Pages


Photobucket

Monday, February 4, 2013

Mbunge wa Arusha Mjini Lema-CHADEMA amekabidhiwa Kiwanja cha kujenga hospitali ya Mama na Mtoto


CHADEMA ikiongozwa na kamanda Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa wamekabidhiwa kiwanja cha ekari 3 cha kujenga hospitali ya Mama na Mtoto. 

Hii ni utekelezaji wa ahadi aliyowa kuwaahidi wananchi wa Arusha katika uchaguzi wa 2010. Kiwanja hicho chenye thamani ya dolla za kimarekanai USD300,000 sawa na Tsh 480,000,000/ kimekabidhiwa na kampuni ya Mawala Advocates waliowakilishwa na moja ya mawakili na wakurugenzi wa kampuni hiyo.


KUTOKA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akichangia hoja katika Bunge- Dodoma. Mussa Zungu Azzan (ILALA) na Mbunge wa Mafia Abdulkarim Shah (kulia) wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Bunge Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbene (kulia), Mwingulu Nchemba (katikati) , na Vick Kamata (Viti Maalumu ) kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja Bungeni – Dodoma. Mbunge wa Peramiho Jenista Mhagama akichangia na kuunga mkono hoja ya Mbunge wa Nzega Dkt,Hamis Kigwangala ya kuita Serikali ianzishe mpango maalumu wa kukuza ajira kwa vijana kwa kuanzisha Mfuko wa Mikopo ya Vijana wanaowekeza kwenye kilimo na viwanda venye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo. PICHA ZOTE NA MWANAKOMBO JUMAA- MAELEZO.

KUTOKA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA

 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akichangia hoja katika Bunge- Dodoma.
 Mussa Zungu Azzan (ILALA) na  Mbunge wa Mafia Abdulkarim Shah (kulia)  wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Bunge Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbene (kulia), Mwingulu Nchemba (katikati) , na Vick Kamata (Viti Maalumu ) kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja  Bungeni – Dodoma.
Mbunge wa Peramiho Jenista Mhagama akichangia na kuunga mkono hoja  ya Mbunge wa  Nzega  Dkt,Hamis Kigwangala ya kuita Serikali ianzishe mpango maalumu wa kukuza ajira kwa vijana kwa kuanzisha Mfuko wa Mikopo ya Vijana wanaowekeza kwenye kilimo na viwanda venye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo. PICHA ZOTE NA MWANAKOMBO JUMAA- MAELEZO.

TASWIRA YA SHEREHE ZA MIAKA 36 YA CCM, ZILIZOFANYIKA JANA MKOANI KIGOMA,


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Uwanja wa Lake Tangayika kuongoza wananchi katika kilele cha sherehe za miaka 36 ya CCM, leo,
Wananchi wakichangamkia kumsalimia Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipowasili Uwanja wa Lake Tanganyika leo kwenye sherehe hizo
Wananachi wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akipoingia uwanjani kwenye sherehe hizo
Rais Kikwete akitazama ngoma ya Warundi waliokuwa wakitumbuiza wakati wa sherehe hizo. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kianana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba.
Mtoto ambaye ni msanii kutoka kundi hilo la Warundi akimkubatia Nape, alipokuwa akishuhudia ngoma yao
Vijana wa CCM wakipita kwa Ukamavu mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa gwaride maalum la vijana hao la maadhimisho ya sherehe hizo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa amesimama kupokea heshima wakati gwaride maalum la Vijana wa CCM, wakati wa sherehe hizo. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Phili Mangula, na kulia ni Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha wananchi kuchangamsha sherehe hizo
 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye sherehe hizo, huku Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfuatilia kwa makini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kwenye mkutano huo. Kushoto ni Nape
 Wananchi wakiwa wamefurika Uwanjani wakati wa sherehe hizo, kiasi cha baadhi kualazimika kushika viatu mkononi kama huyu anayeshangilia
Diamond akitumbuiza kwenye sherehe hizo.
Msongamano mkubwa uwanjani kutokana na maelfu waliohudhuria sherehe hizo
Waalikwa kutoka Chama tawala cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa na bendera yao kwenye sherehe hizo
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye sherehe hizo
Kikwete akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye sherehe hizo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akitazama ndizi zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda la Wakulima wa Kasulu mkoani Kigoma nye ya Uwanja wa Lake Tanganyika
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akitazama moja ya moja zilizovuta kumbukumbu zake, kwenye banda ya  Uhuru Publications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Chama ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, kwenye banda la kampuni hiyo, nje ya Uwanja wa Lake Tanganyika. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Kulia ni Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Josiah Mufungo
 Hali iliyokuwa ikionekana nye ya Uwanja wa Lake Tanganyika wakati wa sherehe hizo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Masika” Bungeni, ikiendelea waanze kutekeleza ‘Kilimo Kwanza’ mumo humo ndani

Picture


BAADHI ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanaoendelea na kikao cha 10, wameulalamikia uongozi wa Bunge kwa kutojali kufanya marekebisho ya jengo la Bunge wakidai kuwa linavuja kwa muda mrefu sasa.

