Pages


Photobucket

Sunday, March 17, 2013

President Obama's Bilateral Meeting with His Majesty Sultan of Brunei

RAIS KIKWETE KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA HOSPITALI YA KAIRUKI, DAR ES SALAAM, LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo Machi 16, 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Mama Koku Kairuki akimkabidhi tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, na viongozi wa hospitali ya Hubert Kairuki wakiwa katika picha ya pamoja na vijana waliozaliwa katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita leo Machi 16, 2013
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Msanii Mrisho Mpoto akiburudisha wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Seehemu ya wageni waalikwa na wanafunzi na wafanyakazi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.PICHA NA IKULU.

KIJANA ALIYEANDAA VIDEO YA LWAKARE NAYE AMEKAMATWA


Anayedaiwa  kupiga  video  iliyosababisha   kukamatwa kwa  Rwakatale (  pichani ) maarufu kwa jina la  Ludovik Joseph amekamatwa  mkoani Iringa .kijana   huyo anadaiwa kuwa ni mhitimu  wa  chuo kikuu cha DUCE

-------------------------------- Ndugu zangu,
Usiku huu nikiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wangu pale Highlands Hall Iringa nilifikiwa na habari kuwa Kijana Ludovick amekamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda.


Namfahamu kijana Ludovik tangu  akiwa Chuo Kikuu ( DUCE). Ni mmoja wa Watanzania wengi  walionifahamu kupitia kazi zangu za magazetini.


Kwangu Ludovick ni kijana mtaratibu na mpole sana, na hata niliposikia habari hizi  kwa namna fulani nimeshtushwa nazo. 


Ludovick ambaye amekuwa akiishi Dar ni mmoja wa vijana waliokuwa wakinisaidia kwa kujitolea kwenye kazi zangu za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii. Amekuwa na mchango mkubwa, na hata katika miezi ya karibuni,ndiye yeye aliyekuwa akifanya kazi ya kuingiza magazeti  kwenye Mjengwablog kila asubuhi.

 Akiwa Dar na mimi nikiwa Iringa, Ludovick hakuwa mwajiriwa wangu kama wanavyodhani wengine, bali , amekuwa ni mmoja wa vijana waliokuwa tayari kunisaidia kwa kazi za hapa na pale ikiwamo kunipelekea invoice kwa watangazaji kwenye Mjengwablog.

Mara nyingi nimekuwa nikimtambulisha kama ' Msaidizi wa Mwenyekiti'.

Na jana nilimwomba aje Iringa aniletee vitabu vyangu vya invoice na risiti kwa vile nilitarajia ugeni wa kutoka TMF- Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari. Kwamba huenda vitabu hivyo vingehitajika wakati wa mazungumzo  na watendaji wa TMF yaliyofanyika leo asubuhi.


Hata hivyo, katika hili lililomtokea, siwezi hapa kumtetea wala kumtia hatiani. Maana, naye ni binadamu kama wengine, siwezi kusema kuwa ninamfahamu sana.  Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama , nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima.


 Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo. 


Ni mimi:
MAGID MJENGWA

Credit: mjengwablog

Tuesday, March 5, 2013

MARA FOUNDATION YAJIDHATITI KUIBUA VIJANA WAJASIRIAMALI WATAKAOSAIDIA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA.


Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi akisikiliza mawazo ya mmoja wa vijana wajasiriamali mwenye nia ya kukataka kukuza biashara yake na kuifanya kuwa endelevu wakati wa uzinduzi wa Mara Foundation ambao uliotoa fursa ya washiriki kuzungumza na wafanyabiashara waliopiga hatua na wenye uzoefu katika kuendesha biashara zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga akimsikiliza mmoja wa washiriki ambaye ni mjasiriamali anayechipukia aliyetaka kupata uzoefu na mawazo zaidi jinsi ya kuendesha biashara yake.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali akimsikiliza mjasiriamali mdogo mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa kimataifa.
Ma-Mentors waliokuja kuzungumza na wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya kuwapa mbinu mbalimbali za kibiashara na kuwaongoza kufikia malengo yao.

