Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Lawrence Masha ameibuka kidedea akiwashinda wapinzani wake, Biku Kotecha
na James Bwire katika uchaguzi wa mjumbe wa Nec baada ya kuwashinda
washindani wake. Mwenyekiti: Kada wa siku nyingi wa CCM, Raphael
Shilatu ameshinda nafasi hiyo akiwashinda washindani wake, Yahya
Nyaonge, Joseph Bupamba na Mashaka Kaguna.
Songea Mjini
Nec: Kwa upande wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Msimamizi wa Uchaguzi huo, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho alimtangaza Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mshindi wa Mjumbe wa Nec.
Mwenyekiti: Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya imechukuliwa na Gerod Muhenga.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa: Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa ni Anusiatha Ngatunga, Andrew Chatwanga , Charles Muhagama, Consolatha Kilowoko na Mathias Nyoni.
Dk Emmanuel Nchimbi
Morogoro Mjini
Nec: Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ameibuka mshindi wa nafasi hiyo. Mwenyekiti: Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Fikiri Juma ametetea chama hicho baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi uliofanyika jana.
Mh. Abdulaziz Abood
Iringa Mjini
NEC: Katika nafasi hiyo Mahamoud Madenge alishinda kwa kupata kura 281, huku akiwabwaga Vitus Mushi Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Enock Ugulumo na Michael Mlowe.
Nafasi ya Mkutano Mkuu wa Taifa: Katika nafasi hiyo ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela aliibuka kidedea. Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa CCM Iringa mjini, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Daudi Yasin aliwataja wengine walioshinda nafasi hiyo inayohitaji wajumbe watano kuwa ni Salim Abri (Asas) Diwani wa Viti Maalumu, Agusta Mtemi, Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi na Fatuma Ngole. Mwenyekiti: Mwenyekiti wa zamani wa CCM Wilaya Iringa Mjini, Abeid Kiponza aliibuka mshindi na kutetea nafasi yake huku akimshinda mpinzani wake ambaye ni
Katibu Mkuu wa Soka Mkoa wa Iringa, Eliud Mvela. Aliwataja wajumbe wawili wa halmashauri kuu kundi la wazazi kuwa ni Alli Mbaya na Shadrack Mkusa. Walioshinda nafasi hiyo kundi la wanawake ni Nikolina Lulandala ambaye ni Diwani wa Kata ya Gangilonga, Ashura Jongo na Halima Msanya. Upande wa vijana walioshinda ni Ally Simba, Salum Kaita, Mwaija Mwinyikayoka na Crala Shirima.
Kwa upande wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa, wagombea wawili ambao ni Zainab Kufakunoga na Chiku Masanja ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanawake, Iringa mjini walipita bila kupingwa.
Mh. Fredrick Mwakalebela