Pages


Photobucket

Sunday, February 15, 2015

BARAZA LA BIASHARA MKOA WA DODOMA LASISITIZA USHIRIKIANO BAINA YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI ILI KUONGEZA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUKUZA UCHUMI WA DODOMA


Mkuu wa Mkoa Dodoma na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa hotuba ya kufungua mkutano wa baraza hilo Mjini Dodoma Feb. 13,2015.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) Ndg. Raymond Mbilinyi akiwasilisha majukumu ya Baraza hilo katika kusaidia mabaraza ya biasara ya Mkoa na jinsi ya kukuza ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi wakati wa mkutao wa baraza la biashara la Dodoma Feb. 13, 2015.
Wajumbe wa baraza la biashara Mkoa wa Dodoma wakifuailia mada juu ya ushirikiano wa serikali na sekta binafsi na kuzalisha fursa za uwekezaji Mkoani Dodoma wakati wa Mkutano wa Baraza hilo Feb. 13, 2015.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) Manispaa ya Dodoma Ndg. Nobert Donald akiwasilisha changamoto zinazowakabili wamachinga wakati wa mkutano wa baraza la biashara Mkoa wa Dodoma Feb. 13, 2015.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara, wakulima na wenyeviwanda Mkoa wa Dodoma (TCCIA) Ndg. Faustine Mwakalinga akiwasilisha mada juu ya fursa za kipekee za uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma na Changamoto zilizopo wakati wa Mkutano wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma Feb. 13, 2015

Taarifa zilizopatikana kuhusu hofu ya uhalifu, ugaidi Tanga


Askari mmoja wa jeshi la wananchi ameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine wanne wa jeshi la polisi wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo kufuatia mashambulizi ya kurushiana risasi katika mapango kati yao na vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi.

Habari kutoka katika eneo la tukio zinadai kuwa vikundi hivyo vilikuwa ndani ya mapango huku askari wakiwa nje hatua ambayo imedaiwa kuwa majibizano ya risasi yalisababisha askari wa jeshi kupigwa ya tumboni na kuwahishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga bombo lakini baadae alifariki Dunia.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na ITV wameingiwa na hofu kufuatia tukio hilo huku baadhi yao wakidai kuwa wanashindwa kutoka katika nyumba zao kwa kuhofia usalama wao kufuatia milio ya risasi katika eneo la Amboni hasa nyakati za usiku .

Hata hivyo kamishna wa Polisi -Operesheni na mafunzo Paul Changonja akielezea tukio hilo amekiri kuwa askari wake watatu na mmoja wa jeshi la wananchi wamejeruhiwa kwa risasi wakati askari wake walipoingia katika mapango hayo ndipo mmoja kati ya wanakikundi hao aliporusha risasi na kuwajeruhi askari.

Hata hivyo jitihada za ITV kwenda katika eneo la tukio ziligonga mwamba baada ya askari polisi wa kikundi cha (FFU) kuweka ulinzi na kudai kuwa hatakiwi mwandishi wa habari kwenda katika eneo hilo huku mganga mkuu wa mkoa wa tanga Dr,Asha Mahita naye akitoa maelezo kama hayo kuwa waandishi wazuiwe wasiingie katika wodi ya galanosi kwa ajili ya kuwaona askari waliojeruhiwa.


  • --- Taarifa ya ITV



Askari sita wakiwemo wanne wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamejeruhiwa vibaya kwa risasi wakati wa mapigano baina yao na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati wa Msako Maalum wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye moja ya eneo la mapango ya Amboni.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, amebainisha hayo alasiri, wakati akitoa taarifa kwa wanahabari jijini Tanga kuhusu hali ya matukio ya uhalifu yanayoendelea jijini humo.

Amesema mapambano hayo yametokea muda mfupi tu wakati wa msako maalum wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye moja ya eneo la mapango ya Amboni, yaliyoko umbali wa kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Tanga.

“Baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wasiri wetu ndipo alfajiri ya leo (jana) askari wetu walienda eneo la tukio kwa lengo la kutafuta hizo silaha na ghafla wakavamiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliokuwa wamejificha”, alisema.

Alisema kujeruhiwa kwao kumetokana na mapambano ya kurushiana risasi yaliyodumu kwa dakika 15 alfajiri ya kuamkia leo katika mashimo ya mawe ambayo yako jirani na mapango ya Amboni.

Kamishna Chagonja alisema chanzo cha mapambao hayo, ni tukio la Januari 26 mwaka huu, wakati askari wawili walipovamiwa na watu wasiojulikana na kunyang’anywa bunduki mbili aiana ya SMG, zilizokuwa na risasi 60.

“Upelelezi wetu uliendelea baada ya tukio hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuwasaka na tukafanikiwa kupata wahalifu…jana asubuhi tuliarifiwa kwamba silaha hizo zimefichwa kwenye moja ya mapango ya Amboni na ndiko wakapeleka askari huko ili kuzitafuta,” alisema.

