Pages


Photobucket

Friday, February 1, 2013

NAPE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ILAGALA KIGOMA

 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akiangalia matunda ya Mchikichi ambayo yanachemshwa katika mapipa kwaajili ya kukamua mafuta ya mawese katika Kijiji cha Ilagala, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
 Wana CCM wa Igalula wakiwa katika kikao cha ndani na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akikagua maendeleo ya ujenzi katika Kituo cha afya Ilagala.
 Nyumba ya Daktari wa Ilagala
 
Wakazi wa Ilagala wakimsikilaza Nape Nnauye
 Nape akihutubia wakazi wa Ilagala ambao walitoa kilio chao kuwa ni mgogoro wa ardhi baina ya Kijiji na Magereza .

SAKATA LA GESI MTWARA: Mbowe ambana Pinda


Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mwenyekiti  wa
CHADEMA Freeman Mboe
KIONGOZI wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amembana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitaka serikali iwachukulie hatua watendaji waliozembea kudhibiti vurugu za mzozo wa gesi Mtwara.

Mbowe pia alimhenyesha Pinda akimtaka alihakikishie Bunge ni lini serikali itakuwa tayari kuweka wazi mikataba kadhaa ikiwamo ya mafuta na gesi asili ili kuondoa upotoshaji wa miradi hiyo kama ilivyotokea Mtwara.
Akiuliza swali hilo bungeni jana mjini hapa, Mbowe alisema kwa kuwa vurugu hizo zimetokana na uzembe wa kisiasa na viongozi wakiwamo wa vyombo vya dola kushindwa kubaini na kudhibiti ghasia hizo mapema, kwanini wasichukuliwe hatua kwa uzembe huo.
Akijibu maswali hayo, Pinda alirejea kauli yake ya mara kwa mara tangu alipotoka kusuluhisha mzozo huo Mtwara, akisema vyama vya siasa vimechangia sana kukuza na kupotosha ukweli wa mradi huo.
Alisema wanasiasa walitumia mzozo huo kujiimarisha kisiasa na kujijenga kwa ajili ya uchaguzi unaokuja. "Suala la kuwawajibisha watendaji hao liko chini ya waziri mkuu na rais, tutaliangalia,” alisema Pinda.
Hata hivyo, Pinda alisema jambo la msingi si kutafuta mchawi, kwani tatizo la Mtwara ni la wote, na siku zijazo kutakuwa na ushirikishwaji wa jamii katika kutoa elimu ili kuepuka madhara kama yaliyotokea Mtwara.

