Pages


Photobucket

Saturday, May 4, 2013

NAMSHANGAA DIAMOND MIMBA IPI KWANZA...HII NI KAULI YA VJ PENNY... SOMA HAPA STORY NZIMA




Mwanamziki anayefanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ siku za nyuma alitoa kauli ya kuwa mchumba wake ambaye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ ana ujauzito wake na kwamba amemnunulia ‘mkoko’ (gari) la mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kwenda nalo kliniki kama utakuwa mfutaliaji mzuri wa story zetu basi utakuwa umeshaisoma hii sasa Penny ameifungukia kauli hiy
Baada ya penny kulizwa juu ya ujazito wa Mwanamziki Diamond alioneka kushangzwa sana na kauli hiyo na kupaniki ghafla
Alisema amekuwa akisoma habari za ‘mimba’ yake kupitia magazeti lakini hajawah kuulizwa na mwandishi yeyote, jambo linalomshangaza sana.
Na hivi ndivyo ilivyo kuwa katika maongezi na mwandish kutoka GPL
Penny alisema: Namshangaa! Ni mimba ipi kwanza?uhusiano wangu na Diamond unaninyima raha kutokana na maneno ya watu.
Penny: Mh! Yaani sijui hata niseme nini, nashangazwa sana na hizi habari, nazisikia tu halafu mimi mwenyewe mhusika sijapewa nafasi ya kuzungumza.
Unajua sijazoea maisha haya ya kila wakati kuzungumza na waandishi. Naomba mniache, nani aliwaambia kuwa mimi nina mimba?
Funguka: Diamond.
Penny: Kama ni Diamond muulizeni yeye mwenyewe! Mbona nakosa raha jamani?
Funguka: Vipi mna mpango wa kuoana na Diamond?
Penny: (kwa hasira) Hizo ni ishu zangu binafsi, kama tutaoana au hatuoani ni mipango yetu, sioni sababu ya kutangaza kwenye media.
Funguka: Unaichukuliaje kauli ya mama mkwe wako, yaani mama Diamond? Inadaiwa alisema hatambui uhusiano wowote wa mtoto wake na mwanamke mwingine hadi atakapofunga ndoa.
Penny: Tafadhali sana, sitaki kuzungumzia habari kuhusu mama Diamond. Kwa hilo ‘no comment.’
Funguka: Vipi lakini, unainjoi kuwa na uhusiano na Diamond?
Penny: (Akakata simu).
Funguka: Haloo… haloo!
Hata hivyo mapaparazi wetu walipojaribu kumpigia simu tena hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu mpaka kukatika yenyewe.

Pinda's exams probe team finds 'scapegoat'


  Government rushes to nullify National Form Four results
NECTA's Executive Secretary, Dr Joyce Ndalichako (Left) and Prime Minister Mizengo Pinda (Right)
Faced with criticism and pressure from Parliament, the general public as well as a section of education experts, the government yesterday announced ‘a scapegoat’ that it believes was behind the mass failure recorded during the National Form Four examination of 2012.

The scapegoat is the National Examinations Council of Tanzania (NECTA), the body that has supervised and managed all examinations in Tanzania for decades, which the committee formed by Prime Minister Mizengo Pinda established that it used a new grading system that caused mass failures.

To repair the damage, the government has yesterday nullified the National Form Four results for all students who sat for the examination. But judging the reality on some of the examination’s answer sheets displayed by NECTA to the media early this year on which, one student drew a cartoon showing Barcelona’s star player Lionel Messi dribbling the ball, there might be more than just the offending ‘grading system’ factor.

Announcing the government decision yesterday in Parliament Minister of State in the Prime Minister’s Office (Policy, Coordination and Parliamentary Affairs) William Lukuvi said the committee formed by the prime minister to investigate the reasons behind such massive failure learnt that NECTA used a new system called Fixed Grade Ranges (FGR) in grading students’ performance.

The government announcement came only four days after the inquiry committee led by Prof Sifuni Mchome tabled its preliminary report of findings to the cabinet in Dodoma. It was on April 29th last week that the committee met the cabinet in Dodoma to table its preliminary findings. Lukuvi said the new system used by NECTA to grade the Form IV results last year was different from the traditional system used in previous years called National Mean Difference ( NMD).

According to Lukuvi, the NMD also took on board the respective student’s average Continuous Assessment (CA) for each subject. Lukuvi gave no more details with regard to the new system (FGR) in grading students’ performance last year besides maintaining that such a system was not thoroughly researched and prepared before its application by NECTA.

Lukuvi said after the meeting with the committee the cabinet agreed unanimously that the 2012 Form IV results be nullified, aaccording to advice from the inquiry task force. The minister said the results would now be standardized so that the pass marks could tally with efforts that students used while studying. The cabinet also agreed that NECTA should suspend application of the new grading system (Fixed Grade Ranges) and should instead apply the old system in grading the 2012 Form results (National Mean Difference).