“Wakati askari hao wakiendelea kutafuta, ghafla walivamiwa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa wamejificha kwenye eneo lingine la pango hilo …ikalazimika wajibu mapigo,” alisema.

Kamishna Chagonja alisema baada ya kuzima mapigano, waliamua kuingia ndani ya mapango hayo na kukuta vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko, pikipiki moja, baiskeli tatu, silaha mbalimbali za jadi ikiwemo mishale, pinde , visu na mapanga lakini hawakufanikiwa kukuta mtu.

Akizungumzia kuhusu watu hao kwamba ni kikundi cha wahalifu wa Alshabab au la, alisema mpaka sasa Polisi haijabaini kutokana na ukweli kwamba katika opereshi hiyo hawajafanikiwa kukamata mtu ambaye wanaweza kumfananisha na magaidi hao.

“Msako wetu unaendelea tunaomba wananchi watoe ushirikiano… kwa ukweli ni mapema sana kuthibitisha kwamba hao wahalifu ni wa kikundi cha Al-Shabab kama inavyodaiwa mitaani, kwa sababu mpaka sasa hatujatambua sura zao na kubaini ni watu wa aina gani,” alisema.

Alisema askari waliojeruhiwa, wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo na hali ya afya zao inaendelea vizuri.

Hata hivyo taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika ndani ya Hospitali ya Bombo, imeeleza kwamba askari mmoja wa JWTZ amefariki dunia jana saa 8.30 mchana ingawa Chagonja amekataa kuthibitisha kifo hicho.

Licha ya kudai kwamba hali imerejea kuwa shwari, lakini mpaka sasa wako kazini na ulinzi umeimarishwa kuanzia katika eneo la Utofu lililoko umbali wa kilometa 5 kutoka mjini, ambapo askari wanaonekana kutaka kupata taarifa za kila mtu na magari yanayoendelea kutumia njia hiyo.

Mitaani hali ya ulinzi na usalama miongoni mwa wananchi katika halmashauri ya Jiji la Tanga, iliendelea kugubikwa na hofu kubwa na mashaka kutokana na mapigano yaliyokuwa yakisikika baina ya askari na kikundi cha wahalifu hao.

Mapigano hayo yalikuwa katika kitongoji cha Mikocheni kilichopo kata ya Kiomoni kwenye machimbo ya mawe ambayo yameambatana na eneo la Mapango ya Amboni.

Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa kata hiyo iliyoko umbali wa kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Tanga, walianza kuona vurugu za magari ya askari wa kutuliza ghasia pamoja na JWTZ wakikatiza katika maeneo hayo huku ikisikika milio ya risasi na vishindo vikubwa.

Agata Juma, mkazi wa Kiomoni Majimoto, alisema vurugu hizo zilisababisha wapate hofu na kukumbuka tukio la hivi karibuni la mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono, uliotokea wiki tatu zilizopita kwenye eneo hilo.

“Yani hatuelewi kinachoendelea, maana askari hawazungumzi kitu na wananchi bali tunasikia sauti za ving’ora pamoja na mishindo ya vitu kama mizinga mikubwa ikilia … mambo hayo yanafanyika huko jirani na mampango ya Amboni,” alidai.

Naye Jumaane Amboni, alidai usiku kucha hawakupata usingizi kutokana na hofu, hasa baada ya kupata taarifa ambazo hata hivyo hazijathibitishwa na Polisi, kwamba eneo hilo limevamiwa na kikundi cha Waislamu wenye itikadi kali wa Al-shabab.

“Usiku wa kuamkia leo mambo yalikuwa magumu sana mana tumesikia risasi zikirindima na vishindo kama vya mizinga vikilia mara kadhaa pasipo kuelewa cha kufanya…. tumeamua kukaa ndani na kujifungua.

“Tunachofanya hapa ni kujaribu kukusanya mahitaji ya muhimu kama chakula na vitu vingine, kwa sababu hatuelewi hayo mapigano yataisha lini hasa ikizingatiwa kwamba eneo walilojificha ni ndani ya sehemu ya mapango ya mawe ambayo hayatumiki kabisa,” alisema.

Hata hivyo baadhi ya wakazi katika maeneo ya katikati ya Jiji la Tanga, ingawa shughuli zinaendelea kama kawaida lakini wamekuwa katika hali ya wasiwasi.
  • --- Taarifa ya HabariLeo


Balozi wa promosheni ya JayMillions awalipia nauli abiria wote

Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud "Zembwela"(kushoto)akimkabidhi fedha mmoja wa abiria wa basi linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano cha ubungo kwenda Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwalipia abiria wenzake nauli ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda.