Kuhusu kuweka wazi mikataba ili kuondoa upotoshaji, Pinda alisema mikataba hiyo haina siri na inaweza kuwekwa wazi kupitia mifumo ya kibunge.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hakuridhika na majibu hayo na katika maswali yake ya nyongeza alimtaka waziri mkuu kutamka wazi bila kumng’unya maneno kama serikali iko tayari kuweka mikataba hiyo wazi.
Pia alihoji ni kwa nini serikali iko tayari kutekeleza kero za wananchi pale inapobanwa kwa presha na maandamano kama ilivyotokea Mtwara.
Katika hoja hiyo, Pinda alisema serikali haiko tayari kuweka wazi mikataba hiyo kupitia magazeti, kwani mingine ina taratibu zake lakini iko tayari kuweka wazi kupitia mifumo ya kibunge.
Kuhusu serikali kusikiliza kero za wananchi baada ya presha za maandamano, Pinda alisema maandamano si njia sahihi ya kuwasilisha madai ya wananchi.
"Ndugu yangu Mbowe anajaribu kuleta hoja ambayo haina mashiko. Mimi siamini kuwa maandamano ndiyo njia sahihi ya kuwasilisha malalamiko ya wananchi,” alisema Pinda.
Mapema kabla ya maswali kwake, Pinda alitoa taarifa ya kueleza kuhusu vurugu za Mtwara pamoja na madhara yaliyojitokeza, ambapo hata hivyo alirudia kile alichowaeleza waandishi wa habari juzi.
Alisema kulikuwa na upotoshaji mkubwa kwamba bomba hilo la gesi lingeishia Bagamoyo ambako inajengwa bandari ya kusafirishia gesi hiyo nje na kumhusisha Rais Jakaya Kikwete, jambo ambalo si la kweli kabisa.
Waziri Mkuu Pinda aliwatangazia wabunge uharibifu wa mali na hasara iliyopatikana kutokana na vurugu hizo, sambamba na kuorodhesha majina ya watu waliochomewa nyumba, magari na mali nyingine.
Pia alitaja majengo na ofisi za serikali zilizochomwa moto pamoja na magari, ambapo uharibifu huo umesababisha hasara ya mabilioni ya fedha, akisema serikali itaangalia namna ya kuwafidia.
Mbunge amwaga machozi
Wakati akitaja majina ya watu waliochomewa nyumba na mali zao, Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kasembe, alitokwa machozi ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Hali hiyo ilifanya baadhi ya wabunge wanaokaa jirani naye kumtoa nje ya ukumbi na kumbembeleza huku wakimpa pole.
Mbunge huyo ni mmoja wa wabunge waliochomewa nyumba, magari na mali nyingine.
Wengine ni Anna Abdallah na Hawa Ghasia, ambao nyumba zao ziliteketezwa kabisa.
Tume ya Spika yayeyuka
Spika wa Bunge, Anne Makinda, ametengua uamuzi wake wa kutaka kuunda kamati ya Bunge kwa ajili ya kuchunguza sakata la vurugu za Mtwara.
Akitangaza uamuzi huo jana, Makinda alisema baada ya taarifa ya waziri mkuu kuhusu mzozo huo, hakuna haja ya kuunda tume hiyo.
"Kwa vile taarifa ya serikali imejitosheleza, Bunge hatuna sababu tena ya kuunda tume. Nampongeza waziri mkuu kwa kazi aliyoifanya na niwapongeze wananchi wa Mtwara kwa kuelewa na kudumisha amani,” alisema.
Mnyika awapinga
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amesema hajaridhika na taarifa ya waziri mkuu pamoja na uamuzi wa Spika kuhusu mgogoro wa gesi mkoani Mtwara.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alisema kuwa taarifa zinadhihirisha kwamba nchi imefika hali hiyo kutokana na udhaifu wa serikali na ombwe la kiuongozi na kiusimamizi ikiwamo wa kibunge.
Alisema kuwa taarifa ya waziri mkuu ilijibu baadhi tu ya madai ya wananchi lakini pia imefafanua sehemu ndogo ya masuala ambayo aliyahoji bungeni Julai 27, mwaka jana, lakini serikali ikakwepa kutoa ufafanuzi.
“Taarifa hiyo itawezesha kutuliza mgogoro kwa muda lakini haijengi msingi wa ufumbuzi endelevu. Sikubaliani na uamuzi wa spika wa kubadili uamuzi wake wa awali alioutangaza wa kuunda kamati kufuatia maelezo ya waziri mkuu yasiyokuwa na vielelezo vyovyote, kwa kuwa kufanya hivyo ni kulinyima Bunge fursa ya kuisimamia serikali ambayo ndiyo chanzo cha migogoro kuhusu gesi asili,” alisema.
Alisema kuwa ikiwa Spika amebadili uamuzi wa kuunda kamati ya kwenda Mtwara alipaswa aunde Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ili ipitie vielelezo kubaini usahihi wa maelezo hayo ya waziri mkuu bungeni katika hali ya sasa.
Mnyika aliongeza kuwa waziri mkuu hajatoa maelezo kamili kuhusu mipango ya matumizi ya gesi asili katika eneo la viwanda Bagamoyo na ujenzi wa Bandari ya Mbegani.
“Spika wa Bunge atumie mamlaka yake kuelekeza kamati mojawapo ya kudumu ya Bunge kushughulikia suala la gesi asili kama nilivyoomba katika barua zangu kwake za Oktoba 2012 na Januari 2013, ambazo hadi sasa hazijapatiwa majibu,” alisema Mnyika.

Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Shein Azindua Sherehe za Madhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM

  Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akivalishwa skafu na  Kijana Chipukizi,Pili  Hassan Suluhu, wakati alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo asubuhi,kwa ajili ya Uzinduzi wa Sherehe za Madhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM.
 Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,wakielekea katika jengo la  Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,kwa ajili ya kuweka saini kitabu cha wageni,wakati wa Uzinduzi wa Sherehe za Madhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM.


 Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi,waliohudhuria katika Uzinduzi wa Sherehe za Madhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM,zilizofanyika leo katika  viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

KIPANYA LEO

304851 329639433809444 913536318 n c848e

Kumi wafa kwa ajali ya boti Zanzibar


                                  Msemaji wa Mkuu wa Polisi nchini, Advera Senso 

Na:  George Njogopa-Mwananchi

BOTI ya abiria iliyokuwa ikitokea Pangani mkoani Tanga kwenda Zanzibar ikiwa na watu 32 juzi usiku ilizama katika eneo la Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Zanzibar ambapo watu 10
wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha.

Taaarifa zilizofikia gazeti hili jana jioni zilisema kati ya abiria 27 na wafanyakazi watano waliokuwa kwenye boti hiyo, ni watu 20 tu waliokuwa wameokolewa wakati wengine 10 wakiwa hawajulikani walipo.

Msemaji wa Mkuu wa Polisi nchini, Advera Senso alisema jahazi liitwalo Sunrise liliondoka Tanga juzi saa 2:00 usiku kuelekea Zanzibar, lakini lilipigwa na dhoruba katika eneo la Nungwi.

“Mpaka sasa watu 22 wameokolewa akiwamo nahodha Abdallah Selemani, kumi wanatafutwa ijapokuwa wanahofiwa kuwa wameishakufa. Kati ya hao ni watoto watatu na watu wazima ni saba,”alisema Senso katika ujumbe alioutuma kupitia simu yake ya mkononi.

Aliendelea: “Boti kutoka Tanga ipo kwenye eneo la tukio kusaidia uokozi na wakazi wa Kaskazini Unguja wamepokea watu waliookolewa na kuwapa huduma. Taarifa zaidi tunaendelea kufuatilia Tanga na Zanzibar”.

Hata hivyo idadi ya watu waliookolewa kwa mujibu wa Senso ilitofautiana na ile iliyokuwa imetolewa awali na Kamanda wa Wanamaji na Bandarini Zanzibar, SP Martin Lisu aliyesema juhudi za kuwaokoa abiria hao zilikuwa zikiendelea na kwamba waliokuwa wamepatikana wakiwa hai ni watu 21.
Lisu alisema abiria hao walionusurika kifo walipelekwa hospitalini kwa ajili ya kuchunguzwa afya zao na wengine walipatiwa huduma za kwanza kutokana na mshtuko walioupata.

“Kusema kweli tulifanikuwa kuwaokoa abiria 21 na wengine siwezi kusema kama wamezama ila nachoweza kusema ni kwamba bado hatujawapata,” alisema Kamanda Lisu na kuongeza:
“Taarifa nilizonazo ni kwamba, hii boti ilikuwa ikitokea Pangani, ilipofika eneo la Nungwi ikakubwa na dhoruba kali na kisha kuanza kupoteza mwelekeo”.
Eneo la Nungwi
Eneo la Nugwi lina historia ya kusababisha ajali za mara kwa mara na mara ya mwisho ndiko ilitokea ajali ya meli ya MV Spice Islander iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 400 mwaka 2011.

Ajali hiyo ilielezwa kusababishwa na uzembe wa baadhi ya watendaji ikiwemo kukosekana kwa ukaguzi kabla ya meli hiyo kuondoka.Taarifa zilizema kuwa meli hiyo ilizidisha idadi ya abiria na mizigo hivyo ilipofika eneo la Nungwi ilizidiwa na kuanza kuzama.

Katika kujaribu kusaka ukweli wa mambo, Rais wa Zanzibar, Dk Ally Mohamed Shein aliunda tume maalumu kuchunguza mazingira yaliyosababisha ajili hiyo.
Ripoti ya tume hiyo ilifichua uzembe uliojitokeza kwenye mamlaka husika na kupendekeza hatua kadhaa ili kuimarisha hali ya usafiri kwenye maji.

Ajali nyingine kubwa ni ya meli ya MV Skagit iliyotokea mwaka jana ikiwa inakaribia katika bandari ya Zanzibar, ambayo hatua za awali za uokoaji zilishindikana na kusababisha vifo vya mamia ya watu.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 01, 2013