Malalamiko ya wabunge hao yalifikishwa kwa Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai jana, ambapo walisema kwamba wana wasiwasi na usalama wa jengo hilo.

Ubovu huo ulibainika siku ya  Ijumaa iliyopita  baada ya mvua kuanza kunyesha usiku saa saba na kuendelea hadi mchana katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma. Mbali na eneo linalokaliwa na wabunge kuvuja, maeneo mbalimbali ya jengo la bunge yalikuwa yanavuja.
Taarifa mheshimiwa Naibu Spika, hili jengo linavuja, kwa kweli hata hapa nilipokaa ndiyo hasa maji yanapita... sasa tuhakikishiwe usalama wetu Naibu Spika (alisema Mchungaji Peter Msigwa).

Taarifa zimefika kwa sasa wataalamu wetu wa maeneo mbalimbali ya jengo wanafanya kazi kuhakikisha wanarekebisha hali hiyo. (alisema Ndugai alipopokea taarifa hiyo).
Jengo la Bunge mjini Dodoma lililojengwa kisasa zaidi kwa ushirikiano kati ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa gharama ya zaidi ya Sh29.8 bilioni kwa sasa lina uwezo wa kubeba wabunge 350 kwa pamoja, wageni maalumu zaidi ya 100 na wananchi wasikilizaji 200.

Ukumbi huo wa kisasa umekuwa mfano wa kuigwa ambapo wawakilishi wa mabunge kadhaa kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao wamekuwa wakifika mjini Dodoma wamekuwa wakiuchukulia kama mfano.

---
via gazeti la Mwananchi

UNESCO yaanza harakati za ukarabati na uhifadhi wa maeneo ya urithi wa kiasili Mali


Mkurungenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova na
Rais wa Ufaransa François Hollande wakipatiwa maelezo
katika moja ya maeneo waliyotembelea
"Tunataka hatua za haraka za kulinda na kujenga upya maeneo ya kipekee ya urithi wa kiutamaduni nchini Mali".
Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Matiaifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, aliyoitoa Jumamosi baada ya kuwasili nchini Mali, ikiwa ni sehemu ya harakati za shirika hilo za kusaidia ulinzi na kukarabati maeneo hayo yaliyoharibiwa kutokana na mapigano yaliyoanzia maeneo ya kaskazini.
Bi. Bokova ambaye anatembelea Mali akiwa ameambatana na Rais François Hollande wa Ufaransa, amekaririwa akisema kuwa uhifadhi na ukarabati wa maeneo hayo ya urithi wa kiutamaduni pamoja na nyaraka mbali mbali za kiasili ni hatua muhimu kwa umoja wa kitaifa na maridhiano wakati huu ambapo wananchi wa Mali wanaimarisha misingi ya amani ya nchi yao.
Mkuu huyo wa UNESCO anatarajiwa kuainisha mpango wa utekelezaji wa harakati hizo za ukarabati wa maeneo ya urithi wa kiutamaduni kwa kushirikiana na serikali ya Mali ambapo UNESCO itasaidia ukarabati na uhifadhi.
Atakuwa na mazungumzo na viongozi wa mamlaka mbali mbali kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako na mji wa Timbuktu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mpango huo.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU

IMG-20130204-00692 1f86d

IMG-20130204-00693 411a4
IMG-20130204-00695 ad6ddIMG-20130204-00697 9f105

IMG-20130204-00698 e2339
IMG-20130204-00699 05088

IMG-20130204-00700 de2a6IMG-20130204-00701 65388IMG-20130204-00702 85db3
IMG-20130204-00703 a8aefIMG-20130204-00704 49f35

IMG-20130204-00705 64de1
IMG-20130204-00707 57f22
IMG-20130204-00708 0e2a6
IMG-20130204-00709 2d428

Sunday, February 3, 2013

Rais Kikwete aongoza Matembezi ya Mshikamano ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM mkoani Kigoma leo


 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM},Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete leo wameongoza Matembezi ya Mshikamano yaliyoanzia kwenye eneo la Mnarani na kuishia kwenye ofisi za CCM mkoani Kigoma,asubuhi ya leo. Matembezi hayo hayo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM},Rais Jakaya Kikwete akionekana kuwapungia wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliokuwa wamejipanga kwa wingi pembezoni kwa barabara Lumumba/Ujiji asubuhi ya leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM},Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi hayo.
Maandamano yakiendelea