Taasisi ya Mara Foundation ilianzishwa na Ashish Thakkar ambaye ndie mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Mara Group. Ashish alitumia muda wake mwingi katika kutimiza malengo ya Taasisi hiyo kwa kuwa alikuwa na imani na wajasiriamali na kuendeleza biashara ndogo.
Tangu mwaka 2009 Taasisi hiyo ililenga mtazamo wake na imefanya vizuri sana nchini Uganda, Tanzania, Kenya na Nigeria katika muelekeo huo. Kuanzia mwaka 2013 mikakati ya taasisi ya Mara Foundation inaendelea kukua katika nchi za Kusini mwa Jangwa la sahara huku ikiendelea kuongeza wigo wake katika nchi nyingine duniani. Mara Foundation inafanya kazi ya kubuni na kukuza uchumi endelevu na kufungua fursa endelevu kwa vijana wamiliki wa biashara za kati kwa kupitia vituo vya uwezeshaji vya Mara Launchpad na Mara Launch Fund.
Pichani juu na chini ni Washiriki na wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kabla ya mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu kuzindua Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Tanzania Nina Werner (kulia) akizungumza machache kuhusiana na malengo ya Taasisi yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mh. Dkt. Mary Nagu kuizindua rasmi.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akizungumza wakati kuzindua taasisi ya Mara Foundation ambapo amewataka vijana wajasiriamali kutumia fursa ya taasisi hiyo kujijenga kibiashara Taasisi ya Mara Foundation yenye makao yake makuu jijini Dubai sasa imejikita katika nchi za Afrika ambazo ni Uganda, Tanzania, Kenya na Nigenia kwa lengo kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuwezeshwa kimuongozo na kuwa wafanyabiashara wakubwa ambao wataweza kutoa ajira kwa watu wengine.
Washiriki na wageni waalikwa wakifurahi jambo wakati mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu akitoa risala kwenye uzinduzi wa Taasisi ya Mara uliofanyika hivi karibuni kwenye jengo la Mayfair Plaza.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akikata utepe kuzindua rasmi taasisi hiyo yenye matawi 28 barani Afrika. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Nina Werner.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Wageni waalikwa wakishangilia kwa makofi.
MC wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Problem Solved Eric Mutta akimkabidhisha Mjasiriamali mdogo Peter Christopher kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (katikati) atakayekuwa mshauri wake wa kibiashara kwa muda wa miezi sita ijayo.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali (katikati) akimpokea mmoja wa wajasiriamali waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation kwa lengo la kuhakikisha anatimiza malengo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga (kushoto) akipata picha ya ukumbusho na kijana aliyemchagua kumsaidia kimawazo na kumwongoza kwa muda wa miezi sita ijayo mpaka kufikia lengo lake.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation uliofanyika hivi karibuni Mayfair Plaza.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) na Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mara Foundation.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha (kulia) na Mkurugenzi wa man Magazine Dismas Massawe (katikati) katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Mara Foundation.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA KIVUKO CHA MV MUSOMA LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Kivuko cha MV Musoma, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara. Kutoka (kulia) kwake ni mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Bw. John
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi uzinduzi wa Kivuko cha Mv Musoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013, kijiji cha Kinesi Wilayani Rorya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akibonyesha kitufye kupiga alam, kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko cha Mv. Musoma, wakati wa uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013 katika kijiji cha Kinesi. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akipiga makofi kufurahia uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakiwa ndani ya Kivuko cha Mv. Musoma baada ya kuzinduzliwa rasmi na Makamu wa Rais, leo Feb 5, 2013 wilayani Rorya kijiji cha Kinesi mkoa wa Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa MKoa wa Mara, John Tupa, pamoja na viongozi wa Chama na Serikali, wakiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu baada ya uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na viongozi wa Chama na Serikali, wakati akitoka kukagua Kivuko cha Mv. Musoma, baada ya kukizindua rasmi leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi wilayani Rorya. Picha na OMR.

Saturday, March 2, 2013

HUYU NDIYE "SADIFA HAMIS" MKT WA UVCCM (T) ALIPOKUWA ZIARANI MKOANI MOROGORO


MWENYEKITI WA  UVCCM (T)  BW, SADIFA HAMIS


Vijana machacahari Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walioihama Chadema hivi karibuni, wakiserebuka nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro, baada ya msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa,  Sadifa Hamis Juma kuwasili kwenye ofisi hiyo, Februari 28, 2013 kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.





Sadifa akipatiwa burudani ya shairi na mmoja wa waghani maarufu wa mashairi mkoani Morogoro.Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda


Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis Juma akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda wakati wa mkutano wa ndani kati ya Mwenyekiti huyo na wajumbe wa Baraza la Vijana mkoa wa Morogoro


Mkuu wa Utawala wa UVCCM Taifa, Abdallah Mpokwa akitoa utambulisho wa watu walioambatana na Sadifa kwenye msafara huo, katika ukumbi wa CCM mkoa wa Morogoro


Kada wa CCM aliyehamia kutoka Chadema hivi karibuni, Mtela Mwampamba akisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini.


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Juma Borafya akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho cha ndani. Wapili kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro mjini, Ali Issa, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Taifa, Mfaume Kizigo na Sixtus Mapunda


VIVA VIJANA VIVAAAA!!!!!, Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Sixtus Mapunda akiongoza salaam maalum kwa Vijana wa UVCCM ukumbini. Pamoja naye kutoka kulia ni Katibu wa CCM Morogoro, Ali Issa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Mfaume Kizigo. Walioketi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Harrieth Sutta na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa.


VIVAAAA!!!, vijana wakiitikia salam ya Sixtus ukumbini, baadhi yao ni Shonza na Abubakar Assenga


VIVAAAA, VIVAAAA!!!!, Vijana wakiitikia  salam


Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Morogoro Herieth Sutta akimkaribisha Sadifa kuzungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Sixtrus Mapunda


 NAFURAHI KUWA NA WEWE! Sadifa akimwambia Sixtus Mapunda kabla ya kuanza hotuba yake ya mkutano huo wa ndani uliofanyika Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro


Sadifa akizungumza kwenye mkutano huo wa ndani


Sadifa akisisitiza jambo


Na kusisitiza zaidi


Sadifa akizidi kusisitiza hotuba yake huku viongozi wakiwa makini kumzikiliza



 "Wapendeni waliowapinga wakati wa uchaguzi" msiwanunie, kama mtu hakukuunga mkono leo kwa hili ipo siku atakuunga kwa jengine", akasema


Sadifa akitoka na wenyeji wake ukumbini