jambo linalohitaji maandalizi ya muda mrefu na kuna mambo ya msingi kuyafahamu, haiwezekani tuu , ukaacha kazi na kusema ok, acha nijiajiri.
Makala hii inachambua mambo ya msingi ya kujiandaa na kuyafahamu kabla mtu hajaamua kuacha kuajiriwa.
 
Mkakati ni muhimu: Wazo au ndoto isiyo na mkakati wa kuitimiza ni upuuzi yaani ndoto hiyo au wazo hilo halina maana, hivyo basi ndoto yako ya kujiajiri siku moja, ni lazima iwekewe mkakati wa kuifanikisha ikiwa ni pamoja na muda hasa wa lini utaitimiza hiyo ndoto. 
Katika kuweka mkakati huu wa kutimiza ndoto yako, fanya utafiti wa kina kuhusu mipango yako binafsi ya maisha, mtazamo wako kuhusu maisha, mpenzi/mke wako, familia yako, na hali ya jamii kwa ujumla inavyoenda kama vile mabadiliko ya hali ya kisiasa, teknolojia, na uchumi. 
Tengeneza malengo ya aina ya shughuli unayotaka kuifanya ukiacha kuajiriwa, na pima uwezekano wa shughuli hiyo kufanyika kweli na kama itakulipa. Utambue pia aina ya watu na rasilimali nyingine utakazozihitaji, na jinsi utakavyozipata.
Unahitaji fedha: Ndio, unahitaji kiasi cha fedha za kutosha kununua vifaa na malighafi za kutengenezea bidhaa yako. Pia unahitaji fedha za kuwalipa wafanyakazi wako, na zaidi sana , unahitaji fedha za kuendesha maisha yako na familia yako , kwa kipindi fulani kabla ya biashara kuanza kukulipa mshahara. Hivyo kabla haujaacha kibarua chako, hakikisha umetengeneza bajeti ya kutosha na una akiba ya kutimiza mahitaji ya bajeti yako. Usingependa uache kazi halafu uanze kuwa omba omba kwa rafiki na jamaa, au uanze kujuta.
Network ni muhimu: Kumbuka katika kujiajiri kwako, utahitaji wateja, washirika, wafanyakazi na hata washauri mbalimbali ili mambo yako yaende vizuri. Hivyo, wakati ukiwa umeajiriwa ndio wakati wako muafaka wa kutengeneza na kupanua wigo wako wa watu unaowafahamu na waliokaribu nawe.
Kumbuka kuendeleza mawasiliano kwani watu hawapendi kuona wewe unataka kuwatumia tuu kisha unawatupa. Endeleza mawasiliano walau hata kwa salamu tuu. Zaidi sana, heshimu watu wote, hata usiowafahamu au wale unaodhani 'sio watu muhimu'. 
Jenga taswira nzuri kwa jamii kwa lugha fasaha, picha na matukio mengine, usifanye watu wakufikirie vibaya.
Usipitwe na wakati: Hakikisha kuwa unafuatilia taarifa za matukio, dili na watu wanaohusiana na aina ya shughuli unayopanga kuifanya wakati utakapojiajiri. Hii itakusaidia kupata uzoefu na kusoma alama za nyakati, na pengine kutambua fursa nyingine zaidi. 
Endelea kujifunza zaidi kuhusu kazi yako, watu na jamii kwa ujumla kwani kujiajiri kunahitaji uzoefu zaidi, na zaidi sana uwezo wa kupambana na changamoto nyingi ambazo nyingine haujawahi kukutana nazo kabisa, ila taarifa za awali na kujua jinsi mambo yanavyoenda kwa ujumla katika jamii vitakufanya ushinde changamoto.
Maana halisi ya biashara: Baada ya kuacha kuajiriwa, hautarajii kuwa mtu wa ‘kuganga njaa’ yaani kufanya biashara ili mradi tuu hela iingie, lakini haujui mwelekeo wa biashara yako upoje, na wala hakuna mkakati wa kuikuza na kuimarisha biashara husika. 
Biashara inahusu kutimiza mahitaji ya watu, kwahiyo ili mradi utakuwa na uwezo mkubwa wa kutimiza mahitaji ya watu, na kuendelea kuhamasisha watu zaidi kuja kwako uweze kutimiza mahitaji yao , basi biashara itakua, na itaendelea kuwa endelevu. 
Kinyume cha hapo, ushindani utakutoa katika biashara kwani wateja watakambilia kwa wengine. Biashara sio tuu kupata wateja, ni vile kuweza kuendelea kupata wateja na kuendelea kupanua biashara. 
Inabidi uipende shughuli husika unayoifanya, na uweze kutimiza mahitaji ya wateja kupitia biashara husika. 
Muda wako mwingi utautumia katika shughuli yako mpya utakayojiajiri hivyo, kama ambavyo kazi uliyonayo pengine ‘inakuboa’, hakikisha ajira yako binafsi ‘haikuboi’.
Umuhimu wa wafanyakazi: Watendaji wa shughuli husika za biashara yako utakayoianzisha ni muhimu wawe wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha wa kufanya shughuli husika, na uweke mikakati ya kuwapatia nyenzo zote muhimu za kufanyia kazi ikiwemo teknolojia na mazingira mazuri ya kazi. Hivyo basi wakati unajiandaa kujiajiri tilia maanani hili katika bajeti yako ya kuajiri. Usingependa wafanyakazi wao wajisikie vibaya kama vile wewe ulivyojisikia vibaya katika ajira yako fulani (pengine ajira yako ya sasa). Muda huu ambao umeajiriwa, ndio muda pia muafaka wa kusaka 'vipaji'- yaani watu ambao utafanya nao kazi utakapojiajiri.
Inakuhusu wewe : Mafanikio yako katika kujiajiri yanategemea mambo mengi ila zaidi sana yanakutegemea wewe. Je, nini hasa sababu yako ya kutaka kujiajiri? 
Ni kweli una bidhaa au huduma haswa ya kupeleka sokoni itakayokufanya iendeshe maisha yako na kuiendeleza biashara husika au ni hasira tuu za jinsi bosi wako anavyokuchulia hapo ofisini kwako, au kwakuwa mshahara uliopo sasa haukutoshi. Je, mipango yako mingine ya maisha ipoje? 
Ndoto zako za kusoma, au kuishi sehemu tofauti tofauti, pengine mkoa mwingine tofauti na uliopo sasa, au pengine hata nchi husika. Je, yote hayo yanaathiri vipi mipango na mikakati yako ya kujiajiri, bila kusahau msukumo toka kwa familia yako.
Ndoto sahihi: Ni kweli kuwa upo sahihi kufikiria au kuota kufanya biashara kubwa na yenye mafanikio sana, lakini kumbuka mafanikio hayaji kwa usiku mmoja, na hata kama yatakuja kwa usiku mmoja, inahitajika kazi ya muda mrefu kuyafanya yawe endelevu. 
Hivyo basi, usingoje wakati ‘muafaka’ wa wewe kuwa na kiasi kikubwa cha fedha au kwamba ‘umeyaset’ vema mambo yote. 
Anza kidogo kidogo, kubali kufanya makosa, na tambua kuwa hata kama utafanya uchambuzi na uchunguzi wa kutosha kuhusu soko, jamii na teknolojia, hali halisi unayoenda kukumbana nayo inaweza kuwa tofauti na ile uliyojifunza wakati wa uchambuzi au uchunguzi wako kwakuwa hicho unachoenda kufanya ni kipya hakikufanyiwa uchambuzi, bali unakifanya kutokana na uchambuzi uliofanya hapo awali. 
Kuna mtu mwingine atakuja kutumia makosa au mafanikio yako kupanga mambo yake.