The traditional grading system, according to Lukuvi, should also be used in grading Form Six National Examination results. He called upon NECTA to involve educational stakeholders when making changes on the grading system.

“The decision by the cabinet is aimed at doing justice to parents, students and teachers who have spent time, effort and other resources to ensure they fulfilled their desired educational objectives,” Lukuvi said. However, he said a drastic increase in number of students and pupils in schools across the country had since overwhelmed the government’s ability to provide all educational requirements, affecting the quality of education and students’ performance.

Giving statistics, Lukuvi said from 1961 to 2001 the number of primary school pupils increased from 486,470 to 4,875,764; but for the period between 2001 and 2012 the number of primary school pupils increased from 4,875,764 to 8,247,472. Secondary school students also increased from 11,832 during independence (1961) to 289,699 in 2001 but the country experienced a drastic increase from 289,699 students in 2001 to 1,884,270 in 2012.

Lukuvi attributed such a drastic increase of pupils and students in schools to various educational programmes implemented by the government such as Primary Educational Development Programme (PEDP) and Secondary Educational Development Programme (SEDP). On February 18, this year the government announced the Form IV national examination results, indicating that over 60 per cent (240,000) of the 367,756 candidates who sat for the examination on October last year had completely failed. According to the breakdown provided, only 23, 52 students scored Divisions One to Three, while 103,327 candidates scored Division Four.

Though the committee has initially come up with such findings and recommendations, educational policy in the country needs to be reviewed. This will necessitate an overhaul of the education curriculum.

The committee cites other factors that contributed to poor performance as lack of proficiency in English language which is the medium of instruction, poor motivation to teachers, ill-training of teachers and lack of learning and teaching material.
 

MAJAMBAZI MATANO YAUAWA NA POLISI JIJINI MBEYA LEO MCHANA .Tazama PICHA



Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha



Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo
Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.




MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa  baada ya watu watano wanaodhahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu. Alisema baada  ya  Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG aina ya Toyota Spacio.....Baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo  ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
 Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya. Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana mara moja ambapo miili  yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
 Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.

Azam ready for FAR challenge






Tanzania's sole representatives in 2013 continental tournaments, Azam FC, will be subjected to maximum test when they face Moroccan side FAR Rabat today but coach Stewart John Hall says his team is ready for the challenge.

"It is a good side. I have watched them five times, three times on DVDs and two times live, thus we have clear idea on how they play," he said.

He affirmed that in those five games they have used 14 players and they have scored three goals and conceded one goal. “This is a clear indication that they almost keep the same squad, they don't score many goals and they don't concede many either."

Hall says he understands that his opponents will be tactically disciplined, a factor that necessitates Azam FC to play with their heads. "We have to be disciplined too.

I believe in our pace; we can upset them on the counter attack," noted the Briton.
He observed further that Azam FC have a tactical plan and have a clear idea on how FAR Rabat play, and the work ahead is to put the two things together to win the game.
Following a scoreless draw in Dar es Salaam a fortnight ago, Azam need a victory or a score draw to advance to the third round of the Confederation Cup.

Asked on the Azam's best away performance compared to home, the tactician said in away games teams play open games, making it easier for Azam to play.

"In Juba when we were leading 3-1 from the first leg, Al Nasri wanted to beat us in the early stages of the second leg. As a result we won 5-0.

“Likewise in Monrovia, BYC II tried to do the same but the game went on our side as we eventually won 2-1,” he asserted.
The coach has confirmed that he will make only one change by bringing in Ugandan import Brian Umony who will be operating on the right flank, replacing Mcha Khamis for the purpose of attacking with pace.

Mwadini Ali will maintain his position as goalkeeper, assisted by Himid Mao and Waziri Salum on the right and left back, respectively.

The center backs are David Mwantika and Jockins Atudo. The midfield will be commanded by Michael Bolou, shouldered by Salum Abubakar and Humphrey Mieno.

Umony wil lead the attack from the right flank as attacks from the left flank will be entrusted to Kipre Tchetche, as captain John Bocco will play as leading striker.

Azam FC have been in Rabat for most of the week. The match will be officiated by Algerian referee Abib Medh.