  • Awataka watanzania kuchangamkia fursa
  • Ahimiza wateja kuangalia kama namba zao zimeshinda kila siku
  • Atembelea stendi ya mabasi Ubungo na kumwaga ofa kwa wasafiri

Balozi wa promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud‘Jaymillions’ mwishoni mwa wiki alikuwa kivutio kwa wananchi wengi alipotembelea eneo kituo cha mabasi cha Ubungo Mawasiliano na kuwahimiza wananchi kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika maisha yao ambapo pia alitoa ofa ya kuwalipia nauli wasafiri waliokuwa wamepanda mabasi kuelekea sehemu mbalimbali za jiji waliokuwa kituono hapo.

Ziara hiyo ilileta msisimko mkubwa wa wananchi waliokuwa eneo hilo ambapo baadhi yao walilazimika kuacha shughuli zao kumwangalia balozi huyo na wengine kuomba kupiga naye picha ikiwemo waliompiga picha kwa kutumia simu zao zao mkononi.

Balozi huyo alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa wanaotumia mtandao wa Vodacom wahakikishe kila siku wameangalia kama namba zao zimeshinda mamilioni ya fedha kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544 na aliwataka wale ambao hawako kwenye mtandao wa Vodacom wajiunge nao ili washiriki kwenye promosheni hii kubwa iliyolenga kubadilisha maisha ya watanzania wengi kuwa mamilionea.

“Leo nimewafuata huku kuwapatia ofa na kuwafikishia ujumbe kwa maana naona wengi wenu bado hamjachangamkia fursa hii kwa kuangalia iwapo namba zenu zimeshinda kila siku,bado tunayo mabilioni ya fedha kwa ajili yenu hivyo changamkia fursa hii muweze kujishindia mamilioni ya fedha katika kipindi hiki cha promosheni.Kila siku kuna mshindi 1 wa shilingi milioni 100,000,washindi 10 wa milioni 10 na washindi 100 wa shilingi milioni 1 hivyo kazi kwenu na Vodacom”.Alisema

Naye Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi uliopita mteja mmoja ameishajishindia milioni 100, wateja 2 wamekwishajishindia milioni 10 na wateja kumi na moja wameisha jishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu ya wateja wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

Wateja wa Vodacom ambao tayari wamejipatia mamilioni ya fedha kupitia promosheni hii ni Uwezo Magedenge mfanyakazi nyumba ya wageni wilayani Kilolo mkoani Iringa ambaye amejishindia milioni 100. Waliojishindia milioni kumi kila mmoja wao Hynes Petro Kanumba mkulima kutoka Inyonga mkoani Rukwa na James Mangu mfanyabiashara kutoka wilayani Magu

Washindi wa milioni moja ni Chiphold Wanjara mjasiriamali wa Kutoka Mwanza ,Janeth Nganyange wa Njombe,Evarista Minja mwanafunzi kutoka Mwanza,Stanley Bagashe Mwalimu wa Shinyanga,Ramadhani Maulid Mkulima kutoka Dodoma, ,Lucas Masegese wa Shinyanga,Ayub Makonde mfanyabiashara wa Mbeya,Hyasinti Mlowe Fundi gereji kutoka Njombe,Florian Gwayu mchapishaji kutoka Arusha,Modesta Millanzi mjasiriamali kutoka Peramiho mkoani Ruvuma na Nobert Minungu mwanafunzi kutoka Mbwanga mkoani Dodoma.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo juma hili inaingia katika wiki ya nne na bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.”Alisisitiza.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam Mudy Seleman(kushoto)akikabidhiwa fedha kwa ajili ya nauli na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela” wakati wa kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisubiria usafiri katika kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)baada ya kuwalipia nauli wakati wa kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo hicho.

Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akitoa elimu kwa mmoja wa abiria wa basi liendalo Gongolamboto kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam juu ya Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo wateja wanatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda. 005.Baadhi ya abiria wakiwa na watoto wao katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam, wakifafanuliwa jambo na mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Joyce Mhina kuhusiana na Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo wakati Balozi wa promosheni hiyo alipoenda kituoni hapo kutoa elimu kuhusiana na promosheni hiyo na kuwalipia wasafiri wote bure wa daladala nauli kulingana na sehemu wanayo kwenda ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kushirikia katika promosheni hiyo.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(aliyesimama)akitoa elimu juu ya promosheni hiyo kwa abiria waliopanda daladala zinazofanya safari za mlandizi kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam na aliwalipia nauli abiria wote bure ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kushirikia katika promosheni hiyo.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Kondakta wa basi linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo kwenda Kawe jijini Dar es Salaam, Hamis Omari (kushoto)akikabidhiwa nauli ya abiria wote waliopanda gari lake na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kulia) wakati alipokuwa akihamasisha wateja wa kampuni hiyo kituoni hapo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda. Ambapo abiria wote waliokuwepo kituoni hapo walilipiwa nauli kulingana na safari zao.