MTU MMOJA AFARIKI PAPOHAPO BAADA YA KUFARIKI AKIJARIBU KUDANDIA DALADALA LEO MAENEO YA ILALA BOMA, TAZAMA KILICHOJIRI HAPA

   

Asubuhi hii ajali mbaya imetokea maeneo ya Ilala Boma na  kusababisha kifo cha abiria huyu ambaye hajatambulika kwa jina mpaka sasa baada ya abiria kutaka kudandia bahati mbaya akadondoka na kupasuka kichwa na kusababisha umauti wake
Wasamaria wema wakisaidia kumpakia kwenye gari kwa kumpeleka hospitalini
                
Damu ya marehemu ambayo kwa kiasi kikubwa imetoka kichwani baada  ya kupasuka vibaya
Mwili wa marehemu ukiwa tayari kuondolewa kwenda hospitali
               
Hii ndio daladala ambayo marehemu alikuwa akitaka kudandia na kudondoka kwa bahati mbaya
Umati wa watu ukishuhudia ajali maeneo ya Ilala Boma asubuhi hii
                                   
Askari wa usalama barabarani akichukua maelezo kwa dereva aliyesababishaa ajali.



HII NDO ILE PICHA YA RAISI MUGABE ALIPONASWA WIKI ILIYOISHA KATIKA KIKAO CHA VIONGOZI WA AFRIKA. TAZAMA HAPA

african leader sleeping addis ababa
HII ILIKUA NI MJINI ADISABABA MAY 26 MWAKA HUU KATIKA KIKAO CHA VIONGOZI WA AFRIKA

HUU NDIO UKWELI KUHUSIANA NA MESSAGE ILIYOSAMBAA SANA KUA P FUNK NA MCHOMVU WALIPIGANA VIWANJA VYA LEADERS. SOMA HAPA

Leo jioni kuna msg zilikuwa zikitembea zikisema kuwa Prod Majani amepigana na mtangazaji kutoka Clouds FM anajulikana kwa jina la Adam Mchomvu maeneo ya Learders Club wakati sio kweli kabisa. P-Funk yeye alikuwa busy na kamati na hadi uvumi huo unatokea Adam alikuwa hayupo kwenye eneo la tukio kabisa. Adam yeye alitokea majira ya jioni na kushangaa story hizo, picha hiyo niliwapiga wakiwa pamoja ili kuwaambia watu kuwa huo uvumi ni kutaka kuleta mvurugano wakati huu tuliokuwa nao wakuondokewa na mwenzetu Albert Mangweha

DIAMOND AENDELEA KUWEKA WAZI MAISHA YAKE YA KIMAPENZI, HIKI NDO ALICHOKISEMA. SOMA HAPA

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
DIAMOND ANAFAFANUA

“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.

“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”

JACQUELINE WOLPER

Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.

PENNY SASA

Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.

“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu, hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”Chanzo:www.globalpublishers.info