Pages


Photobucket

Sunday, October 20, 2013

MKUU WA WILAYA YA CHAWINO AIPONGENZA AIRTEL

                Mh. Mkuu wa Wilaya  ya Chamwino Bi.Fatma  S. Ally


Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatma S. Ally  Ameipongeza kampuni ya simu ya  Airtel  kwa  kutoa msaada wa vitabu  katika shule ya sekondari ITISO. Mkuu huyo amesema hayo wakati akitoa hotuba yake  katika Mahafali ya  Kidato cha nne  iliyofanyika   Shule ya Sekondari ITISO  Tarehe 18/10/2013 " Nimefurahi kusikia  juhudi zilizo onyeshwa na  Kampuni, ya simu ya  Airtel kwa  kutoa vitabu vya sayansi katika shule hii,hivyo nichukue  fursa hii kwa upekee kuipongeza kampuni hii  ya simu" Alisema Bi. Fatma.

Katika hatua nyingine aliwataka wanafunzi wa  kidato cha nne kujikita zaidi katika maadalizi ya mitihani iliyoko mbele yao na kuongeza kuwa bado wanayo nafasi ya kupitia vyema kile walicho kisoma  ili waweze kuwa katika hali nzuri ya kujibu mitihani yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM  Wilaya ya  Chamwino  Mh. Joel Mwaka  alisema  wazazi bado wanayo nafasi kubwa kuhakikisha watoto wao  wanafanya vema katika masomo yao kwa maana ya kufatilia kwa ukaribu maendeleo yao  kitaaluma.Jukumu la  ufaulu kwa mwanafunzi  linahusisha Mwanafunzi mwenyewe,Mwalimu pamoja na Mzazi,Alisema Bw. Joel


      Mkuu wa Shule ya Sekondari  Itiso  Bw. Andrea  A. Mauki  Akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi
     Baadhi  ya wahitimu wa Kidato cha Nne  wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Mgeni Rasmi.




         Mkuu wa Shule ya ITISO Akikabidhi Risala kwa Mgeni Rasmi
                       Mwenyekiti wa Kijiji cha ITISO akizungumza  wakati wa mahafali hiyo.


                         Afisa Elimu (Sekondari) wa  Halmashauri ya Chamwino  Bi.Nyemo  Masimba
        Mkuu wa  Shule  ya  Sekondari ya ITISO Bw. Andrea  A. Maukia  kifuatilia kwa umakini Matukio mbalimbali katika Mahafali hayo 
           Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  CCM (Wilaya ya Chamwino) Mh. Joel Mwaka
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Ndugu Raymond  Mwakifamba akizungumza katika mahafali  hayo


   Chereko na shangwe kwa Wahitimu...!!!!!

Sunday, October 13, 2013

MTANGAZAJI WA ITV/RADIO ONE UFOO SARO APIGWA RISASI, AMPOTEZA MAMA MZAZI

Ufoo Saro (kulia) aliyepatwa na mkasa leo hii
HABARI zilizotufikia leo  zinasema mtangazaji wa kituo cha ITV, Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa risasi, huku mama yake mzazi akipoteza maisha baada ya mtu anayedakiwa kuwa mchumba wake au mumewe kuwafyatulia risasi katika ugomvi wa kimapenzi.

Taarifa zinasema kuwa mchumba wa mtangazaji huyo aliyetajwa kwa jina la Ansel aliyekuwa nchini Sudan kikazi alitua nchini jana na kufikia kwa Ufoo lakini kukatokea mzozo ambao haukupata suluhisho.

Hivyo wawili hao waliongozana hadi kwa mama wa mtangazaji huyo kutafuta suluhu, asubuhi hii na kwa bahati mbaya hali ilikuwa tete na ndipo kijana huyo alipotoa bastola aliyokuwa nayo na kumtwanga mama mtu risasi ya kichwa iliyomuua papo hapo.

Kama hiyo haikutosha inaelezwa jamaa huyo alimtwanga risasi Ufoo kifuani na nyingine mguuni na kudhani amemuua kabla ya yeye mwenyewe kujilipua mwenyewe kwa risasi ya kidevuni na kumuua.

Tayari miili ya watu hao wawili yaani mama yake Ufoo na jamaa huyo imepelekwa Muhimbili sambamba na mtangazaji huyo anayeelezwa yupo katika hali mbaya kwa ajili ya kuhifadhiwa na matibabu zaidi.

Haifahamiki chanzo cha mauaji hayo licha ya kudaiwa huenda ni ugomvi wa kimapenzi na haifahamiki jamaa huyo huko Sudan anakodaiwa kuwa alikuwa akifanya kazi UN alikuwa kama nani japo inaelezwa huenda alikuwa mwanajeshi ambapo kabla ya kwenda huko aliwahi kuwa mpiga picha wa ITV na kufanya kazi Mahakama ya Kimataifa ya Arusha kabla ya kuomba kazi UN.
MICHARAZO inaendelea kufuatia kwa kina taarifa hii na itawafahamisha. Pia inamuombea kila la heri na salama mtangazaji huyo aweze kupona katika mkasa uliopata na kumpoa pole kwa msiba uliompata kwa kumpoteza mama yake mzazi.

Rais Jakaya Kikwete Aagana na Balozi wa Oman nchini Anayemaliza muda wake.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Oman nchini anayemaliza muda wake Mhe.Yahya Mousa Al Bakary ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Balozi huyo alikwenda ikulu kumuaga Rais
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Oman nchini anayemaliza muda wake Mhe.Yahya Mousa Al Bakary ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Balozi huyo alikwenda ikulu kumuaga Rais.Picha na Freddy

Kuhusu Rais Kenyatta kutohudhuria kesi Mahakamani The Hague


Uhuru Kenyatta 11
Imefahamika kwamba Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hatohudhuria vikao vya kesi dhidi yake kwenye Mahakama ya ICC The Hague haya yakiwa ni maafikiano ya viongozi wa Afrika kwenye kongamano la Umoja wa Afrika Ethiopia.
Mkutano huo unakusudia kuwatuma Marais watano wa Afrika nchini Uholanzi ili kuitaka Mahakama hiyo kuahirisha kesi ya rais Kenyatta itakayoanza November 12 ambapo pia mkutano huu umesema hata Naibu Rais William Ruto hafai kushtakiwa kwenye Mahakama hiyo ya ICC.