Shirika la Equality For Growth lazindua Mradi wa Msaada wa kisheria

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  mradi wa msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani Lushoto mkoani Tanga jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita na Katibu Tawala wa wilaya hiyo (DAS), Josephine Kisigila. Mradi huo unaendeshwa na EfG.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akitoa hutuba fupi kwa mgeni rasmi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliopatiwa mafunzo hayo.
 Wanawake wa Wilaya ya Lushoto wakiwa kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa mradi huo na ofisi.
Viongozi mbalimbali waliojumuika kwenye uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (mbele katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wasaidizi hao wa kisheria na maofisa wa EfG.
 Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Shadrack (Channel 10), Nasra Abdallah (Tanzania Daima), Dotto Mwaibale (Jambo Leo na Mtandao wa www.habari za jamii.com na Sophia kutoka Televisheni ya Mlimani.
 Wanafunzi nao walijumuika kuona shughuli mbalimbali za uzinduzi huo hasa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani.
 Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.
 Zawadi zikitolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita.
 Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Mary Magigita akiwa ameshika mkungu wa ndizi aliozawadiwa. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Josephine Kisigila.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo (kushoto), akifurahi na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita baada ya kukabidhiwa machapisho mbalimbali ya EfG.
Maofisa wa EfG, Eva (kushoto) na Samora wakiwa katika maandalizi ya uzinduzi huo "Chezea EfG wewe"

Doto Mwaibale

WAJASIRIAMALI wanawake wametakiwa kutumia mafunzo ya usimamizi wa sheria katika masoko waliyopata kwa kuwaelimisha wengine badala ya kukaa nyumbani bila ya kutoa elimu hiyo.

Mwito huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto Dk.Hassan Shelukindo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mradi wa msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani humo  mkoani Tanga jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Jumanne Shauri. 


"Ninyi Wanawake wa Lushoto mmepata bahati kubwa ya kuletewa mradi huu pamoja na mafunzo haya mliyopata nawaombeni nendeni mkayafanyie kazi katika maeneo yenu" alisema Dk. Shelukindo

Alisema elimu waliyoipata ya msaada wa kisheria ni muhimu sana kusaidia jamii katika masoko na itasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijisinsia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), ambalo linaendesha mradi huo, Jane Magigita alisema lengo la mradi huo katika wilaya hiyo ni kuhamasisha na kulinda haki za wafanyabiashara iwanawake katika masoko kwa kuwapatia elimu ya sheria, biashara, elimu ya vicoba, elimu ya uongozi na usimamizi wa vikundi.

Alisema EfG ni shirika la pekee nchini linalotoa msaada wa kisheria kwa sekta isiyorasmi hivyo kuonesha ni kiasi gani sekta hiyo ilivyo sahulika.

Alisema EfG  inaendesha mradi huo katika masoko ya wilaya ya Lushoto pamoja na vikundi mbalimbali vya maendeleo na kuwa shirika hilo linawajibika kutoa mafunzo  ya siku 25 kwa wasaidizi 25 ambao watasambaza huduma sheria kwa jamii.

Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu tano ambapo kila awamu yatakuwa yanafanyika kwa  takribani siku tano.

" Shirika linawajibika kutoa mafunzo mafunzo mbalimbali kwa wafanyabiashara ikiwa na lengo la kuinua hali za wanawake wafanyabiashara sokoni kupitia mafunzo ya biashara, uundwaji wa vikundi vya Vicoba, mafunzo mbalimbali kwa watendaji na viongozi wa Halmshauri ya wilaya ya Lushoto kwa lengo la kuboresha hali za wafanyabiashara sokoni" alisema Magigita.

Alisema mpaka sasa shirika hilo limefanikiwa kuwapatia mafunzo ya sheria ya siku tano wasaidizi wa sheria 25, wanaume 8 na wanawake 17 kutoka katika masoko na wengine kutoka katika vikundi vya maendeleo ndani ya Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto.

Alisema pia wanakituo maalumu cha msaada wa sheria katika ofisi za EfG Lushoto ambapo wafanyabiashara mbalimbali wanaruhusiwa kupeleka matatizo yao ya kisheria kila siku za Jumatatu na Jumatano kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 10 jioni.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

HAPPY BIRTHDAY MR. REMIDIUS M.EMMANUEL


     Uongozi wa Blog ya MWEMA unapenda kukupongeza na kukutakia maisha  marefu  Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Youth Empowerment and Support (YES) na  Afisa Tarafa  (Tarafa ya ITISO) Wilaya ya Chamwino - Dodoma  Bw. Remidius Emmanuel kwa kutimiza miaka kadhaa. 
  Mungu akupatie Maisha Marefu yenye Baraka

Hongera  Mr. Remidius