YALIYOMPATA RICK ROSS, SASA YAMPATA LIL WAYNE. MKATABA WAKE NA MOUNTAIN DEW WAPIGWA CHINI

Baada ya Rick Ross kupigwa chini na Reebook, sasa ni zamu ya Tunechi. Lil’ Wayne amepoteza mchongo wake kama msemaji wa kinywaji cha Mountain Dew kufuatia mashairi kwenye wimbo wake Karate Chop.
lilwayne_emmett_till
Lil’ Wayne ambaye amekuwa akitumiwa kwenye matangazo ya Mountain Dew tangu mwaka 2012, ameikasirisha familia ya Emmitt Till kwenye wimbo “Karate Chop” ambapo Weezy anasikika akisema, “Pop a lot of pain pills, ’bout to put rims on my skateboard wheels … beat that p***y up like Emmett Till.”
Emmett Louis Till alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyeuawa huko Mississippi mwaka 1955 akiwa na miaka 14 baada ya kumtongoza msichana wa kizungu.
Licha ya kutuma barua ya kuomba radhi kwenye familia hiyo, ilikataliwa na ndugu zake pamoja umma kumkosoa vikali Lil Wayne.
Japo kampuni ya Pepsi haijatoa maelezo zaidi, hatua hiyo ilitangazwa na msemaji wa Lil Wayne Sarah Cunningham, aliyesema kuwa ni kutokana na kupishana kiubunifu.

JK AWAOMBA WAMILIKI WA SHULE BINAFSI KUPUNGUZA ADA ZAO, JE HII ITAWEZEKANA ? SOMA HAPA


SHULE zinazoendeshwa na kumilikiwa na tabinafsi, zimetakiwa kurekebisha ada zao ili Serikali iangalie uwezekano wa kushirikiana nazo katika kulipia. Ushauri huo umetolewa na Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Chama cha Wamiliki wa Vyuo na Shule Binafsi (TAMONGSCO) uliofanyika hivi karibuni katika ukukbi wa Mkapa mjini Mbeya.asisi na watu

Hatua hiyo ilitokana na mapendekezo ya Tamongsco yakitaka Serikali ipeleke wanafunzi kwao na kuwalipia ada, kupitia mfumo wa ushirikiano wa Sekta Binafsi na ya Umma (PPP).
Katika mapendekezo yao, walitaka Serikali ipunguze msongamano wa wanafunzi waliozidi katika shule zake, kwa kuwapeleka katika shule binafsi. Akijibu hoja hizo, Rais Kikwete, aliyealikwa kuhudhuria, alisema wazo hilo ni zuri lakini lina changamoto.
“Nimesikiliza kwa makini sana hoja yenu ya kutaka kushirikiana na Serikali kuondokana na msongamano wa wanafunzi katika baadhi ya shule zake. “Natambua kwamba wakati Serikali inahangaika kupunguza msongamano kwenye shule zake, baadhi ya shule zenu zina madarasa yaliyo wazi na zingependa kuletewa wanafunzi na Serikali,” alisema Rais.
Rais alifafanua kwamba pamoja na uzuri wa wazo hilo, suala hilo lina changamoto zake kutokana na ukweli kwamba gharama katika shule hizo ni kubwa, hivyo wazazi au Serikali hawataweza kumudu. Ombi la JK Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete katika mkutano huo wenye kaulimbiu ya ‘Changamoto na fursa zilizopo katika ushirikiano baina ya sekta ya umma na isiyo ya umma katika utoaji wa elimu bora’, alitaka walimu hao kujadili tatizo hilo la ada kubwa.
“Nina ombi moja kwenu ambalo napenda mlijadili kwenye mkutano wenu. Ombi lenyewe si geni, linahusu ada kubwa zinazotozwa na shule au vyuo vyenu. Wapo wananchi wengi ambao wangependa sana kunufaika na elimu nzuri mnayoitoa, lakini wanashindwa kutokana na ada inayotozwa kuwa kubwa.
“Sisemi ada zenu zifanane na za shule za Serikali, lakini baadhi ya shule na vyuo vyenu vinalalamikiwa na wananchi kwa kutoza ada kubwa na kwamba hazitabiriki kwani hupandishwa wakati wowote,” alisema Rais Kikwete.
Tathmini Pamoja na ombi hilo kwa Tamongsco, Rais Kikwete alisema Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imeliona hilo na imeamua kulifanyia kazi. Alisema tathmini ya gharama halisi za uendeshaji kwa mwanafunzi mmoja, itafanywa ili kutoa ushauri stahiki kwa wamiliki wote wa shule au vyuo kuhusu kiwango cha ada.
Alirejea kauli yake, kwamba elimu ni huduma muhimu na haki kwa mtoto na si vema kugeuzwa kuwa biashara ya kuleta faida kubwa. Alisema hadi sasa uthamini kwa vyuo vya elimu ya juu umeshafanyika na mapendekezo ya gharama halisi yameandaliwa.
Rais alisema tayari hatua za kumpata mtaalamu elekezi zimefanyika, kwa ajili ya kutathmini gharama za uendeshaji kwa shule za sekondari. Hata hivyo, aliwahakikishia Tamongsco kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nao, ili kuwawezesha vijana wengi zaidi wa kitanzania kupata elimu.
“Tutaendelea kupokea na kufanyia kazi ushauri wenu ili kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya elimu.”
Sera ya Elimu Wakati huo huo, Serikali imesema Sera mpya ya Elimu inatarajia kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka huu ambapo pia mitaala ya elimu itapitiwa upya, ili kwenda sambamba na sera hiyo.
Rais Kikwete alisema mchakato wa kutunga sera hiyo mpya ya elimu baada ya ile ya mwaka 1995, umefikia hatua za mwisho na kinachosubiriwa sasa ni maoni ya wabunge ili sera ikamilishwe.
“Naamini kabla ya mwisho wa mwaka huu, sera itakuwa tayari kutumika, tunaamini kuwa sera hiyo mpya italeta mabadiliko katika uendeshaji wa mifumo yetu ya elimu nchini, na kutoa majibu kwa maswali mengi,” alisema.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, nafasi ya sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya elimu nchini itafafanuliwa kwa upana na kina zaidi.
Alifafanua, kwamba mitaala mipya itakayotokana na sera hiyo, itakwenda sambamba na hali ya sasa na mahitaji ya maendeleo nchini na duniani, huku akiwahakikishia kuwepo kwa ushirikishaji wa wadau, wakiwamo wa sekta binafsi katika suala hilo. Idara ya Elimu Kuhusu Idara ya Ukaguzi wa Elimu, Rais alisema itapewa kipaumbele na Serikali inatambua kuwa hali ilivyo sasa hairidhishi.
“Serikali imeanza na inaendelea kuchukua hatua thabiti kuimarisha ukaguzi wa shule na vyuo nchini, miongoni mwa mambo yanayofikiriwa kufanywa ni kubadili Idara ya Ukaguzi kuwa taasisi inayojitegemea na kuiwezesha kwa rasilimaliwatu, vitendea kazi na fedha,” alisema
Alisema anaamini kwa njia hiyo, wataimarisha utendaji wa ukaguzi na matokeo yake yataonekana kwa muda mfupi na kuwakumbusha kuwa mkaguzi wa kwanza wa shule ni Mkuu wa Shule.

MWANAFUNZI WA CHUO CHA IFM - DAR AFARIKI DUNIA KWA KULISHWA SUMU NA MKE WA MTU , SOMA KISA HAPA

Habari zilizotufikia toka IFM- Dar es salaam ni kwamba mwanafunzi mmoja ambaye bado hatujafanikiwa kulipata jina lake amefariki dunia kwa kulishwa sumu katika chakula alicholetewa na mpenzi wake ambaye ni mke wa mtu...... Taarifa zaidi zinadai kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa na uhusiano wa karibu sana na mke wa mtu ambaye mbali na starehe za kimapenzi alikuwa pia anampekea chakula cha jioni Baada ya mchezo huo kudumu kwa muda, mume wa mwanamke aliusoma mchezo mzima na kuandaa tego la kuwaangamiza wote.... Habari zinadai kwamba Siku ya jumatano jioni mwanaume huyo aliwahi kurudi nyumbani na kufanikiwa kukinasa chakula kilichokuwa kimeandaliwa tayari kwa kupelekwa kwa huyo mwanafunzi ambaye alikuwa anatembea na mke wake..... Baada ya kukinasa, alijifanya kuzuga na kupotezea...Mkewe alipotoka alikichukua na kukitia sumu chakula hicho na kisha kukiweka kama kilivyokuwa kimeandaliwa.... Lengo lake lilikuwa ni kuwamaliza wote maana alijua ni lazima akifika watakaa na kula pamoja..... Mwanamke alipopeleka chakula hakukaa kula na badala yake alimwambia yule mwanafunzi kuwa mume wake amewahi kurudi siku hiyo hivyo hatoweza kukaa wale pamoja....Mwanafunzi huyo akakipokea na kukila na ndipo mauti yakamkuta Habari toka chuoni hapo zinadai kwamba mwanafunzi huyo alikuwa ameshadisco lakini alikuwa amepewa nafasi nyingine ya kurudia mwaka wa pili , hivyo aliendelea kukaa mtaani kama mwanafunzi.... Mwili wa marehemu bado uko Muhimbili kwa uchunguzi zaidi baada ya polisi kuuzuia kuzikwa.... Hizi ni habari mbaya sana kwa wanafunzi wa chuo hicho maana ni jumatatu tu mwanafunzi mwingine alifariki katika hali ya kutatanisha baada ya kifo cha mpenzi wake miezi michache iliyopita.... Habari za ndani zaidi zinadai kuwa toka mwaka huu uanze mpaka sasa chuo cha IFM kimepoteza wanafunzi 12 huku wawili wakiripotiwa kuwa na hali mbaya zaidi katika hospitali ya Muhimbili....